Je Mtume (Saw) Alifasiri Quran na Akabainisha Maana Yake?

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah,

Imeelezwa katika kitabu cha Shakhsiyyah Islamiyyah juzuu ya tatu katika mada “Kupatikana kwa hakika za kisharia”, maelezo yenyewe ni: (…Lililothibiti ni kwamba Mueka sharia ameusimamisha ummah juu ya kunukulu majina hayo kutoka

katika maana zake za kilugha kwenda kwenye maana mpya iliyoyawekea sharia na hilo ni kwa kubainisha Mtume (SAW) maana hizi. Allah Mtukufu anasema: “Na tumekuremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu kile walichoteremshiwa”  na kusudio ni uwabainishie maana yake, na katika hizo maana ni maana za majina ya kisheria. Na Mtume (SAW) amesema: “Swalini kama mlivyoniona mimi naswali”. Ameitoa Bukhari. Basi huwa amewakalifisha amali na amewafahamisha hizo amali, hakuwakalifisha lile wasilolifahamu).

Je kutokana na hili tufahamu kwamba Mtume (SAW) ameifasiri Quran na amebainisha maana yake? Au tafsiri yake imefungika na kubainisha maana ya majina ya kisheria?

Allah akulipe kheri.

Jawabu:

Waalaykumu Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,

Ili kueka wazi jawabu naeleza mambo yafuatayo:

Kwanza: Swali lako linarejea kwenye kilichoelezwa katika Shakhsiyyah ya Tatu:

(Lililopo ni kwamba majina ya kisharia ni wakia ya maneno ya sharia na yapo kwa sifa yake kuwa ni hakika zenye kutofautika na hakika za kilugha, nayo ni maneno waliyoyaweka warabu. Ikaja sharia ikayanukulu kuyapeleka kwenye maana nyengine na yakawa mashuhuri kwa maana hiyo. Na kuyanukulu huko sio kuwa ni kwa kuwa mafumbo (majaz) bali ni kuwa kunukulu hakika za kimazoea (alhakiikatul ‘urfiyyah), kwa sababu sharia haikuyanukulu kwenda kwenye maana ya pili kwa mahusiano (lil-‘alaqah) kama ilivyo sharti ya fumbo (majaz), zaidi ni kwamba yamekuwa mashuhuri katika hiyo maana ya pili. Na fumbo (majaz) ni neno lililowekwa kwa ajili ya maana fulani kisha likanukuliwa kwenda kwenye maana nyengine kwa sababu ya mahusiano na wala si mashuhuri kwa hiyo maana ya pili, yaani haijatambulikana sana. Kwahivyo haiwi kunukulu jina la kisharia kwenda kwenye maana ya pili ambayo imewekwa na sharia kwa kuwa ni fumbo (majaz), haiwi hivyo kwa njia yoyote ile, bali ni kwa kuwa ni hakika ya kisharia…

Lililothibiti ni kwamba Mueka sharia ameusimamisha ummah juu ya kunukulu majina hayo kutoka katika maana zake za kilugha kwenda kwenye maana mpya iliyoyawekea sharia na hilo ni kwa kubainisha Mtume (SAW) maana hizi. Allah Mtukufu anasema: “Na tumekuremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu kile walichoteremshiwa”  na kusudio ni uwabainishie maana yake, na katika hizo maana ni maana za majina ya kisheria. Na Mtume (SAW) amesema: “Swalini kama mlivyoniona mimi naswali”. Ameitoa Bukhari. Basi huwa amewakalifisha amali na amewafahamisha hizo amali, hakuwakalifisha lile wasilolifahamu).

Pili: Mtume (SAW) kubainisha yale yaliyomo katika Quran Tukufu, huko si kwa ajili ya maana ya kisharia tu humaanisha Sunna kukifafanua Kitab katika yafuatayo:

1-Kufafanua kilichoelezwa na Quran kijumla jumla: Na katika hilo ni kwamba Allah Mtukufu ameamrisha swala katika Quran bila ya kubainisha nyakati zake, nguzo zake, na idadi ya rakaa zake. Sunna ikabainisha hayo. Kasema Mtume (SAW):

«صَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي»

“Swalini kama mulivyoniona mimi naswali”. Imetolewa na Bukhari…

Kisha Mtume (SAW) kwa vitendo vyake akabainisha kwa Waislamu ufafanuzi wa namna ya kuswali katika aliyoyapokea Abu Humaid Al-Saidy (RA):

« كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلَاةِ اعْتَدَلَ قَائِمًا وَرَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ قَالَ اللَّهُ أَكْبَرُ وَرَكَعَ ثُمَّ اعْتَدَلَ فَلَمْ يُصَوِّبْ رَأْسَهُ وَلَمْ يُقْنِعْ وَوَضَعَ يَدَيْهِ عَلَى رُكْبَتَيْهِ ثُمَّ قَالَ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ وَرَفَعَ يَدَيْهِ وَاعْتَدَلَ حَتَّى يَرْجِعَ كُلُّ عَظْمٍ فِي مَوْضِعِهِ مُعْتَدِلًا ثُمَّ أَهْوَى إِلَى الْأَرْضِ سَاجِدًا ثُمَّ قَالَ اللَّهُ أَكْبَرُ ثُمَّ جَافَى عَضُدَيْهِ عَنْ إِبْطَيْهِ وَفَتَخَ أَصَابِعَ رِجْلَيْهِ ثُمَّ ثَنَى رِجْلَهُ الْيُسْرَى وَقَعَدَ عَلَيْهَا ثُمَّ اعْتَدَلَ حَتَّى يَرْجِعَ كُلُّ عَظْمٍ فِي مَوْضِعِهِ مُعْتَدِلًا ثُمَّ أَهْوَى سَاجِدًا ثُمَّ قَالَ اللَّهُ أَكْبَرُ ثُمَّ ثَنَى رِجْلَهُ وَقَعَدَ وَاعْتَدَلَ حَتَّى يَرْجِعَ كُلُّ عَظْمٍ فِي مَوْضِعِهِ ثُمَّ نَهَضَ ثُمَّ صَنَعَ فِي الرَّكْعَةِ الثَّانِيَةِ مِثْلَ ذَلِكَ» هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ

“Mtume (SAW) alikuwa anaposimama kuswali anabakia kuwa amesimama na ananyanyua mikono yake mpaka inakabili mabega yake, akitaka kurukuu ananyanyua mikono yake mpaka inakabili mabega yake , kisha husema Allahu Akbar, na hurukuu kisha hutulia hakiinamishi kichwa chake wala hakiinui na huweka mikono yake kwenye magoti yake, kisha husema sami’allahu liman hamida  na hunyanyua mikono yake na hutulia mpaka kila unarejea kila mfupa kwenye mahali pake hali yakuwa ametulia, kisha huporomoka ardhini kusujudu kisha husema Allahu Akbar  kisha huweka mbali sehemu zake za juu za mikono (‘adhud) kutoka kwapa zake na hudhihirisha vidole vya miguu yake miwili, kisha huupinda mguu wake wa kushoto na huukalia, kisha hutulia mpaka kila mfupa unarejea kwenye mahali pake hali ya kuwa ametulia, kisha huporomoka kusujudu kisha husema Allahu Akbar  kisha hupinda mguu wake na kukaa na kutulia mpaka kila mfupa hurejea mahali kwenye mahali pake, kisha huinuka, kisha hufanya tena kama hivyo katika rakaa ya pili”. Ameitoa Tirmidhi na akasema hadithi hii ni hasan na sahih

2- Kukieleza kitu kuwa maalumu kutoka katika kitu kilichoelezwa kwa ujumla (Takhswiisu ‘aamuhu): Katika Quran kuna yaliyoelezwa kwa ujumla (‘umuumaat) na Sunna ikaja kuyaeleza yaliyo maalumu kutoka haya ya ujumla. Na katika hayo ni kwamba Allah Mtukufu ameamrisha watoto wawarithi wazazi wao kwa namna aliyoibainisha katika kauli yake Allah Mtukufu:

﴿يُوصِيكُمُ اللَّهُ فِي أَوْلَادِكُمْ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْ

“Allah anakuusieni kwa watoto wenu kuwa mtoto wa kiume anarithi fungu la watoto wawili wa kike”.

 Hii ni Aya, na hukmu hii ni ya ujumla (‘aam) kwa kila baba anaerithiwa na kwa kila mtoto anaerithi. Sunna ikaja kueleza baba maalumu wanaorithiwa kuwa sio Mitume, kwa kauli yake (SAW):

«لاَ نُورَثُ، مَا تَرَكْنَا صَدَقَةٌ»

“Haturithiwi, tunachokiacha ni sadaka”. Ameitoa Bukhari na Muslim. Na Sunna pia ikaeleza mwenye kurithi maalumu kuwa si muuaji kwa kauli yake (SAW):

«.. وَلاَ يَرِثُ الْقَاتِلُ شَيْئاً»

“…na muuaji harithi chochote”. Ameitoa Abuu Daud…

3-Katika Quran kuna Aya zilizoeleza katika hali ya wazi bila ya mpaka (mutlaqa), ikaja ikaifunga (qayyadat) hii itlaq  kwa kifungo (qayd) maalumu. Na katika hayo ni kauli yake Allah Mtukufu:

﴿وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّى يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِنْ رَأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِنْ صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ﴾

“Msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama wafike ihlal zao, mwenye kuwa mgonjwa kati yenu au ana maradhi kichwani kwake basi ana fidia huyo ya funga au sadaka au kuchinja” .

Haya mambo matatu kufunga, sadaka na kuchinja ni nakira zilizothibiti, ambayo ni maneno mutlak, lakini yakafungwa kwa hadithi ambayo ameitoa Muslim kwa njia ya Ka’ab bin ‘Ajra kwa kauli yake (SAW) kumwambia yeye:

«فَاحْلِقْ رَأْسَكَ وَأَطْعِمْ فَرَقًا بَيْنَ سِتَّةِ مَسَاكِينَ وَالْفَرَقُ ثَلاَثةُ آصُعٍ أَوْ صُمْ ثلاَثةَ أَيَّامٍ أَوِ انْسُكْ نَسِيكَةً»

“Nyoa kichwa chako, na ulishe farqa kwa masikini sita na farq ni pishi tatu, au funga siku tatu, au chinja mnyama”, basi ikafungwa itlaq ya funga kwa siku tatu, na itlaq ya sadaka kwa farq kwa masikini sita na farq ni pishi tatu, na itlaq ya kuchinja kuwa ni kuchinja mbuzi mmoja.

4. Kulikutanisha tawi katika matawi ya ahkaam kuyakutanisha na asili yake ambayo imetajwa katika Quran, likadhihiri tawi hili kuwa kuwa ni sharia mpya, na kwa uchunguzi wa kindani hubainika limekutanishwa na asili yake ambayo imetajwa katika Quran. Na haya yapo mengi. Na katika hayo ni kwamba Allah Mtukufu ametaja viwango vya mirathi na hakutaja mirathi ya ma asaba isipokuwa kile kilichoelezwa katika kauli yake Allah Mtukufu:

﴿يُوصِيكُمُ اللَّهُ فِي أَوْلَادِكُمْ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْنِ﴾

“Allah anakuusieni kwa watoto wenu kuwa mtoto wa kiume anarithi mafungu mawili ya mtoto wa kike” . Na kauli yake:

﴿وَإِنْ كَانُوا إِخْوَةً رِجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْنِ﴾

 “Na ikiwa ndugu warithi ni wanaume na wanawake basi mwanamume ana mafungu mawili ya mwanamke” , haya hupelekea kwamba asaba wasiokuwa watoto au ndugu hawana fungu lililokadiriwa (lililoelezwa), bali huchukua kilicho bakia baada ya kugawiwa mirathi. Mtume (SAW) akabainisha hivyo akasema:

«أَلْحِقُوا الْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَهُوَ لأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ»

“Wapeni mafungu wanaostahiki, kinachobakia ni cha aliye bora mwanamume”. Ameitoa Bukhari.

Akakutanishwa asaba asiyekuwa katika watoto akakutanishwa na ndugu na watoto. Na pia wamefanywa ndugu wa kike pamoja na watoto wa kike kuwa ni ma asaba. Kutoka kwa Al-As-wad:

«أَنَّ مُعَاذَ بْنَ جَبَلٍ وَرَّثَ أُخْتًا وَابْنَةً، فَجَعَلَ لِكُلِّ وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا النِّصْفَ، وَهُوَ بِالْيَمَنِ، وَنَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَئِذٍ حَيٌّ»

“Hakika Muadh bin Jabal alimrithisha ndugu wa kike na mtoto wa kike, kila mmoja katika hao akampa nusu, nay eye yuko Yemen, na Mtume (SAW) siku hiyo yuhai”  Ameitoa Abu Daud. Na Muadh hahukumu kama hivi katika uhai wa Mtume (SAW) isipokuwa kwa dalili anayoijua na kama hakuwa na dalili asingefanya haraka kuhukumu…n.k.

Tatu: Pamoja na hayo hapakupatikana hadithi kutoka kwa Mtume  (SAW) inayobainisha kila Aya kama ninavyojua… Na vitabu vya tafsiri kwa wingi wake na sherehe zake kwa upana havikueleza kila Aya kuwa ina hadithi sahihi… Kwa hivyo hutegemewa kilichopokelewa kutoka kwa Mtume (SAW) na kilichokuwa hakijapokelewa hufuatwa kwa ajili yake njia sahihi ya kutafsiri kwa namna ifuatayo:

1.Kilichonukuliwa katika tafsiri kutoka kwa Mtume (SAW) hakika kikisihi basi huzingatiwa kuwa ni sehemu ya tafsiri, wala hakizingatiwi kuwa tafsiri kwa inayoeleweka na wafasiri, kwa sababu huwa kilichothibiti kuwa ni sahihi kutoka kwa Mtume (SAW) katika kubainisha Aya fulani basi huwa ni nass ya kisharia kama Quran Tukufu.

2-Ama kilichonukuliwa kutoka kwa masahaba katika tafsiri hakika hicho huchukuliwa ni rai yake, hakika wao (RA) ndio walio karibu zaidi kuliko watu wote kwa kupatia katika kutafsiri Quran kwa kuwa juu ufahamu wao wa lugha ya kiarabu, na kwa kumsuhubu kwao yule aliyeteremshiwa Quran (SAW)…

3-Lakini inabakia njia ya kutegemewa ya kutafsiri ni kuifanywa lugha ya kiarabu na Sunna ya Mtume (SAW) ndio nyenzo pekee za kuifahamu Quran na tafsiri za maneno yake na sentenzi zake, na maana za kisheria, na ahkam za kisheria, na fikra ambazo zina wakia za kisheria… Basi ikisihi kutoka kwa Mtume (SAW) hadithi inayobainisha Aya basi hiyo ndiyo itakayotegemewa, na kama si hivyo basi hutegemewa lugha ya kiarabu ambayo Quran imeteremshwa kwayo katika kutafsiri Aya Tukufu. Lakini ni kwa wajuzi wa lugha wanaoijua vyema…

Hii ndio njia ya kutafsiri Quran ambayo ni wajibu ajifunge nayo mfasiri, na abebe jukumu hili yule anayetaka kufasiri Quran. Allah ndie Mjuzi zaidi na Mbora zaidi wa hekima.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta

25, Dhulhijjah 1439H – 05, September 2018

 

Maoni hayajaruhusiwa.