Ulezi ni Zaidi ya Cheti au Stashahada ya Ualimu

Wakati tukiwa na masikitiko na huzuni na tukiwapa pole sana wazazi, ndugu na jamaa waliondokewa na mtoto Sperius Eradius, mwanafunzi wa darasa la 5 Shule ya Msingi Kibeta, Bukoba baada ya kuchapwa viboko kinyama na mwalimu.

Kosa na mapungufu ya msingi katika mfumo wa kidemokrasia ni kule kuuangazia uwalimu kuwa ni kazi tu, ilhali ni zaidi ya hivyo:

Ualimu unaambatana na suala la ulezi, na sio kila mtu huwa ana sifa ya ulezi, licha ya kuwa kasomea ualimu. Kosa msingi kwa mfumo huu, unaandaa walimu kwa mzigo wa vyeti lakini sio walezi. Bali unazalisha mazonge mengi ya kuwachanganya hata hao walezi kupoteza muelekeo.

#UislamuNiMfumoMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.