Hizb ut Tahrir kamwe haijawahi kuwa na wala haitokuwa Kundi la Kigaidi!

0

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika muendelezo wa kipindi cha Redio/Tv Imani cha ‘Jihadi na Ugaidi’ kilichorushwa hewani mnamo tarehe 03/07/2017 (na kurejewa tena 06/07/2017) mwendeshaji wake Muhammed Issa alitoa tuhuma ya hatari dhidi ya Hizb ut-Tahrir kwamba ni kundi la kigaidi.

Muhamed Issa alitoa tuhma hiyo dhidi ya Hizb ut-Tahrir bila ya kunukuu hata tembe ya ushahidi licha ya Hizb ut-Tahrir kuwa na machapisho mengi kama vitabu, vijitabu, majarida nk. yanayofafanua kwa uwazi fikra zake na njia yake. Na kuhusiana na njia yake, Hizb ut-Tahrir iko wazi nyeupee kwamba inajifunga na njia ya mapambano ya kifikra na mvutano wa kisiasa tu bila ya kujihusisha  na utumiaji wa nguvu, mabavu wala vurugu kufikia lengo lake.

Kwa nguvu zote Hizb ut Tahrir Tanzania tunailani kauli hiyo ya uzushi na uwongo wa wazi yenye nia mbaya haswa dhidi ya Hizb ut-Tahrir na Umma wa Kiislamu kwa ujumla. Kwa hakika kauli hiyo isiyo na hoja si tu imetusikitisha sisi, bali imemsikitisha kila mtu makini na muadilifu. Zaidi ya hayo, kauli hiyo ni uvunjifu wa maadili ya habari na msingi wa kanuni ya kusimamia haki (natural justice) kwa kuunyima upande wa pili fursa ya kusikilizwa.

Sisi Hizb ut Tahrir Tanzania licha ya kukutana ana kwa ana na uongozi wa Redio/Tv Imani, kuwasilisha rasmi malalamiko yetu kwao tukiwataka warekebishe tuhuma hizo, bado tumo ndani ya jitihada kuonana ana kwa ana na Muhammed Issa ambae kwa bahati mbaya anaonekana kusitasita na kwa woga anajaribu kutukwepakwepa. Hatua za ziada zimo ndani ya mchakato katika kukabiliana na qadhia hii.

 

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.