Uzushi (Bid’ah) wa Kuwacha Masafa ndani ya Swala ya Jamaa
بسم الله الرحمن الرحيم
Hili hapa jibu la maswali juu ya Swala ya Ijumaa ambayo mumeuliza kuihusu:
1- Nyuma tumetoa jibu la swala za Ijumaa mnamo 2 Sha’ban 1441 H sawia na 26/3/2020 M, vilevile mnamo 18 Sha’ban 1441 H – 11 Aprili, 2020 M, kisha mnamo 17 Shawwal 1441 H – 6/8/2020 M, na haya yametosheleza maswali yenu, ambapo yafuatayo yametajwa katika majibu haya:
Kwanza: Jibu letu mnamo 2 Sha’ban 1441 H 26/3/2020 M, ndani yake imekuja:
(Ama swala ya Ijumaa, ni faradhi ya lazima (Fard Ain)…
﴾إِذَا نُودِي لِلصَّلاَةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ﴿
“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara.” [Al-Jumu’a: 9] Ombi (Talab) hili katika ayah hii ni la lazima kutokana na dalili ya Qarina (kiashiria) cha kuharamisha kile ambacho kimeruhusiwa (mubah), ikiashiria ombi la lazima (jazim). Na Al-Hakim amesimulia katika Al-Mustadrak juu ya Al-Sahihain kutoka kwa Tariq bin Shihab, kutoka kwa Abu Musa, kutoka kwa Mtume (saw) kwamba amesema:
«الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ»
“Swala ya Ijumaa ni haki ya lazima kwa kila Muislamu katika jamaa isipokuwa kwa watu wanne; mtumwa anayemilikiwa, mwanamke, mtoto, au mgonjwa”. Al-Hakim amesema: “Ni hadith Sahih kwa sharti la Masheikh wawili.” Na sio wajib kwa yule aliye katika hofu, kutokana na yale yaliyosimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba Mtume (saw) amesema:
«مَنْ سَمِعَ النِّدَاءَ فَلَمْ يُجِبْهُ فَلَا صَلَاةَ لَهُ إلَّا مِنْ عُذْرٍ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَمَا الْعُذْرُ؟ قَالَ: خَوْفٌ أَوْ مَرَضٌ»
“Yeyote mwenye kuusikia wito (Adhan) kisha asiuitikie hana swala isipokuwa kutokana na udhuru, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu na udhuru huo ni upi? Akasema: Hofu au Maradhi” Imepokewa na Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra. Hivyo, swala ya Ijumaa ni faradhi kwa kila Muislamu, isipokuwa kwa wale walio na andiko la kisheria linalowatenga) Mwisho.
Pili: Jibu letu mnamo 18 Sha’ban 1441 H – 11 Aprili M, ndani yake imekuja:
(Mwenyezi Mungu (swt) asema:
﴾يَا أيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ﴿
“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.” [Al-Jumu’a: 9]. Muislamu anakwenda kuswali bila ya kuzuiwa.
﴾فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ﴿
“nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara..” [Al-Jumu’a: 9].
Kutekelezwa kwa swala hiyo ni lazima kwa sababu inahusishwa na kuacha kilichoruhusiwa (Mubah)… yaani swala haifanyiki katika sehemu za faragha, kama vile nyumba, ambapo uharamu huo unaruhusiwa … Hii ndiyo sababu ilielezwa katika Swali na Jibu hilo kwamba kufungwa kwa misikiti na watawala na kuzuia swala misikitini ni jambo ambalo haliruhusiwi na lina dhambi kubwa kwa watawala hawa. Kwa hivyo, ikiwa watawala wamezuia kuswali swala za Ijumaa msikitini, na hakuna mahali pengine panapo patikana kwa ajili ya swala hii isipokuwa majumba, basi huswaliwa nyumbani kama Rakaa nne za Adhuhuri, na dola inayofunga misikiti itabeba dhambi kubwa.
Ama suala la kuchukua njia (al-Asbab), hiyo ni sahihi, lakini bila kukiuka Shariah. Kuchukua njia hapa itakuwa kwamba mgonjwa haendi kwenye swala ya Ijumaa na walio wazima wanakwenda … Tumetaja katika Swali na Jibu hili (maalumati) ya kutosha kuonyesha kwamba misikiti haifai kufungwa ili walio wazima waweze kuswali, na kwamba hatua zapaswa kuchukuliwa kuwazuia wagonjwa aliye wenye maradhi ya kuambukiza kuhudhuria swala, ambapo iko wazi. Haiwezi kusema kuwa watu walio wazima huenda wakawa wagonjwa na virusi vya korona, lakini dalili zikawa hazionekani, na kwa hivyo wote wazuiwe kuingia misikiti, yaani, wakaazi wote wa sayari hii wazuiwe kuingia misikitini! Haya ni maneno ambayo hayana hoja hata kwa kiwango kidogo cha shaka!) Mwisho.
Tatu: Jibu letu mnamo 08/06/2020 M, yafuatayo yalitajwa mwishoni mwake:
(Sita: Mukhtasari wa yaliyo juu ni kama ufuatavyo:
1- Kubadilisha njia ambayo Mtume (saw) ameiweka kwa swala hukadiriwa kuwa ni uzushi. Bali, hukmu ya Kisheria katika hali hii ni kuwa mtu aliye mzima aende akaswali kama kawaida katika safu zilizo nyoka kwa kukaribiana pamoja, na bila ya kuacha nafasi, na mgonjwa aliye na maradhi ya kuambukiza asende na asiambukize wengine.
2- Endapo dola itafunga misikiti, na kisha kuwazuia watu walio wazima kutokana na kwenda misikitini kwa swala za Ijumaa na jamaa, basi itakuwa katika madhambi makubwa ya kukatiza swala za Ijumaa na jamaa, kwani misikiti ni lazima ibakie wazi kwa ajili ya swala kama ilivyo ashiriwa na Mtume (saw).
3- Vilevile, endapo dola itawakataza waumini kuswali kwa mujibu wa njia iliyo wekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) bali kuwalazimisha kuweka nafasi ya mita moja au mbili baina ya muumini mmoja na yule aliye karibu yake kwa hofu ya maambukizi, hususan pasi na kuonyesha ishara za maradhi, basi hili ni dhambi kubwa.
Hii ndio hukmu ya Sheria ambayo naipa uzito katika jambo hili, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi na ni Mwingi wa hekima … Na namuomba Yeye, Subhanahu, awaongoze Waislamu katika njia sahihi ya kumuabudu Yeye, Subhanahu, kama alivyo amrisha, na wamelazimika kujifunga na njia ya Mtume Wake (saw), na kusimamisha Shari’ah halisi isiyo na mkengeuko wowote kupitia kusimamisha Khilafah Rashida … ambayo ndani yake kuna kheri na ushindi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ambaye hashindwi na chochote mbinguni wala ardhini, Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.) Mwisho.
Nne: Ni wazi kutokana na yote yaliyotajwa hapo juu kuwa Ijumaa (swala) ni Fard Ain (Faradhi kwa mtu binafsi) na kwamba lazima iswaliwe kulingana na njia iliyowekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pamoja na nguzo zake (Arkan), masharti ya Usahihi wake na kutengeza safu kulingana na utaratibu wa kisheria, kama tulivyoonyesha katika majibu yetu ya awali… .Kuzuia kwa mamlaka utekelezaji swala kwa njia hii ni dhambi kubwa inayo anguka mabegani mwa mamlaka, ima hiyo ni kupitia dola kufunga misikiti au kupitia kuzuia kuswaliwa kwake kwa njia ya Kisheria …
Na kwa sababu Ijumaa (swala) ni faradhi ya mtu binafsi, kila Muislamu anayewajibika kisheria (mukallaf) ana wajibu wa kuitafuta na kuiswali kwa njia ya kisharia, pamoja na nguzo zake, masharti ya usahihi wake, na kuweka safu pamoja karibu karibu… nk. Na ikiwa mtu huyo hana uwezo kwa sababu ya kizuizi cha kimwili au mtawala dhalimu ambaye anazuia kutekelezwa kwa swala za Ijumaa kwa njia ya kisharia, badala yake
anawalazimisha wanaoswali kuzua kwa kulazimisha utengano, na anayeswali hana uwezo wa kuzuia hilo, basi mtu anapaswa kuiswali kulingana na uwezo wake, na mtawala huyo dhalimu anabeba dhambi hilo …
Mtume (saw) amesema, kama ilivyoripotiwa na Al-Bukhari na Muslim, Mwenyezi Mungu awarehemu, kutoka kwa Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu amridhie.
«وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ»
“Na pindi ninapowaamrisheni jambo litekelezeni kwa kadri ya uwezo wenu” na lafdhi ni ya Al-Bukhari … Kwa hivyo, ikiwa Muislamu anaweza kutekeleza Swala ya Ijumaa (wajibu wa mtu binafsi) kwa safu zilizonyooka karibu karibu basi inapaswa kuswaliwa kwa njia hii kwa sababu kujitenga ni uzushi maadamu anaweza kukwepa. Lakini ikiwa hana uwezo kwa kitendo cha mamlaka yenye dhambi, basi anapaswa kuswali kwa njia inayowezekana kwake. Al-Nawawi, (aliyekufa: 676 H) alisema katika kitabu chake, Al-Minhaj Sharh Sahih Muslim Ibn Al-Hajjaj katika kuelezea hadith hii kwa lafdhi ya Muslim: Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«فإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ»
“Na pindi ninapowaamrisheni jambo litekelezeni kwa kadri ya uwezo wenu” Al-Nawawi amesema katika ufafanuzi wake:
[(«فإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ» “Na pindi ninapowaamrisheni jambo litekelezeni kwa kadri ya uwezo wenu”) hii ni kutokana na sheria muhimu za Uislamu na maneno ambayo ni mafupi lakini yenye maana kamili ambayo alipewa Mtume (saw) na ni pamoja na chini yake vifungu vingi kama vile swala za aina zote. Ikiwa mtu hawezi kutekeleza nguzo zake (Arkan) au baadhi ya masharti (shurut) anapaswa kutekeleza yaliyosalia … Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi] Mwisho.
Tano: ipasavyo, ndugu na dada ambao waliuliza maswali haya wanapaswa kutekeleza Swala ya Ijumaa kwa sababu ni Fard Ain (faradhi ya mtu binafsi):
﴾يَا أيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ﴿
“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.” [Al-Jumu’a: 9]. Na Mtume (saw) amesema:
«الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ»
“Swala ya Ijumaa ni haki ya lazima kwa kila Muislamu katika jamaa isipokuwa kwa watu wanne: mtumwa anayemilikiwa, mwanamke, mtoto, au mgonjwa”. Al-Hakim amesema: “Ni hadithi ya Sahih kwa sharti la masheikh wawili.” Na wanapaswa kuiswali kwa njia ambayo Mtume (saw) aliagiza katika safu zilizonyooka karibu karibu, na ikiwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu mamlaka inawazuia kufanya hivyo na kuwalazimisha watengane, basi wacha waswali kulingana na uwezo wao, na fanyeni kazi kwa umakini na bidii kusimamisha Khilafah Rashida ambayo itatekeleza Shariah kwa njia yake sahihi bila kupotoka kokote kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na mafanikio kutoka Kwake.
Nataraji kuwa hili linatosheleza na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa Hekima.
Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
27 Safar 1442 H
14/10/2020 M
Link ya jibu kutoka kwa Ukurasa wa Amiri wa Facebook.
Maoni hayajaruhusiwa.