Biashara ya kulipa kidogo kidogo

ﺑﺴﻢ ﷲ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

Swali:

Mtu anauza gari kwa 10,000/= na mnunuzi analipa hivi sasa 5000/= na kiasi kilichobaki atakuja kulipa kidogo kidogo kwa muda wa mwaka mmoja, lakini mwaka ukimalizika na akakamilisha kulipa deni anapewa khiyari mnunuzi baina ya kumilikishwa hiyo gari au achukue kile alichotoa, lakini kitapungua kidogo kwa kuangalia hali ya gari ilivyo, na kuangalia namna alivyoitumia, nini hukmu ya muamala huu na unaitwa ni muamala gani?

Jibu:

Biashara ya kulipa kidogo kidogo inaruhusiwa kisheria, kama ilivyowekwa wazi katika kitabu cha shakhswia Juzuu ya pili chini ya kipengele cha “Kuuza kwa Deni Na kwa kulipa Kidogo kidogo” na katika namna yake ni kulipa Mnunuzi Kiasi cha thamani hivi sasa, “Malipo ya Mwanzo” na atalipa kile kilichobaki kidogo kidogo ambacho watakubaliana Muuzaji na Mnunuzi…. na kinakuwa kile kitu kilichouzwa kwa mujibu wa mkataba huu ni milki ya mnunuzi kwa kule tu kulipa yale malipo ya mwanzo, na kunamalizika kulipa thamani yote kwa kulipwa fungu la mwisho, na kwa hili ndio humalizika jambo baina ya muuzaji na mnunuzi, na katika mkataba huu anaruhusiwa muuzaji kubakisha vile vile jina lake kwenye bidhaa husika mpaka pale mnunuzi atakapolipa ile sehemu ya mwanzo  ya kutolewa sasa hivi, “malipo ya mwanzo”.

Na kuna namna nyingine ya biashara ya kutoa kidogo kidogo nayo ni kutoa thamani kidogo kidogo inaanza baada ya kuda wa kufanyika  biashara, yaani pasina kutanguliza chochote cha mwanzo, kama vile kuanza kulipwa sehemu ya mwanzo baada ya mwezi au miezi miwili au mwaka mmoja, kisha baada ya hapo inatolewa sehemu ya pili na yatatu na yanne kwa mpangilio wanaokubaliana muuzaji na mnunuzi, na katika hali hii haifai kwa muuzaji abakishe ile bidhaa kwa jina lake, kwa sababu hakuna kile kilichotangulizwa mwanzo katika thamani, isipokuwa thamani yote hutolewa kimafungu kidogo kidogo kwa muda utakaokubalika baada ya kufanya biashara.

Kwa hivyo yale yaliopokelewa katika swali lako kwamba mnunuzi anamiliki gari baada ya kutoa fungu la mwisho, hiyo haifai katika Biashara ya kulipa kidogo kidogo, isipokuwa inafaa kwa muuzaji abakishe bidhaa kwa jina lake tu mpaka pale itakapotolewa sehemu ya mwanzo ya kutangulizwa, na hii ndio inaitwa katika fiqhi “Kuuza Rehani Kwa thamani yake” na tayari tulishajibu huko nyuma juu ya Rehani ya kinachouzwa kwa thamani yake yaani katika hali mbali mbali inajuzu kwa muuzaji kubakisha bidhaa kwa jina lake, na ninakurejeshea Tamko la jibu hilo:

(Hakika Mas’ala haya yanafahamika katika Fiqhi kwa Jina la (Rehani ya kinachouzwa kwa Tamani yake) yaani kinabaki kile kinachouzwa kwa muuzaji mpaka mnunuzi atakapolipa Thamani yake. Na Mas’ala haya hayajitokezi mpaka anapokuwepo Muuzaji na Mnunuzi kama alivyosema Mtume (S.a.w) :

أخرجه البخاري عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: «رَحِمَ اللَّهُ رَجُلًا سَمْحًا إِذَا بَاعَ، وَإِذَا اشْتَرَى، وَإِذَا اقْتَضَى»

Katika ambayo ameitoa Imam bukhari toka kwa Jabir Bin Abdillah: “Amrehemu Allah Mtu Mwenye kufanya wepesi pindi anapouza, na anaponunua na anapokopa (Kopesha)”

Lakini wakati Mwingine huwa wanatofautiana juu ya kupokea ile Bidhaa kwanza au kutoa hela kwanza, na huenda akakusudia muuzaji kuzuia ile bidhaa kwake yaani kuifanya rehani mpaka mnunuzi alipe thamani, na hapa ndio chipukio la Mas’ala haya, na hili wametofautiana wanazuoni, wapo wanaoruhusu kwa Masharti, na wapo wasioruhusu kabisa, na wapo wanaoruhusu katika hali Fulani na kutokuruhusu katika hali nyingine…. Na mengine yasiokuwa hayo .

Na kile ambacho ninakipa nguvu baada ya kutafiti mas’ala haya ni hiki kilichopo katika hali hii hapa chini :

Kwanza: Aina ya kinachouzwa:

1 – Kiwe kile kinachouzwa kinapimika kwa kilo au mizani au kwa urefu…..nk kama kuuza Mchele au pamba au  Vitambaa….nk.

2 – Kiwe kile kinachouzwa si chenye kupimika kwa kilo au mizani au urefu….nk kama vile kuuza Gari au Nyumba au Mnyama…nk

Pili : Thamani ya Kinachouzwa

1 – Iwe ni kulipwa hapo hapo, yaani keshi kama vile kununua Bidhaa kwa Alf kumi za kulipa muda huo huo.

2 – Iwe ni ya kulipwa Baadae kama vile kununua bidhaa kwa Alf  kumi ambazo zitalipwa baada ya mwaka mmoja.

3 – Kiwe kiasi Fulani kitatangulizwa kulipwa na kiasi kingine kitalipwa baadae, kama vile kununua bidhaa na ikalipwa mwanzoni alf Tano na alf tano nyingine zitalipwa baada ya Mwaka, au kugawa ulipaji kwa kila mwezi kiasi Fulani….

 

Tatu: Kutofautiana Hukmu ya kisheria kwa kule kutofautiana mambo yaliotajwa hapo Juu.

Hali ya Mwanzo: Kinachouzwa hakipimiki kwa kilo wala mizani… yaani mfano wa kuuza nyumba au gari au mnyama……

1 – Kulipa thamani keshi hapo hapo, yaani unanunua gari kwa alf kumi za kulipa keshi  na hili liwe limethibitishwa kwa makubaliano.

Katika hali hii inafaa kwa muuzaji azuie bidhaa, yaani itabaki kwake kama rehani kama itakapolipwa thamani yake kwanza kwa mujibu wa Makubaliano, na dalili juu ya hayo ni:

أخرجه الترمذي وقال عنه “حديث حسن” عن أبي أمامة قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ r يَقُولُ فِي الخُطْبَةِ عَامَ حَجَّةِ الوَدَاعِ: «العَارِيَةُ مُؤَدَّاةٌ، وَالزَّعِيمُ غَارِمٌ، وَالدَّيْنُ مَقْضِيٌّ» الزعيم: الكفيل، غارم: ضامن،

Hadithi tukufu ambayo ameitoa Tirmidhi na akasema ni “hadithi Hasan” Toka kwa Abuu Umaamah amesema: Nimemsikia Mtume (S.a.w ) akisema katika Khutba mwaka wa hija ya kuaga “Chenye kuazimwa kitekelezwe, na Mdhamini Alipe, na Deni lilipwe” Zaimu ni Mdhamini, Gharimu: Ni Dhamana ya kulipa, na namna ya ushahidi uliopo hapa katika hadithi ni kauli yake Mtume (S.a.w) “Na Deni Lilipwe” Pale mnunuzi atakapopokea Bidhaa kabla hajalipa thamini yake basi inakuwa ameinunua kuwa ni Deni, na “Deni ni Lenye Kulipwa”, yaani ni la mwanzo kulipwa muda wa kuwa kununua ilikuwa ni kwa keshi, na kwa maelezo mengine kulipa thamani mwanzoni kwa kuwa makubaliano ni kulipa mwanzoni yaani keshi…

Anasema Alkaasaaniy katika kitabu Badaaiu swanaai akitolea maelezo hadithi hii, Kauli Mtume (S.a.w ) “Deni ni Lenye Kulipwa” Ameelezea Mtume (S.a.w) kuwa Deni kwa kuwa ni lenye kulipwa kiujumla au moja kwa moja, kama itachelewa kupokea thamani kwa kupokea bidhaa, halitokuwa deni hili ni lenye kulipwa na hii ni tofauti na Dalili.)

Na juu ya hayo inafaa kwa muuzaji azuie bidhaa mpaka mnunuzi alipe thamani yake, hapo patakuwa hapana deni, na hii inaafikiana na makubaliano kwa sababu hapakuwa na  deni bali imekuwa ni thamani  ya kulipwa.

 

2 – Iwe thamani ni kulipwa Baadaye, kama vile kununua gari kwa Alf  kumi na kuja kulipa baada ya mwaka mmoja, katika hali hii haifai kuzuia bidhaa mpaka kulipwa kwa thamani kwa sababu thamani ni ya kulipwa baadaye kwa mujibu wa makubaliano ya biashara, haifai kwake kuzuia bidhaa kwa dhamana ya thamani yake muda wa kuwa aliuza kwa thamani ya kulipwa baadaye, basi ameangusha haki yake ya kuzuia bidhaa, kwa sababu hiyo haifai kwake kuzuia bidhaa, bali amkabidhi mnunuzi.

Tatu – Inakuwa thamani inatangulizwa na kuchelewesha, kama vile kununua gari kwa kulipa keshi  mara moja alf tano, na alf tano nyingine utazilipa baada ya mwaka mmoja mara moja au utazilipa kidogo kidogo kwa nyakati zijazo.

Katika hali hii inafaa kwa muuzaji kuzuia bidhaa mpaka deni lilibaki litakapolipwa, na baada ya hapo haifai kuzua bidhaa kwa kuwa keshalipwa sehemu iliobaki, na hayo kwa yale tulioyataja katika kipengele cha 2- 1

 

Na hitimisho ni kwamba inafaaa kwa muuzaji kuifanya rehani bidhaa kwa thamani itakayolipwa Baadae, yaani ikiwa makubaliano ya Biashara yamekubaliwa kulipwa kwa baadae inayolipwa sasa hivi, hapo itafaa azuea bidhaa hiyo kwake mpaka atakapolipa Mnunuzi hiyo thamani ya Baadae kwa mujibu wa Makubaliano ya Mauziano, na kadhalika inafaa kwa muuzaji kuzuia Bidhaa kwake mpaka pale atakapolipa Mnunuzi ili sehemu mwanzo kwa mujibu wa Makubaliano ya Biashara .

Na wala haisemwi hapa ni vipi Mnunuzi anaweka rehani biadhaa yake kabla hajaipokea, yaani kabla ya kuimiliki? Nayo ni kwa sababu Rehani haifai isipokuwa kwa yale yale yananavyofaa kuyauza, na kwamba Bidhaa ilionunuliwa haifai kuiuza isipokuwa baada ya kuipokea, kwa kutegemea kauli ya Mtume (S..a.w )”

رواه البيهقي، عن ابن عباس قال: قال رسول الله r لعتاب بن أسيد: «إني قد بعثتك إلى أهل الله، وأهل مكة، فانههم عن بيع ما لم يقبضوا».

Ambayo kaipokea Baihaqi toka kwa Abdallah bina Abbas amesema : Amesema Mtume (S.a.w ) kwa kumwambia Ataab ni Usaid bin Usaid : “Hakika mimi nimekutuma kwa watu wa Allah, watu wa Makkah, wakataze kuuza kile ambacho hawajakipokea”

والحديث الذي رواه الطبراني عن حَكِيمَ بْنَ حِزَامٍ قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنِّي أَبِيعُ بُيُوعًا كَثِيرَةً، فَمَا يَحِلُّ لِي مِنْهَا مِمَّا يَحْرُمُ عَلَيَّ؟ فَقَالَ: «لَا تَبِيعَنَّ مَا لَمْ تَقْبِضْ»،

Na hadithi ambayo ameipokea Twabarani toka kwa Hakim Bin Hizaam amesema : Ewe Mtume wa Allah mimi nafanya biashara ya vitu vingi sana, ni kipi ni halali kwangu na kipi ni haramu kwangu, akasema: “Usiuze kile ambacho hujakipokea” Hadithi hizi ziko wazi katika kukataza kuuza kile ambacho hujakipokea, basi ni vipi kuweka rehani bidhaa kabla ya kuipokea ?

Na wala haisemwi kuwa hadithi hizi mbili kwa vitu vinavyopimika kwa mizani na kilo….. ama ikiwa kinachouzwa si katika hivyo kama vile nyumba, gari na wanyama…… basi inafaa kukiuza kabla ya kukipokea kwa kutegemea hadithi ambayo kaipokea Bukhari toka kwa Ibn Omar amesema:

رواه البخاري عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ r فِي سَفَرٍ، فَكُنْتُ عَلَى بَكْرٍ صَعْبٍ لِعُمَرَ، فَكَانَ يَغْلِبُنِي، فَيَتَقَدَّمُ أَمَامَ القَوْمِ، فَيَزْجُرُهُ عُمَرُ وَيَرُدُّهُ، ثُمَّ يَتَقَدَّمُ، فَيَزْجُرُهُ عُمَرُ وَيَرُدُّهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ r لِعُمَرَ: «بِعْنِيهِ»، قَالَ: هُوَ لَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «بِعْنِيهِ» فَبَاعَهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ r، فَقَالَ النَّبِيُّ r: «هُوَ لَكَ يَا عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ، تَصْنَعُ بِهِ مَا شِئْتَ»

Tulikuwa pamoja na Mtume (S.a.w ) katika safari, nilikuwa juu ya ngamia mdogo wa Omar na alikuwa ananishinda, watu wananitangulia, basi Omar akawa anamkemea na kumrejesha, kisha anatangulia mbele, basi Omar akawa anamkemea na kumrejesha, akasema Mtume (s.a.w ) kumwambia Omar niuzie, akasema Chukua ni wako huyo ewe Mjumbe wa Allah, akasema niuzie, basi akamuuzia Mtume (S.a.w), na akasema Mtume (S.a.w) Huyo ni wako ewe Abdallah Bin Omar mfanye utakavyo” na huku ni kutumia Bidhaa kwa kuitoa Hiba, kabla ya kuipokea jambo linaloonyesha kuwa kumetimia kumiliki Bidhaa kabla ya kuipokea, na inaonyesha kufaa kuiuza kwa kuwa kumitimia kumiliki kwa Muuzaji.

Na juu hayo inafaa kuweka rehani  bidhaa kabla ya kuipokea kwa kuwa inafaa kuiuza kabla ya kuipokea, lakini hii peke yake ni vitu ambavyo si vyenye kupimika ….. kama nyumba, gari na wanyama nk, na wakati wa kutoka au kufanyika Biashara kwa thamani ya kulipwa hapo hapo au katika hali ya kuwepo malipo ya mwanzo wakati wa kufanya Biashara, basi inafaa kuweka rehani bidhaa kabla kuipokea mpaka itakapotolewa thamani ya mwanzo au malipo ya mwanzo.

Hali ya pili: Kinachouzwa ni katika vinavyopimika kwa kilo na mizani… kama kununua kiasi cha mchele au pamba au vitambaa… katika hali hii haifai kwa muuzaji kuzuia bidhaa kwa thamani yake kwa kiasi chochote kitakachokuwa cha thamani: sawa ni kulipwa kwa kutanguliza au kucheleweshwa, au ni mara moja au kidogo kidogo:

Na pindi ikiwa thamani ni ya kulipwa baadae pia haifai kuzuia bidhaa kama tulivyobainisha hapo juu.

Na ikawa thamani ni ya kulipwa kwa kutangulizwa pia haifai kuzuia bidhaa, yaani kuifanya rehani, kwa sababu haifai kufanya rehani kitu chenye kupimwa kabla ya kukipokea kwa mujibu wa hadithi ya Mtume (S.a.w ) ambayo tumeitaja hapo juu. Na muuzaji hapa katika hali ya kuuza kwa kutanguliza yupo kati ya Mambo Mawili :

Ima amuuzie Bidhaa kwa kulipa mwanzo na asubiri sawa atalipwa hela saa hiyo hiyo au baada ya muda, pasina kuifanya bidhaa ni rehani… na ima asiuze bidhaa, yaani pasina kuifanya rehani kwa hali yoyote ile .

Na juu ya hayo pindi biashara ikifungwa kwa thamani ya kutanguliza au kuchelewesha katika hali ya kuwa Bidhaa ni yenye kupimika kwa kilo au mizani, haifai kwa muuzaji aifanye ni rehani kwake mpaka kulipwa kwa thamani .

Mwisho.

Na kwa sababu hii, kwa hakika tamko ambalo nimelitaja katika swali kwamba haijuzu (Haifai) kwa sababu inafahamika kuwa Mnunuzi hamiliki gari kwa kule kulipa tu malipo ya mwanzo, isipokuwa ataimiliki baada ya kukamilisha sehemu ya mwisho, ikiwa yeye amechagua hivyo yaani kana kwamba mauziano yanaanza toka kumalizika kwa sehemu ya mwisho na hili halifai katika mauziano ya kulipa kidogo kidogo katika Uislamu, kwa sababu bidhaa inakuwa ni  milki ya mnunuzi kwa kule kukubaliana tu, na wala haifai kwa muuzaji abakishe bidhaa kwa jina lake baada ya malipo ya mwanzo kutolewa, pindi mauziano yakiwa ni kulipa kidogo kidogo, ama kama hakukuwa na malipo ya mwanzo, bali mauzo yote ni kulipa kidogo kidogo basi haifai kubakiwa kwa jina la muuzaji baada ya kufanyia makubaliano.

Ama yale ulioyataja katika swali la mwisho kwamba pindi akiaumua kuwa hanunui gari, na arudishiwe yale malipo aliotanguliza pamoja na kupunguzwa kiasi kwa kutumia kwake gari, yaani kana kwamba ni makubaliano ya kukodisha nayo si sahihi kwa sababu mkataba wa kukodisha ni wajibu ufanyike kabla ya kutumia gari na wala si baada ya kutumia.

Na hitimisho ni kuwa tamko (la makubaliano ) ambalo umelitaja katika swali Haifai ?

Nataraji liwe jambo hili limekuwa wazi kwa ukamilifu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu .

Na hii ndio yenye nguvu, na Allah ndio Mjuzi na Mwenye Hikma zaidi.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta

06/Shaabani / 1436 Hijria, sawa na 24/05/2015 Miladi .`

Maoni hayajaruhusiwa.