Kudorora kwa Elimu Sababu Kuu ni Demokrasia

بسم الله الرحمن الرحيم

Dola ya  Khilafah itatoa elimu bure kwa watoto wote takribani milion 22.5 wa Pakistan ambao hawapo shuleni , shilika la haki za binadamu  (HRW) limesema, ripoti mpya iliyotolewa mnamo tarehe 13 mwezi wa 9 2018 kama ilivyoripotiwa na DAWN. Ripoti imesema kwamba, mbali na wale ambao hawapo shuleni 32% ni wanawake na 21% ni wavulana . Pia imedokeza kwamba mnamo mwaka 2017 Pakistani imetumia chini ya 2.8 ya pato lake la ndani katka elimu_wakati mwanzo ilitakiwa asilimia 4 hadi 6. Elimu imekua sio muhimu kwa serikali ya kidemocrasia ya Pakistani. Sekta hii nyeti katika maendeleo ya jamii imekua ikiwekewa kiwango kidogo kabisa cha bajeti. Hali imekua mbaya sana Pakistan kiasi ambacho elimu inawekewa bajeti ya asilimia 2.8 ya pato la ndani kama ilivyoainishwa katika ripoti hiyo. Pamoja na kwamba Afghanistani ipo katika hali ya vita lakini imeweka bajeti ya asilimia 4, India imeweka 7% na Rwanda inatumia 9% ya pato lake la ndani katika elimu. Kuweka bajeti ndogo katika elimu kumesababisha hali ya umasikini mkubwa katika elimu, hata kwa wale wanaoenda shule.  Kulingana na ripoti ya mwaka 2016, jumla ya shule 154,144 za Pakistani ni asilimia 52 pekee ndio zinaafadhali kidogo katika baadhi ya huduma mfano maji, umeme na vyoo, wakati huo asilimia 11 ya shule hazina chochote katka mahitaji ya msingi. Data zilizotolewa na UNESCO zinasema , Pakistan ndio inaongoza kwa msongamano na mrundikano wa wanafunzi kuliko nchi yoyote kusini mwa  bara la asia, kwa uwiano wanafunzi 500 kwa walimu watatu. Takwimu hizi zinaonyesha wazi namna mdororo wa elimu ulivyo. Niwazi kwamba watawala hawajali hali ilivyo na hawatekelezi majukumu yao. Zaidi ya hayo, wale waendao mashuleni wanafisidiwa kupitia mitaala iliyotengenezwa na mashirika yasiokua ya kiserikali, USAID, BENK YA DUNIA NA UNESCO.

Hali mbaya katika elimu yaweza kutengemaa kupitia mfumo wa elimu wa kiislamu chini ya  khilafah kupitia njia ya utume. Ni fardhi katika dola ya khilafah kutoa elimu kwa raia wote. Mtume  (saw) asema , « نم هيف ٍ لطي اقيرط كلس  ةنجلا قرط نم اقيرط هب هللا كلس املع»

“ikiwa mtu atafanya safari kwa ajili ya kutafuta elimu basi allah atamsababishia kupita katika moja ya njia za peponi.”

Elimu katika ngazi ya msingi na sekondari itatolewa bure kwa kila mtoto wakike na wakiume . Pia yawezekana khilafah ikatoa elimu ya chuo kikuu bure au kwa gharama ya chini kabisa. Zaidi, kutakua na mtaala mmoja ,na haitaruhusiwa kuwa na zaidi ya huo katika dola. Shule binafsi zitaruhusiwa maadam zitafata taratibu mtaala wa dola na kufata malengo ya sera ya elimu. Mtaala utabebwa na sheria za dini ya kiislamu pekee. Na hautaingiziwa chochote ambacho kitawavuruga waislamu katika usahihi wa dini yao. Pia mafungu ya kifedha yatawekwa kwa ajili ya miundombinu ya kielimu kama maktaba, maabara na vituo vya kiuchunguzi. Pia wanafunzi watahamasishwa kuishi na kubaki katika ardhi za waislamu na kutoa mchango wao kwa ummah wa kiislamu. Tutashuhudia mafanikio ya ustaarabu wa  kiislamu kufuatia utoaji wa elimu katika bara la asia. Na hata wasiokua waislamu watashuhudia na kutoa ushuhuda wao kutokana na mafanikio. Colonel William Sleeman aikiri kwamba elimu iliyotolewa Delhi ilikua na athari kubwa wakati alipotembela Delhi,mji mkuu wa Mughal “pamoja na hayo, zipo jamii chache katika dunia ambazo ambazo zimeacha athari kuliko zile za india.

#UislamuNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.