Inna Lillah waina illah Rajiun

Tumepokea kwa huzuni kubwa msiba wa kufariki dunia mwanaharakati mashuhuri Ustadh Saleh Mukaddam asubuhi ya leo Jumanne katika Hospitali yaTaifa Muhimbili alipokuwa kalazwa kwa ajili ya matibabu.

Marehemu (aliyefungwa pingu mbele ya Ust, Ponda) aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Masjid Haqqa Buguruni, pia kiongozi wa Shura ya Maimamu eneo la Kiwalani na daima atakumbukwa kwa kuwa kiongozi thabiti, hodari, mchapa kazi na asiyechoka katika utumishi wake wa hali ya juu kwa Waislamu na Uislamu. Kwa hakika kaacha pengo kubwa lisilo ni mithili.

Marehemu ataswaliwa Masjid Haqqah (Buguruni, Rozana) adhuhuri ya leo Jumanne na kwenda kuzikwa kijijini kwao Msanga, Kisarawe.

Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na Jumuiya ya Maimamu kwa msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Allah Taala Awape wafiwa ujira mkubwa, Awamakinishe na subra na kwa Rehma Zake Sw Amuingize marehemu katika pepo ya darja ya juu.- Amiin

02 Oktoba 2018

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.