Harakati za Urusi na Amerika Nchini Syria, Hariri ni Mfuasi wa Serikali ya Saudi Arabia

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali la Kwanza:

Twajua kuwa Urusi imeingia Syria kupitia makubaliano na Amerika au kupitia maagizo yake kuidumisha serikali hiyo na kuunda mazingira ya suluhisho la kisiasa na upinzani nchini humo. Lakini imeonekana kuwa Amerika inakaribia kutoa juhudi za Urusi za kuleta pamoja serikali na upinzani eneo la Astana na Sochi na mengineo, na inapo hudhuria (mikutano), itafanya hivyo kama mtazamaji tu mithili ya Jordan! Ni upi ufafanuzi wa hili? Shukran.

Jibu:

Ufafanuzi wa hili unaweza kufupishwa kwa kukusanya maneno mawili: kiburi cha Amerika na ujinga wa Urusi na kuonyesha hilo:

1- Ni kweli kuwa kuingilia kati kwa Urusi kulikuwa kwa ridhaa ya Amerika au maagizo yake kufikia maslahi ya Amerika. Tumefafanua hili siku za nyuma katika taarifa tuliotoa mnamo 11/10/2015, na iliyosema: “… Huu hapa ndio mkakati; Amerika inajidai kuungana na mapinduzi na hivyo kuwa vigumu kuwapiga vita hadharani, na wamesababisha madhara kwa serikali. Kibaraka badala kwa Amerika bado hajapatikana, hivyo basi mchezo wake mchafu ulikuwa ni kwa Urusi kufanya kazi hiyo. Dori yake ni kuisaidia serikali hiyo wazi wazi na kusimama wazi wazi dhidi ya mapinduzi hayo kwa sababu vita dhidi yake vishahalalishwa, na serikali ilikuwa tayari kuiita Urusi kupitia agizo kutoka kwa Amerika. Hicho ndicho kilicho tokea. Urusi imekubali kucheza uovu huu, dori chafu nchini Syria kuihudumia Amerika!” tuliliweka wazi hili katika “Jibu la Swali” tulilotoa mnamo 18/11/2015 kwa anwani: “Maendeleo Mapya katika Uwanja wa Syria”, lililo eleza: “…A-  Uvamizi wa Urusi nchini Syria mnamo 30/9/2015 ulitanguliwa punde tu na mkutano baina ya Obama na Putin mnamo 29/9/2015; mkutano huo ulichukua dakika 90… Mgogoro wa Ukraine ulitawala sehemu ya kwanza ya mkutano huo, huku maraisi hao wawili wakiangazia hali nchini Syria katika sehemu yake iliyo bakia. Matokeo ya mkutano huu moja kwa moja yalionyesha. “Mnamo 30/9/2015 baraza la Urusi (Russian Federation Council) lilipasisha kwa pamoja ombi la Putin la kutumia ndege za kijeshi za Urusi nchini Syria… (Chanzo: Russia Today 30/9/2015)”

B-  Hata maeneo yaliyo shambuliwa na Urusi nchini Syria mengi yao yalikuwa ni kwa makubaliano na Amerika. Shirika la habari la CNN lilinukuu mnamo 4/10/2015: “Jenerali Andrey Kartapolov, afisa wa kijeshi katika wanajeshi jumla wa jeshi la Urusi, alisema mnamo Jumamosi jioni 3/10/2015 kwamba maeneo yaliyo lengwa na jeshi la anga la Urusi nchini Syria yalikuwa tayari yashatambulishwa kwa Moscow na taasisi ya utoaji maagizo ya kijeshi ya Amerika kama maeneo yanayo ficha magaidi pekee.”

Hivyo basi, Amerika iliikaribisha Urusi nchini Syria kusaidia serikali hiyo na kuunda mazingira kwa suluhisho la Kiamerika. Urusi haikuingia Syria kubuni suluhisho kana kwamba ndiyo inayo dhibiti mambo nchini Syria. Lakini ujinga wa Urusi, baada ya maafa iliyo sababisha na kuweza kwake kuzuia kuanguka kwa serikali hiyo, kuliidanganya kufikiri kuwa ingeweza kusimamia suluhisho la kisiasa na kudhani kuwa Amerika haitapinga hili, bali, itakubali maadamu yeye, Urusi, ameongoza dori ya kikatitli nchini Syria kama ilivyo takikana na Amerika na kuilinda serikali kutokana na kuanguka kwake.

2- Kwa msingi wa ufahamu huu wa kimakosa, ikaitisha mikutano maeneo ya Astana na Sochi, na ikaalika makundi nchini humo na kuchora miradi. Na ikaialika Amerika kushiriki na kuwa na dori changamfu ndani yake: “Biskov alisema leo, Jumamosi, kumekuwepo na maendeleo mazuri kuhusiana na suluhu ya Syria katika muda wa hivi karibuni, “Lakini inahitaji juhudi za pamoja kuyafikisha katika hatua mpya yenye thamani, yote haya yahitajia Urusi kuamiliana na Amerika katika njia moja au nyengine…” (Chanzo: Orient News 4/11/2017). Urusi ilikuwa inatarajia kufanya mkutano baina ya raisi Putin na raisi wa Amerika Trump nchini Vietnam katika kongamano la APEC mnamo 10/11/2017, na imekuwa ikikariri na kuitisha mkutano wazi wazi baina ya maraisi hao wawili hata wakati wa kongamano hilo katika hali inayo ashiria haja ya Urusi kushirikiana na Amerika katika mahusiano baina ya nchi hizo juu ya Syria, lakini Amerika haikujibu na ikakubali tu kutoa taarifa ya pamoja ya maraisi hao wawili kana kwamba mkutano huo tayari umefanyika ingawa si kwa kiwango cha kimkutano, ilikuwa ni taarifa iliyo tayarishwa na wajuzi kutoka pande zote mbili na hatimaye kupeana mikono kwa maraisi hao wawili. Huu ni mfano wa Urusi kuiomba Amerika, inayo dhihirisha kutiwa aibu.

3- Urusi wakati huo huo inajua kuwa haiwezi kufanya hivyo bila ya Amerika, na inaendelea kuiomba ikitaraji kupata majibu; aina ya idhilali inayo anza kujitokeza, kama ilivyo tajwa juu kwa kutaka kwake mkutano baina ya Putin na Trump.

Na kwa sababu Urusi inakimbilia kupata suluhisho nchini Syria, raisi wake, Putin, alimualika mhalifu Bashar kufanya naye mkutano eneo la Sochi mnamo 20/11/2017, na kisha kuwasiliana na Trump mnamo 21/11/2017, akimwambia namna ya mazungumzo kati yake na Bashar yalivyo kwenda: “Raisi wa Urusi Vladimir Putin alimpigia simu leo,Jumanne, mwenzake wa Amerika Donald Trump, iliyo angazia juu ya mgororo nchini Syria na matokeo ya mkutano wake na Bashar al-Assad. (Chanzo: Russia Today 21/11/2017)

Hivyo basi, Urusi inapapatiko la kutaka kuharakisha suluhisho la mgogoro wa Syria, na kuota mchana kama kawaida yake kuwa yeye ni dola kuu inayo chukua nafasi sako kwa bako na Amerika katika kutatua mgogoro wa syria, kwa hivyo tunaiona kuwa na hamu kupata suluhisho la kisiasa leo kwa kuwa ndilo litakalo ipatia hadhi katika kuondoka kwake. Suluhisho hili la kisiasa litasitisha kudhaifika kwake hususan katika uchumi kama natija ya kushiriki kwake kijeshi. Kutokana na yote haya, ikachukua hatua ya kufanya mikutano iliyotoa sura ya kuwa yeye ni kiongozi anayeongoza juhudi za kupatikana suluhu nchini Syria; hivyo basi, ikamshurutisha Bashar, kisha Erdogan na Rouhani, na kisha kupanga kuwaita wale wanaojulikana kama wawakilishi wa “matabaka yote ya Syria” kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Urusi inainyenyekea Amerika kushiriki mchakato huu ili kufikia suluhisho la haraka, imetangaza nia yake ya kuondoa baadhi ya wanajeshi wake: “Huenda ikachangia pakubwa kupunguza idadi ya jeshi la Urusi nchini Syria “katika athari inayohisika wazi wazi” na huenda ikaanza kabla ya mwisho wa mwaka huu,” akasema Valery Gerasimov, mkuu wa jeshi la Urusi, mnamo Alhamisi… (Chanzo: euronews 23/11/2017). Lakini, Amerika inakwenda kwa mwendo wa kinyonga katika kujibu maombi ya Urusi.

4- Huu ndio mchezo wa Amerika pamoja na Urusi kuhusiana na Syria, yaani, kuitenga na kutelekeza matakwa yake na kutosimama nayo isipokuwa katika kadhia chache na aghalabu ni kwa kupitia wafuasi wake, jambo linaloonyesha kuwa juhudi za Urusi kuongoza suluhisho la kisiasa nchini Syria zitasambaratika kutokana na Urusi kuanguka ndani ya shimo la Amerika nchini Syria. Kile ambacho Amerika inakinyamazia kimya na kukishajiisha ni kuendelea kuitumia Urusi kama moja ya vifaa vya utawala wa Amerika nchini Syria dhidi ya mapinduzi na athari ya Uislamu ndani yake; Urusi haina dori yoyote ya kuongoza kutatua mgogoro nchini Syria licha ya kuoneka mandhari ya mikutano na makongamano mingi na kupokelewa kwake jijini Moscow na Sochi…

Na kabla ya njia ya Urusi na Amerika kuwa wazi, mipango yote ya Urusi kwa ajili ya suluhisho nchini Syria itasalia kuwa dhaifu ikisubiri kushiriki kwa Amerika. Pindi chembe chembe za suluhisho hilo zitakapo komaa nchini Syria, Amerika inatarajiwa kusonga mbele kupitia Umoja wa Mataifa au kupitia washirika wake wa eneo kulazimisha suluhisho nchini Syria.

5- Hivi ndivyo inavyo jitokeza kwa harakati za Urusi na Amerika nchini Syria, ambazo zaweza kutunguliwa, Allah akitaka, ikiwa makundi ya wapiganaji yatafuata njia iliyo nyoka na kuvunja mafungamano yao na vibaraka wa Amerika wa eneo, hususan Uturuki na Saudi Arabia, na kisha kusimama kidete mbele ya serikali kwa ikhlasi na kushirikiana na wenye ikhlasi miongoni mwa Umma, kwa kushikana na Kamba ya Allah. Hapo ndipo Syria, itakapo kuwa izara kwa Amerika na Urusi, na itakapo kuwa ni yenye kuwavunja migongo yao wote wawili na kutoka huku wakiwa wameshindwa, wakikimbia pasi na kujali chochote chengine nyuma yao. Hili si gumu kwa Alllah kulitimiza.

================

Swali la pili:

Hariri amerudi tena kutoka katika hali ya kujiuzulu kwake na wizara ikakutana chini ya uenyekiti wake mnamo 5/12/2017. Kisha akasema kuwa wizara hiyo imekubali “kutoingilia kati kadhia (nje ya Lebanon)” kufuatia vitendo vya Hariri, fazaa na migongano ilijitokeza: Baada ya miaka mitano ya kukosekana raisi nchini Lebanon, Hariri alikwenda kwa Aoun mnamo 20/10/2016 na kukubaliana naye juu ya uraisi na serikali, akijua kwamba Aoun na Hezbollah ni kundi moja na kwamba Hezbollah ndiye mhusika mkuu. Mnamo 04/11/2017, Hariri alitangaza kujiuzulu kwake nchini Saudi Arabia na kumwaga hasira zake kwa Hezbollah. Ulibatilisha kujiuzulu kwake huku na kuendelea na serikali, ikiwemo Hezbollah! Ni upi ufafanuzi wa fazaa hii na mgongano huu? Na je, uko muelekeo wa kupunguza ushawishi wa Iran na chama chake? Je, watarajia uvamizi kutoka kwa dola ya Kiyahudi kwa Lebanon au kwa Hezbollah, kwa kupatiliza fursa ya dhurufu zilizoko kwa sasa? Jazakallah.

Jibu:

Ili kuweka wazi jibu hili, ni muhimu kutaja uhalisia wa uhusiano kati ya familia ya Hariri na Saudi Arabia: Hariri ni mfuasi wa Saudi Arabia. Ikiwa mtawala wa Saudia ni mtiifu kwa Uingereza basi hili pia litatarajiwa kwa Hariri, katika miondoko yake, katika sera zake nchini Lebanon na hali kadhalika ikiwa huyo ni mtiifu kwa Amerika. Kwa msingi huu, twaweza kujibu yafuatayo:

1- Muhula wa aliyekuwa raisi wa Lebanon Michel Suleiman ulimalizika mnamo Mei 2014, na mtawala nchini Saudi Arabia alikuwa Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz, na kwa sababu Abdullah alikuwa mtiifu kwa Uingereza na kwa kuwa Hezbollah ilikuwa imejitolea kuhakikisha inamfanya Aoun kuwa raisi, na inajulikana kuwa Hezbollah na Aoun wanapewa usaidizi na Iran kibaraka wa Amerika, Mfalme Abdullah hakukubaliana na chaguo la Aoun kuwa raisi wa Lebanon, na hivyo basi kumuagiza Saad Hariri kupinga ugombezi wa uraisi wa Aoun. Saad Hariri sera yake aliichukua kutoka kwa sera ya Saudia, yaani sera ya Abdullah na hivyo basi nafasi kiti cha uraisi wa Jamhuri ya Lebanon imekuwa wazi kwa muda wa zaidi ya miaka miwili na nusu tangu kumalizika kwa muhula wa Michel Suleiman mnamo Mei 2014 mpaka mchana wa Jumatatu ambapo bunge la Lebanon lilikutana na kuchaguliwa kwa Aoun kama raisi wa Jamhuri hiyo na hayo yalikuwa mnamo 31/10/2016.

2- Kilicho saidia ni mabadiliko ya utawala nchini Saudi Arabia. Mfalme Abdullah alifariki mnamo Januari 23/1/2015, na kakake, Salman, kuchukua uongozi kutoka kwake. Kama ilivyo maarufu, yeye ni kibaraka wa Amerika. Mfalme huyu alianza kwa kuwakata mabawa watoto wa Abdullah ambao ni vibaraka wa Uingereza na waliokuwa wafuasi wake mpaka alivyoweza kuyaimarisha mazingira ya utawala wake. Baada ya mambo kutulia, na kwa sababu Amerika ilitaka kumakinisha hali nchini Lebanon kwa njia ya kivyake yeye kupitia kumchagua Aoun kama raisi wa Jamhuri hiyo, Amerika ilimuagiza Salman kumuagiza Hariri kutopinga hili! Hiyo ndio sababu Saad Hariri alikwenda kwa Aoun na kukubaliana naye na kumteua kama mgombezi wa uraisi wa nchi hiyo. Kwa maana nyengine ni kuwa, upinzani ulioongozwa na Saad Hariri katika enzi za Abdullah umemalizika katika enzi ya Salman! (Raisi Saad Hariri aliwasili kutoka makao yake (Bait Al-Wasat) na kumteua mbunge Michel Aoun kuwa mgombezi wa uraisi wa Jamhuri hiyo mbele ya wanachama wa chama chake, wakiongozwa na Raisi Fuad Siniora na mbunge Bahia Hariri. Kisha akatoa hotuba ambapo alisema: “Kwa msingi wa nukta za makubaliano tulizofikia, natangaza mbele yenu leo uamuzi wangu wa kuunga mkono kuchaguliwa kwa Jenerali Michel Aoun kuwa Raisi wa Jamhuri hii”… Chanzo: An-Nahar 20/10/2016).

Baada ya hayo, bunge la nchi hiyo lilikutana mnamo 31/10/2016 na Aoun akachaguliwa Raisi wa Jamhuri…” Uungaji mkono huu wa kiongozi wa chama cha Al-Mustaqbal, Saad Hariri, uliharakisha uchaguzi wa uraisi baada ya kiti hicho kukaa wazi kwa muda wa miaka miwili na miezi mitano tangu kumalizika kwa muhula wa aliyekuwa Raisi wa Lebanon Michel Suleiman mnamo Mei 2014… Chanzo: al-Arabiya 31/10/2017), na hivyo basi ziara ya Aoun nchini Saudi Arabia ilikuwa ni kuonyesha shukrani zake! Kama ilivyo wazi katika maelezo ya juu, Hariri ni mfuasi wa mtawala wa Saudi Arabia, kwa hivyo atapinga au kukubali kile atakacho onyeshwa na mtawala wa Saudi Arabia.

3- Baada ya Trump kuchukua uongozi wa Amerika, alizuru Saudi Arabia mnamo 20/05/2017 na kutoa taarifa kali kuhusu Iran na Hezbollah. Alilenga kutoa taarifa hizo kali kabla ya kongamano la takriban viongozi 50 walegevu wa Waislamu kuziba macho juu ya kadhia ya Waislamu wa Palestina na kuwafanya waangazie juu ya Iran, ambapo ilikuwa ni utangulizi wa kile alichokuwa anakipanga, kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Mayahudi. Ilikuwa wazi katika taarifa hizo katika kukokotezwa ukali wake. Bila shaka, Saudi Arabia na nchi nyenginezo miongoni mwa wafuasi wake zimetabanni muelekeo huu. Na kwa kuwa dori kuu ya Iran katika eneo hilo imetawaliwa na vitendo vya Hezbollah nchini Lebanon na kuingilia kati kwake nchini Syria, Saudi Arabia ilimuagiza Hariri kuwa mpinzani wa Hezbollah na Iran. Hivyo walimuita nchini Saudi Arabia na kumuagiza kujiuzulu huko na kutoa sababu zake kupitia taarifa kali dhidi ya Iran na Hezbollah. Kwa hayo, Hariri aliletwa nchini Saudi Arabia na kutoa taarifa yake kali, na kutangaza kujiuzulu kwake nchini Saudi Arabia mnamo 04/11/2017M.

4- Amerika inafahamu kuwa taarifa zake dhidi ya Iran na Hezbollah hazimaanishi mzozo kati ya Iran na chama chake, bali ni mkokotezo wa kupatiliza fursa ya hofu ya wakaazi wa Ghuba; ndilo lililotakikana kwa Saudi Arabia na Hariri kutuma ujumbe, lakini si kufuata barabara hii mpaka mwisho. Kwa maana nyengine ni kuwa, Amerika haitaki kumaliza uwepo wa chama chake, bali kutuma tu ujumbe uliotathminiwa pasi na kuchochea hali nchini Lebanon. Hii ndio sababu iliiagiza Saudia kuleta utulivu, yaani kumfanya Hariri kupunguza sauti yake. katika tovuti ya An-Nashra mnamo 04/12/2017, ilieleza: “…Mfalme Mtarajiwa wa Saudia, Muhammad bin Salman, hakuchukua hatua isipokuwa baada ya maelekezo kutoka ikulu ya White House, na baada ya ziara ya nne ya mshauri mkuu wa Raisi wa Amerika mkwewe Jared Kushner katika Mashariki ya Kati tangu Raisi Donald Trump kuchukua mamlaka, ziara hii iliwekwa mbali machoni mwa vyombo vya habari. Kushner na ujumbe wake nchini Saudia ulikaa siku nne ikihusisha ziara za mara kwa mara nchini Misri na Jordan na “Israel”. Takriban wiki mbili baada ya kuondoka Kushner, migogoro nchini Lebanon na ukamataji nchini Saudi Arabia ikalipuka. Wakati ambapo migogoro mibaya ya kisiasa ilipo ishambulia Lebanon, dalili ziliibuka kuwa kuna maelewano kati ya ikulu ya White House na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia juu ya Lebanon nayo ni kuishinikiza Hezbollah kufanya marekebisho ya ukubwa wa eneo lake baada ukubwa wa eneo lake kuongezaka. Chini ya anwani hii, Mfalme huyo Mtarajiwa wa Saudia alianzisha mashambulizi yake kwa serikali ya Lebanon kupitia Waziri Mkuu wake, Saad Hariri, na hivyo basi kuvuruga makubaliano ya kati na kati yaliyo fanyika kwa kuwasili kwa Jenerali Michel Aoun katika kasri la Baabda. Lakini mbinu ya Saudia ilikuwa ya vurugu iliyokosa hekima ya kidiplomasia, iliyo hatarisha utulivu wa kindani nchini Lebanon. Huku taasisi za Kiamerika zikiendelea kukariri kuwa shinikizo hili linalo lengwa Hezbollah linadhibitiwa na mipaka maalumu ambayo hakuna anayeruhusiwa kuivuka ili kuchunga kuharibika kwa hali nchini humo. Huku mambo yakizorota, taasisi za Kiimerika zilichukua hatua kwa msingi kuwa utulivu wa Lebanon uko katika hatari ya kuporomoka… (Chanzo: Tovuti ya An-Nashra: 04/12/2017)

Hivyo basi, Hariri akaanza kulainisha sauti yake kwa maagizo ya Saudi Arabia. Ili kuokoa uso wake, Saudi Arabia ilimpokea Raisi wa Ufaransa na kufanya mazungumzo naye na kukutana na Hariri. Kisha Hariri akasafiri hadi Ufaransa na kisha Misri na kuunda mazingira kana kwamba anawashauri ili kuchukua msimamo unaostahili ingawa mandhari yalionekana wazi nchini Saudi Arabia kabla ya kuondoka kwake, ambayo ni kulainisha sauti yake na kutojiuzulu. Haya ndio yaliyotokea; aliregea nchini Lebanon mnamo 22/11/2017 na kisha kupunguza sauti yake kwa kiwango kikubwa dhidi ya Hezbollah, na kusema kuwa Hezbollah haitumii silaha zake nyumbani, kana kwamba anajidanganya mwenyewe kabla ya kuwadanganya wengine, na kusahau kuwa Hezbollah hutumia silaha zao ndani ya Lebanon zaidi ya mara moja mpaka wakati alipo tangaza kusitisha kujiuzulu kwake na kuitisha mkutano wa baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wake mnamo 05/12/2017. Alisema katika taarifa yake (…kwamba hali ya utilivu imeregea baada ya uidhinishaji wa wanachama wote wa serikali wa kujiweka mbali na kadhia za nchi za kiarabu) alisema haya, huku wanamgambo wa Hezbollah wanapigana nchini Syria usiku na mchana!

6- Kwa mukhtasari, Hariri ni mfuasi wa utawala wa Saudi Arabia na sera yake kama mtawala inategemea Saudi Arabia, na utiifu wake unaashiriwa kwa maagizo yake kwake. Hili sio siri, na ni bure kuwapotosha watu kulihusu!

Kwa hivyo kutakuwepo na hatua ya kupunguza ushawishi wa Iran na chama chake, na hili lawezekana, lakini linatarajiwa kufanyika baada kufikia suluhusho nchini Syria kwa kiwango kinacho takikana na Amerika, kisha ikiwa dori za Iran na Hezbollah zitakamilika, huenda ikajiondoa nchini Syria na kupunguza dori ya kijeshi ya Iran na chama chake. Kwa taarifa yako, Hezbollah ni tagaa la serikali ya Iran kama alivyo Hariri tagaa kwa serikali ya Saudi Arabia. Hivyo basi, inatarajiwa kuwa ikiwa kadhia ya Syria itamalizika kwa mipangilio maalumu ya kujiondoa kwa Iran, mipangilio maalumu mengine itafuata kwa chama chake nchini Lebanon.

Je, kuna uvamizi wowote unaotarajiwa wa dola ya Kiyahudi kwa Lebanon na Hezbollah? Hii itategemea mipangilio ya suluhisho nchini Syria, ambayo inategemea dhurufu zilizoko kwa sasa na dhurufu mpya.

21 Rabii’ Al Awwal 1439 H

9/12/2017 M

Inatoka Jarida la Uqab: 13 

https://hizb.or.tz/2018/02/01/uqab-13/

 

Maoni hayajaruhusiwa.