Ummah wa Kiislamu unazo Rasilimali lakini Uongozi Uliopo ndio Kikwazo

بسم الله الرحمن الرحيم

Ukombozi wa Konstantinopli ulikuwa tukio muhimu katika historia ya Uislamu ambao umekamilisha bishara ya Hadithi ya Mtume (saw). Ukombozi umeonyesha nguvu za Dola ya Kiislamu kwa kuwa Konstantinopoli iliweza kuhimili mizingiro mingi katika karne nyingi ukiwemo ule wa Waarabu katika 674-678 M na baadae katika 717-718 M.

Uwezo wa ufahamu na kutumia maarifa na akili wa Waislamu na nguvu za kijeshi na kujiamini huweza kuchukuliwa kuwa ni sababu ya mafanikio ya ushindi. Jeshi la Waislamu lilijawa na wataalamu wabunifu, wahandisi na wahandisi wajenzi.  Walijitayarisha kwa ushindi, kwa kuteka matokeo ya Baizantino ndogo, wakachukuwa udhibiti wa mlango wa bahari na kuikata Konstantinopoli kutoka kwa Bahari Nyeusi na misaada.

Al-Fatih pia aliamrisha ujenzi wa barabara ya magogo ya grisi kupitia Galata upande wa kaskazini wa Pembe ya Dhahabu, na kuburuta meli zake juu ya muinuko, kuelekea moja kwa moja kwenye Pembe ya Dhahabu mnamo 22 Aprili, kukwepa kizuizi cha minyororo walichoweka Wabaizantino kuuhifadhi mji. Na baadaye wakatumia mizinga mikubwa kulipua kuta za Konstantinopoli ambazo zilikuwa zikiuweka mji salama. Mzinga mkubwa wenye kutawanya shaba nyeusi haukupatikana Ulaya kabla na uliweza kurushwa hadi umbali wa maili moja.

Waislamu leo hii pia wanao uweledi kama huo, nguvu za kijeshi na ushupavu katika Ummah. Tuna nguvu ambazo zimeonekana wakati wa Khilafah – tuna rasilimali za: kijeshi, mafuta, gesi, maji, na watu.

Ulimwengu wa Kiislamu una umiliki juu ya milango nyeti ya bahari ya kimikakati kwa jeshi la wanamaji ikiwemo Bahari Nyekundu. Ghuba ya Uajemi, Bahari Nyeusi, Bahari ya Caspian, Bahari ya Kati, Ghuba ya Bengali na mlango wa Gibralta baina ya Moroko na Uhispania. Wanaweza kuutumia mlango wa Hormuz ambapo thuluthi moja ya mafuta ulimwenguni yanasafirishwa kupitia hapo.

Wanauwezo wa kumiliki mafuta na gesi, kwa asilimia 75 kiujumla ya hifadhi yote duniani. Tofauti na Amerika yenye kiasi cha asilimia 2 ya hifadhi ya mafuta na nchi za Ulaya zikiwa na asilimia 4. (Chanzo: Global Research)

Mwaka 2000, idadi ya Waislamu ilikuwa milioni 1209, na idadi ya watu ulimwenguni ilikuwa milioni 6057. (United Nations Population Fund (UNFPA).

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stocholm (SIPRI), kuna nchi tisa zenye umiliki wa silaha za nyuklia na Pakistan ni moja wapo. (Chanzo: The Independent)

Suala hapa sio ukosefu wa rasilimali: ni ukosefu wa umoja na uongozi. Tunazo rasilimali, kama ilivyoonyeshwa katika takwimu hapo juu. Lakini tumekosa uongozi wa mtawala kama Muhammad Al-Fatih aliyeweza kuunganisha rasilimali za Ummah na kuzitumia kukamilisha bishara ya Hadith.

Mtume Muhammad (saw) amesema,

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Mtaifungua Konstantinopoli basi Amiri bora ni Amiri wake, na jeshi bora ni jeshi hilo.”  [Ahmad]

Hii ni kinyume na hali ya sasa ambapo tumekuwa hatuko kitu kimoja na tumegawanyika katika vijinchi ambapo asili vimeundwa na mataifa ya kikoloni ya Kimagharibi. Umuhimu wa mazingatio ya watawala wetu umehama kutoka kutotekeleza sheria za Mwenyezi Mungu, hadi kutekeleza sheria za kisekula, na huku wakiendelea kutugawa na kuzipa uhalali sheria zilizotungwa na wanadamu na utaifa.

Haya yamekuwa yakifanyika kote katika Ulimwengu wa Waislamu. Uturuki iliyokuwa ndio kitovu cha Dolaya Kiislamu, ni dola ya kisekula. Uislamu hata hautambuliki kuwa ni dini ya dola. Katika nchi kama Pakistan, ambapo Uislamu ni dini ya taifa, watawala hawatekelezi sheria za Mwenyezi Mungu. Wanatumia sheria za kidemokrasia kama ni msingi wa hukmu zao, wakijaribu kuwashawishi Ummah kuwa uwepo wa baraza la Kiislamu, lisilo na nguvu, kuwa linatosha. Hiyo sivyo; sheria za Kiislamu lazima ziwe ndio msingi wa nidhamu ya hukmu – sio kile ambacho mtu hukitolea ahadi kwa maneno matupu bila ya kuwa na azma ya kutekeleza, kwa ajili tu ya kuwaridhisha raia.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

أَفَغَيْرَ اللَّهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمْ الْكِتَابَ مُفَصَّلاً﴿

“Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilichoelezwa wazi wazi?” [Al-An’am :114],

مَا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِنْ شَيْءٍ﴿

“Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote” [Al-An’am:38]

وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ﴿

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” [Al-Maida:45]

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«أَعَاذَكَ اللَّهُ مِنْ إِمَارَةِ السُّفَهَاءِ قَالَ وَمَا إِمَارَةُ السُّفَهَاءِ قَالَ أُمَرَاءُ يَكُونُونَ بَعْدِي لَا يَقْتَدُونَ بِهَدْيِي وَلَا يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَأَعَانَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَأُولَئِكَ لَيْسُوا مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُمْ وَلَا يَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي»

“Mwenyezi Mungu akuhifadhini kutokana na uongozi wa masafihi.” Wakauliza Masahaba, “Ni nani hao kutoka uongozi wa masafihi?” Mtume akasema, “Watawala watakaokuja baada yangu na hawatotilia maanani uongozi wangu wala kufuata Sunnah zangu, basi yeyote atakayesadiki uongo wao na kuwasaidia katika dhulma zao, hawatokuwa wenye kutokana nami nami sitokuwa ninayetokana nao. na hawato (ruhusiwa kukaribia) hodhi langu, yaani al-Kauthar.” [Ahmad]

Hivi leo, utiifu wa watawala hauko kwa Uislamu; upo kwenye mifuko yao. Watawaruhusu Wamagharibi kudhibiti nguvu zao kama kumaanisha kwamba nao wataweza kuendelea kunufaika kutokana na uwepo wa mfumo wa Kimagharibi wa kihuria.

Kutokana na hayo, Ummah wa Kiislamu uko katika zahama. Katika vita vya Yemen, Saudi Arabia nchi inayoambiwa ina watawala wa Kiislamu, inaongoza muungano katika vita na sasa nchi inaonekana kukumbwa na ‘mzozo mkubwa zaidi wa kibinaadamu’.

Pakistan inaungana na Uchina kwa maslahi ya kiuchumi, licha ya kuwa Uchina inaendelea kuwatesa Waislamu Wauyghur.

Hii ni mifano miwili tu ya uhakika inayoweza kupatikana katika Ulimwengu wa Kiislamu. Hii imezalisha hali ambayo Ummah wa Kiislamu umeachwa dhaifu na kuwa chini ya huruma za Wamagharibi, ambao unaendelea kupora rasilimali zetu kwa manufaa yao na kuwashambulia wanawake Waislamu na watoto wakiwa hawana hofu ya malipo.

Ili tuweze kubadili hali hii, tunahitaji kurejesha tena Dola ya Khilafah ili tuweze kuungana chini ya utawala wa Kiislamu, na tuweze kutumia rasilimali ambazo Ummah unazimiliki na kupata nguvu ambazo mwanzoni tulikuwa nazo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.