Inna lillah wainna illah rajiun

Tumepokea kwa huzuni na Masikitiko makubwa msiba wa kuaga dunia Sheikh Muhammad bin Nurdiyn bin Hussein Ash’adhliy. Mtoto wa Marehemu Sheikh Nurdiyn Hussein.

Kifo kimetokea jana wakati Sheikh Muhammad akiwa nchini India kwa matibabu. Taarifa za maziko zitatolewa baadae na ndugu.

Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na Jumuiya ya Shadhliya kwa msiba huu mkubwa.

Tunamuomba Allah Taala Awape wafiwa ujira mkubwa, Awamakinishe na subra katika kipindi hiki kigumu, na kwa Rehma Zake Sw Amuingize marehemu katika pepo ya darja ya juu.- Amiin

02 Oktoba 2018

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.