Hukmu ya Picha za Kamera za Kufuatilia Matukio.

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Asalaam Alaikum warahmatullah wabarakaatuh. Kila la Kheri and Eid mubarak kwako amir wetu, Allah akuhifadhi, swali langu ni;

Ni nini hukmu ya matumizi ya kamera za kufuatilia matukio kwa watu na katika maduka, je yaruhusiwa kumshitaki mtu kwa kutumia ushahidi kutoka katika kamera hizi kama picha zitamuonesha mtu akiwa anaiba?

Kutoka kwa Dr Bassam Ash – Shabaan.

Jibu:

Waalaikum salaam warahmatullah wabarakaatuhu.

Swali lako lina sehemu kuu mbili, moja ni hukumu ya matumizi ya kamera za kufuatilia matukio, na pili ni juu ya matumizi ya picha za kamera hizo kama zinaweza kutumika kama ushahidi wa kisheria au la.

Jibu kwa sehemu ya kwanza ni kama ifuatavyo:

Kamera hizi zinahukumiwa juu ya msingi wa kisheria (qaidah) unaosema, “asili ya kila kitu ni halali mpaka ije dalili ya kukiharamisha”, msingi huu umechukuliwa kutoka katika aya ya Quraan.

‘’Humuoni Allah amekuumbieni (mtumie mtakavyo) kila kilichopo katika mbingu na kila kilichopo katika ardhi” (Luqman: 20).

Kisha akasema Allah,’amekuumbieni vyote vilivyopo katika mbingu na ardhi, na vyote vinatoka kwake’’ (Al – Jathiya 13).

Hakuna dalili katika makatazo ya matumizi ya kamera hizo, hivyo zinakuwa chini ya msingi huu (qaidah) na zinabakia kuwa zinaruhusiwa katika asili yake. Lakini japokuwa zimeruhusiwa kama zitatumika katika matendo yaliyokatazwa, matumizi haya yatakuwa hayafai kwa mujibu wa msingi (qaidah) ya kisheria inayosema; “Kile kinachopelekea haram, nacho pia ni haram’’ pia qaidah ya pili inayosema; “kilichoruhusiwa kwa mtu kutumia, kama kinadhuru kinakuwa haram na kitabakia halal katika asili yake”. Hivyo kamera za kufuatilia matukio kama zitatumika katika mambo ya halal kama kudhibiti wizi katika maduka, au mtaani kwa ajili ya kudhibiti foleni na kadhalika hii ni halal inaruhusiwa.

Lakini kama zitatumika kwa ajili ya kufuatilia maisha ya watu binafsi, au kuonesha ndani ya nyumba, yote haya hayaruhusiwi, kwa vile kuchunguza maisha binafsi ya mtu hairuhusiwi kwa msemo wake Allah. “wala msichunguzane‘’ (AL – Hujurat; 12).

Na imepokewa na Abu Dawud katika Sunnan yake kuwa amesema Mtume (s.a.w) “kama kiongozi (amir) hatawaamini watu wake basi atawapoteza’’. Na kwa vile kuchunguza maisha binafsi na matendo ya watu imekatazwa, amepokea Muslim kutoka kwa Abu Hurayra kuwa amesema Mtume (s.a.w) “Mtu anayechungulia nyumba za watu bila ruhusa imeruhusiwa kumtoboa jicho lake mtu huyo’’

Amma jibu katika sehemu yake ya pili ni kuwa, picha za kamera za kufuatilia matukio hazichukuliwi kama ushahidi wa kisheria kwa vile sheria imeweka aina nne (4) tu za ushahidi, nazo ni.

  • Kukiri (confession)
  • Yameen (oath)
  • Ushuhuda (testimory) na
  • Maandishi na hakuna aina tano au zaidi ya hizi kutokana na ushahidi ufuatao;

Iqrar (kukiri/confession).

Amesimulia Zaid Bin Khalid na Abu Huraira Allah awawie radhi kuwa alisema Mtume (s.a.w). “…nenda wa mke wa Fulani, kama atakiri basi mpigeni mawe’’.

Yameen (kiapo/oath)

Amepokea Ibu majah katika sunnah yake kutoka kwa Ibnu Abass kuwa anasema Mtume (s.a.w)

“kama watu watahukumiwa juu ya madai yao, madai ya damu na pesa, kiapo kitakuwa kwa mtuhumiwa’’ na amepokea Ad – Daaraqutni kutoka kwa Ata kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume (s.a.w) Kuwa; “ushahidi lazima utolewe na mlalamikaji, atakaekataa lazima atoe kiapo, isipokuwa katika kesi za Al – Qasama” na katika hadith nyingine amesimulia Amr Bin Shuaib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema; “ushahidi lazima utolewe na mlalamikaji na akikataa mshitakiwa, basi lazima atoe kiapo isipokuwa katika Al Qasamah’’.

Ushahidi wa mtu;  Anasema Allah juu ya hili;

“Na leteni wanaume wawili katika watu wenu kama mashahidi, kama hakuna wanaume wawili, basi leteni mwanaume mmoja na wanawake wawili’’(Al –Baqarah 282)

Ushahidi wa maandishi

Amesema Allah; “Msipuuzie kuandika, japo kidogo au kikubwa katika makubaliano, hilo ni bora mbele ya Allah na ushahidi wenye nguvu katika kuondoa mashaka kati yenu, isipokuwa katika mapatano ya haraka (ya kawaida) baina yenu, katika hayo hakuna lawama kwenu kama msipoandikishana” (Al Baqarah 282).

Hizi ndiyo aina za ushahidi katika sheria,ushahidi mwingine kama alama za vidole (fingerprints), uchunguzi wa damu (Blood analysis), picha, kutumia mbwa wa polisi na kadhakika si zaidi ya viashiria vya utambuzi kwa vile havithibitishishwi na kitabu (Quran) au sunnah, hivyo havichukuliwi kama ushahidi.

Hivyo picha za kamera za kufuatilia matukio hazichukuliwi kama ushahidi wa kisheria, na hii haimaanishi kuwa hazina umuhimu, ni muhimu katika kusaidia utambuzi na ushahidi hapa ni jambo tofauti. Picha hizi zinaweza tumika kusaidia utambuzi wa muuaji kwa mfano, lakini haziwezi kutumika kama ushahidi wa madai haya. Bukhari amepokea katika Saheeh yake simulizi ya Anas Ibu Malik (r.a) kuwa; “Myahudi mmoja alimpiga mfanyakazi kwa kuweka kichwa chake baina ya mawe mawili, na akaulizwa (mfanyakazi) nani amekufanyia hivi akasema ni fulani, mpaka myahudi yule alivyotajwa kwa jina, akakubali mfanyakazi yule. Akaletwa myahudi na akakiri. Mtume akamrisha auawe myahudi yule kwa kupigwa mawe’’

Tunaona hapa pindi Mtume (s.a.w) alipomuuliza mjakazi yule nani aliyemshambulia kwa kutaja majina ya watu na mjakazi yule akamtambua yahudi, hakuchukua kauli ya mjakazi huyo kama ushahidi bali kama utambuzi, na alivyoletwa yahudi na kukiri, ndipo alipoamrisha auawe.

Ushahidi hapa ulikuwa ni kukiri kwa yahudi, na si maneno ya mjakazi aliyeshambuliwa. Hivyo vitu vingine vinaweza kutumika katika utambuzi na si kama ushahidi wa kisheria mpaka vithibitike kutokana na vyanzo vya sheria.

Ndugu yako,

Ata Bin Khalid Abu Al Rashtah, 11th Rabii Al Awal, 1437 AH, 22th  December, 2015 CE.

Maoni hayajaruhusiwa.