Yemen: Maswali Ambayo kila Mmoja Anatakiwa Kujiuliza!

Inawezekana vipi kujiandaa kila siku tukiwa na akili timamu, kuwaandalia chakula kizuri watoto wetu, kuwavisha mavazi mazuri na masafi na kuwalea kwa utulivu na mapenzi tukiwalaza, Lakini tukitazama kiuzembe takribani watoto milioni 1.8 wa Ummah huu ndani ya Yemen wakidhoofika na kuangamizwa bila huruma? Inawezekana vipi sisi tuwe na furaha kwamba watoto wetu wanakuwa na kustawi, wakati takribani watoto 500,000 ndani ya Yemen hawataona siku ya kuzaliwa kwao kutokana na vita vya leo dhidi ya Uislamu?

Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie, alisema:
« مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ، وَتَرَاحُمِهِمْ، وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى »
“Maajabu ya waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao ni kama mwili mmoja. Wakati kiungo kimoja kinaumwa, mwili mzima unashughulishwa kwa kuupelekea kuwa na homa na kukosa usingizi.” (Sahih al Bukhari)

Haituumi kuona kuwa Ummah wa Waislamu uko katika hali hii mbaya leo? Hatuna mioyo myepesi ya kuhisi
machungu haya ya kutisha wanayopitia kaka zetu, dada zetu na watoto wetu Waislamu? Je dunia yenye kuhadaa imetutia upofu kiasi kwamba tumezama ndani ya maisha yetu na matatizo yetu madogo tukisahau kuwa Ummah upo ndani ya mvutano hivi sasa na kwamba mtoto mdogo Muislamu asiyekuwa na makosa anaota kuhusu kipande cha mkate? Hakika tukijitia hamnazo juu ya uhalifu huu; basi hakutakuweko na khair yoyote ndani ya mioyo yetu!
Mtume (saw) alisema:

« إِنَّ فِي الْجَسَدِ مُضْغَةً إِذَا صَلُحَتْ صَلُحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ أَلَ وَهِيَ الْقَلْبُ »

“Kuna kijinyama ndani ya mwili- kikiwa kizuri, mwili mzima umekuwa mzuri. Kikiwa kibaya, mwili mzima umekuwa mbaya. Hakika ni moyo huo.” (Sahih al Bukhari)

Hisia juu ya Ummah ni hisia muhimu. Habari kuhusu hali ya Ummah ni ufahamu muhimu. Lakini hisia na ufahamu pekee hazitoshi kuuondosha uchungu wa Ummah. Ni vyanzo na msingi ambao hukamililika pale tunapotia hisia na fikra zetu na kuzifanyia kazi!

« اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لَ يَنْفَعُ، وَمِنْ قَلْبٍ لَ يَخْشَعُ، وَمِنْ نَفْسٍ لَ تَشْبَعُ، وَمِنْ دَعْوَةٍ لَ يُسْتَجَابُ لَهَا »
“Ewe Mwenyezi Mungu, naomba msaada Wako unilinde kutokana na elimu isiyo na manufaa, kutokana na moyo usiokuwa na hofu juu ya Mwenyezi Mungu, kutokana na nafsi isiyotosheka na kutokana na dua ambayo haikujibiwa.”
(Sahih Muslim)

Tunaona wazi kuwa maadui wa Uislamu hawatousaidia Ummah na kuwaletea kuwa kitu kimoja. Watawasababishia ugomvi zaidi baina yao na kuwapatiliza wao na nchi zao ili kufikia mipango yao miovu.

Na iko wazi kuwa ni kupitia kubadilishwa kwa uongozi wa kiulimwengu, ambao pekee Khilafah kwa njia ya Utume itaweza kubadilisha hali ya Waislamu. Kwa sababu ni kiongozi ambaye ni mchaMungu, yuko makini kuhakikisha Ummah wake haulali njaa na anaulinda dhidi ya maangamivu yoyote.

Kwa nini watu wengi bado wanaamini kuwa Marekani au Ufaransa ndiyo wanao wajali na kuwasaidia Waslamu???
Kwa sababu ni njia ya wazi, inayowadanganya Waislamu na kuwafanya mioyo yao idunde sio kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu bali kwa ajili ya dunia. Ni njia ambayo inawatia motisha Waislamu ili wasione kwamba nguvu kubwa za ulimwengu ndiyo adui mkubwa wa Uislamu. Hatimaye ndiyo njia ya kuugawanya Ummah na kuifanya mioyo yao kuwa migumu na kuwatia upofu.

Kaka na Dada Wapendwa!
Uamuzi tunao mikononi mwetu kuhusu ni njia gani ya kufuata! Ima sisi ni Waislamu tunaowafanya marafiki maadui wa Uislamu. Au sisi ni Waislamu tunaojali tu kuhusu mambo yetu ya kidunia au sisi ni Waislamu tunaojipa matumaini kupitia michango midogo au sisi ni Waislamu tunaofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunaleta ukombozi wa  kweli wa Ummah kupitia kazi ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللََّ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Na Amanah Abed

Inatoka Jarida la Uqab: 23     https://hizb.or.tz/2018/12/01/uqab-23/

Maoni hayajaruhusiwa.