Hatari ya Uvivu na Ukosefu wa Motisha kwa Muislamu

Kila mmoja anaijua hali ambayo mtu anajihisi ulegevu fulani na kutokana na hisia hii inakuwa vigumu kwake kutekeleza majukumu fulani, licha ya kiwango cha umuhimu wa majukumu hayo kwake, ima iwe ni jukumu la Kiislamu, la kimaumbile, matamanio au ghariza, uchungaji watoto, faida ya kiuchumi, masomo au hata majukumu madogo madogo ya nyumbani. Ni kana kwamba kuna kizingiti, kinachozuia kufanya jambo na kizingiti hiki hakiwezi kuondolewa na kwamba kwa bahati mbaya nguvu hiyo pia inazuia jukumu hilo maalumu kutotekelezwa. Hali hii ni hali ya uvivu.
Mtume Muhammad (saw) alikuwa akipenda kuomba:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ، وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْبُخْلِ وَالْجُبْنِ، وَضَلَعِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ“

“Ewe Allah, mimi najilinda kwako kutokana na wasiwasi na huzuni, na ulegevu na uvivu, na ubakhili na uoga, na kuzongwa na madeni, na kughilibiwa na watu.”

Uvivu waweza kuwa hatari mno kwa Muislamu na waweza kumvunja moyo kutokana na amali ya Da’wah, ambayo ni wajib na pia muhimu sana katika uhalisia wa leo wa Ummah pasi na Khilafah. Endapo Muislamu atahisi uvivu aina hii kwa amali ya Kiislamu ya kurudisha tena Khilafah au faradhi nyenginezo za Kiislamu, basi anapaswa kustaajabu ni kwa nini yuko katika hali hii na kuwa na hisia hii ya ulegevu.
Kuna baadhi ya tafiti ulimwenguni kuhusu hali hii ya uvivu. Aqliya ya kirasilimali pia huathiriwa na tatizo hili. Kutokana na matatizo ya kiuchumi katika miaka ya nyuma taasisi kadha wa kadha za kisayansi ziliingiwa na hamu ya kutaka kufanya utafiti iwapo uvivu wa wafanyikazi unaathri maendeleo ya kiuchumi au la, na nini kinachowapelekea wafanyakazi kuwa wavivu. Tyler Cowen, profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha George Mason alisema kuwa wafanyakazi wa Kiamerika wamekuwa wavivu na hili linasababisha Amerika kulemaa kiuchumi. Ripoti mpya ya hali ya sehemu za kazi za Kiamerika inakadiria kuwa wafanyikazi wasiojituma huigharimu Amerika kati ya dolari bilioni 450 na 550 kila mwaka kutokana na kupotea kwa uzalishaji.
Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa na Eden Springs uligundua kuwa takriban nusu ya wafanyakazi wa Uingereza wamevunjika moyo na wavivu kazini na utafiti sawa na huu ulifanywa na shirika la bima ya afya la Global health insurance (BUPA) uliotamatisha kuwa asilimia 46% ya wafanyakazi hawatii juhudi ya ziada katika majukumu yao. Kwa kuwa warasilimali wametambua kwamba wafanyakazi wao wamekuwa wavivu katika miaka ya hivi karibuni na kufanya kazi kidogo na ukosefu wa maelewano na kuwa hili huenda likapelekea dosari ya kiuchumi, imewamepelekea kufanya tafiti za kwa nini mtu huwa mvivu.
Baadhi ya tafiti kuhusu motisha zaashiria kuwa uvivu huenda unasababishwa na kushuka kwa kiwango cha motisha. Kwa warasilimali, inamaanisha kuwa wafanyikazi hufanya kazi vibaya sana kutokana na ukosefu wa motisha na hili hupelekea dosari kwa kampuni. Kwa sisi Waislamu hii yamaanisha kuwa, endapo mtu atakuwa mzembe na mvivu katika utekelezaji wa amali ya Da’wah, itakuwa ni kutokana na ukosefu wa motisha inayompelekea kushindwa kutekeleza jukumu lake la Kiislamu kisawasawa. Hatari kubwa zaidi ya hili ni kuwa inamharibia Akhera yake mwenyewe. Swali linalofuata laweza kuwa, ni wakati gani watu hukosa motisha?
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Carnegie Melon ulifichua kwamba watu hukosa motisha pindi wanapoona thamani ndogo katika mapato yanayojitokeza ya kazi zao. Lakini, endapo watu wataweza kuona wazi wazi namna kazi zao zinavyoafikiana na maslahi, malengo na hamu zao, kuna uwezekano mkubwa kwao kuzithamini kazi zao na kupata motisha kuwekeza nguvu zao ndani yake. Hali ya wafanyakazi wa kirasilimali ni kuwa wanadhulumiwa kwa ajili ya maslahi na malengo ya wengine, na hivyo basi inaeleweka kuwa baada ya muda hukosa motisha kazini na hivyo basi kuwa wavivu. Kwetu sisi hii yamaanisha, yakaribiwa kuwa haiwezekani kwa Muislamu anayefanya kazi kwa ajili ya radhi bora za Allah (swt) na kwa ajili ya Akhera, kukosa motisha katika majukumu yake ya Kiislamu na pia katika faradhi ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Pindi anapoelewa kuwa maisha ni mtihani tu na yanahusu ni nani anayeishi kwa mujibu wa sheria za Allah (swt), basi kimaumbile atawekeza nguvu nyingi na uwezo katika kufikia maslahi, malengo yake na natija ya mwisho.

Vilevile watafiti wa Australia wamegundua hali mpya inayo nasibishwa na uvivu wa hali ya juu: dosari ya upungufu wa motisha (MoDeD). MoDeD hufafanuliwa kama uvivu mkubwa na ulegevu. Vile vile ni ukosefu wa motisha pindi mtu: apotezapo hamu haraka, kutomaliza mambo aliyoyaanza, kuchelewesha na kusitisha kufanya mambo, kujiepusha na kufanya mambo, kulemaa, dhana kuwa yeye ni dhaifu, kuhisi kubanwa, kuhisi kutoeleweka, kuhisi upweke, uchovu na mawazo, kutaka kuimarisha maisha yake, lakini kutofanya lolote kwa hilo, kutokuwa na malengo, au matarajio na kujua kuwa huenda akapata zaidi, lakini hana moyo wa kuzikabili changamoto mpya.

Motisha kwa lugha ya Latin “movere” ni kitu kinachomsukuma mwanadamu kufanya jambo. Motisha ni msukumo wa ndani. Ndio unaokitia nishati kitendo. Kutokana na haya, ikiwa mtu atatambua kwamba amekuwa mvivu katika utekelezaji wake wa majukumu ya Kiislamu pamoja na amali ya Da’wah, anapaswa kuzingatia kama ana motisha ya kutosha kwa majukumu haya. Motisha pekee ya Muislamu ni radhi za Allah (swt) na Pepo ya milele. Hii inamaanisha kuwa daima anapaswa kukumbuka lengo lake ili daima abakie na motisha na daima asonge mbele na ari na ikhlasi na kutimiza majukumu yake ya Kiislamu. Muislamu anapaswa kuwa na fahamu safi za Kiislamu kuhusu maisha haya na kwamba atimize jukumu lake sio kwa kulazimishwa bali kutokana na khiyari yake mwenyewe. Kwa hivyo uwezekano ni mkubwa kwamba fahamu hizi safi zitamsaidia kutopoteza muono wa lengo lake na hivyo hataporomoka ndani ya makucha ya Dunia hii.
Elimu juu ya Jahannam kamwe haituruhusu sisi Waislamu kuwa wavivu na wazembe katika majukumu yetu ya Kiislamu, vile vile hali mbaya ya Ummah haituruhusu kuwa wavivu katika Da’wah ya kulingania Khilafah
#UislamHadharaMbadala

Kutoka jarida la Uqab 19

Maoni hayajaruhusiwa.