Watawala wa Pakistani Sasa Wanawateka Wanawake

Mnamo jumatano ya terehe 15 mwezi wa nane 2018, Wajumbe maalumu wa Hizb Tahrir kutoka uingereza waliwasilisha ujumbe kwa Tume ya ngazi za juu ya Pakistani iliyopo London.

Wajumbe hao waliwasilisha ujumbe wanye pointi zifuatazo:

Utawala wa Pakistan umeanzisha utekaji nyara wanawake katikati ya usiku kutoka katika majumba yao. Katika uislamu, wanawake ni watu wenye kuhitajia ulinzi na stara kubwa lakini utawala wa Pakistani umeonyesha haujali mipaka ya kidini na wala hakuna maadili wanayoshindwa kuyakiuka.

  1. Mara nyingine tena, ufisadi unaofanywa na mfumo wa kisekula wa kidemokrasia umeendelea kuleta madhara makubwa. Dr Roshana , daktari wa anaeheshimika pamoja na Dada Romana , mwalimu anaeheshimika wote wanamama waishio katika mji wa Karachi-wametekwa nyara bila hata ya mmoja kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Ikiwa utawala unawashutumu kwa kuvunja sheria sasa kwanini hauwapeleki katika moja ya vyumba vyake vya mahakama ?? Kwa hakika huu ndio utawala wa sheria uliokatika demokrasia tunayoiona Pakistani leo hii.
  2. Utekaji na ukamataji unaoendelea dhidi ya wanachama ndani ya Pakistan hauta izuia HIZB UT TAHRIR kuendelea na kazi zake za kisiasa kwa njia ya amani katika kubainisha ufisadi na uharibifu unaofanywa na mfumo wa kidemokrasia na kufanya kazi ya kurejesha dola ya khilafah katika Pakistan. Na hii ndio sababu kubwa kwamba, kwanini wanaume kama Naveed Butt, msemaji wa chama ambae amepotea tangu mwezi wa 5 mwaka 2011 na wanawake kama Dr.Roshan na Dada Romana kuendelea kutekwa na kushikiliwa kinyume na sheria.

4.Tunatuma ujumbe kwa utawala wa Pakistani kwamba wanawajibika kwa usalama wa hali zote kwa Dr. Roshana, Dada Romana na Naveed Butt.

  1. Utekaji huu ,kiuhalisia huweka wazi kuanguka kwa utawala katika nyanja zote za kisiasa na za kisomi kwa kule kushindwa kupambana na msuguano wa kisiasa wa Hizb ut tahrir. Badala yake kuamua kutumia mbinu za kidikteta kwa ajili ya kuukandamiza ummah wa kiislamu wa leo.
  2. Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisisasa kilichoegemea zaidi katika mchuano wa kifikra , hutumia njia ya Mtume Muhammad (ﷺ )kurejesha dola ya khilafah. Hili huthibitika kupitia vitabu vyake bora kabisa vinavyopatikana dunia nzima. Kwa hakika, tunatoa chalenji kwa utawala wa Pakistani utoe hata jalada moja tu kukosoa fikra za hizb ut tahrir ambazo zote zemeegemea kwenye uislamu.
  3. Viongozi wa Pakistani wameendelea kuwa ni wateja wa utawala wa Marekani. Huu ni utawala kama ule uliopinga uwepo wa CIA na mawakala wa Black water katika mchananga wa Pakistani pamoja na ndege za kimarekani zisizo na rubani zinapaa kutoka katika kambi za kijeshi za Pakistani-uongo ambao mwishowe  ulifichuliwa. Utawala huu umeendelea mara kwa mara kudanganya watu kuhusiana na ushirikiano wake na marekani, kwa kuendelea kuua watu wake kupitia kivuli cha kupambana na wanamgambo ili kuitengenezea njia Marekani iweze kuitwaa vizuri Afghanistan.
  4. Mbali na kuwa na ushahidi wa wazi wa namna ya mawakala wa marekani wanavyosababisha vifo na ugaidi kwa kupitia mtandao wao wa ujasusi wa Raymond Davis katika Pakistan, lakini bado utawala haujawaadhibu wauaji hao wa Kimarekani. Badala yake utawala umekua ukitoa huduma kwa Marekani kwa kuwateka wanaharakati wake wa Hizb ut Tahrir wanaonadi amani ambao eti kosa lao ni kueleza ushirikiano huu uliopo na kulingania watu katika mfumo wa kisiasa wa kiislamu wa khilafah.

9. Katika hamasa kubwa ya kulinda maslahi yake , utawala umejitahidi kwa upofu kuidhibiti Hizb ut-Tahrir kutokana na ulinganizi wake unaozidi kukua. Pakistan inaendeleza ushirikiano wake na bwana wake wa Kiamerika kitu ambacho Hizb ut Tahrir inaendelea kukiweka wazi. Na huu ndio ukweli kuhusu jambo hili.

Hizb ut-Tahrir inatoa wito wa kuachiwa Dr.Roshan na Dada Romana haraka iwezekanavyo-hawana hatia yoyote. Viongozi wa Pakistan wanapaswa kufahamu kwamba mbinu zao za kurejesha dola za Kimarekani hazitawasaidia kuepuka adhabu ya Allah( ﷻ) katika hii dunia na adhabu kali zaidi huko akhera  kama vile Allah ( ﷻ) alivyosema katika Quran:

ﻭَﻟَﺎ ﺗَﺤْﺴَﺒَﻦَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻏَﺎﻓِﻠًﺎ ﻋَﻤَّﺎ ﻳَﻌْﻤَﻞُ ﺍﻟﻈَّﺎﻟِﻤُﻮﻥَ ۚ ﺇِﻧَّﻤَﺎ ﻳُﺆَﺧِّﺮُﻫُﻢْ ﻟِﻴَﻮْﻡٍ ﺗَﺸْﺨَﺺُ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻟْﺄَﺑْﺼَﺎﺭُ

“ Na wala usiadhanie allah hajui wafanyayo. Bali amewachelesha hadi siku ambayo macho yata kodoka..”

[Ibrahim: 42]

#UislamNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.