Vitisho Vya Atarturk Katika Kuvunja Khilafah

Mabwana Watukufu,

“Mamlaka kamili na Ukhalifah hawezi kuyapata mtu si kwa mjadala wala kwa mazungumzo, taaluma inalithibitisha hilo. Mamlaka kamili na Ukhalifa huchukuliwa kwa nguvu, kwa uwezo na kwa mabavu.

Ni kutokana na mabavu ndipo kizazi cha Uthman kiliweza kupora Mamlaka kamili na Ukhalifa kutoka kwa taifa la Uturuki. Na wameweza kushikilia uporaji huo kwa karne sita.

Sasa taifa la Uturuki limeshaasi na linawazuiya waporaji hao. Na kwa uwerevu limeshayachukuwa Mamlaka kamili na Ukhalifa katika mikono yake. Huu ndio ukweli timilifu. Suala lililopo sasa sio kujadili kwamba Mamlaka kamili na Ukhalifa lipatiwe taifa hili. Bali kilichopo sasa ni utekelezaji tu.

Hili litafanyika katika hali yoyote. Ikiwa waliomo humu Bungeni watalizingatia suala hili kwa umakini, nadhani wataliwafiki bila ya pingamizi. Na hata wasipowafiki, ukweli utachukua mkondo wake. Lakini katika mchakato huu baadhi ya vichwa vitakwenda na maji”

(Kamal Atarturk – kutoka kitabu cha The Struggle Within Islam)

#3machisikuyahuzuni

Maoni hayajaruhusiwa.