Tusimame Kidete Kunusuru Heshima ya Mtume (Saaw)
بسم الله الرحمن الرحيم
Mnamo tarehe 26/05/2022 katika runinga ya Times Now nchini India Msemaji Mkuu wa Kitaifa wa Chama cha Mabaniani cha Bharatiya Janata Party (BJP) Bi. Nupur Sharma alitoa matusi na matamshi ya kashfa dhidi ya Mtume SAAW kuhusiana na ndoa ya SAAW na Mama Aisha ra.
Bi. Nupur Sharma ambaye kwa muda mrefu ni muungaji mkono mkubwa wa Waziri mkuu wa India na chama cha BJP kinachoshilikia fikra za mrengu wa chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu alitoa matamshi hayo wakati wa mjadala kuhusiana msikiti wa Gyanvapi wa Banaras, Uttar Pradesh, kaskazini mwa India ambao mabaniani wanataka kibali cha mahkama ili wafanye ibada ndani ya msikiti huo kwa madai kuwa umejengwa juu hekalu lao tangu karne ya 16.
Kashfa hiyo ya Bi. Nupur Sharma dhidi ya Mtume SAAW iliwafikia wafuasi wengi kupitia mtandao wake wa Twitter na Youtube ya runinga Times hususan kwa kitendo cha bwana Naveen Jindal, kiongozi wa kitengo cha habari cha chama cha BJP jijini Delhi ambaye alitawanya (re-tweet) kashfa hiyo na kuongeza matusi ziada.
Siku tatu baada ya kashfa hiyo, Bi Nupur Sharma alimweleza mwanahabari katika mahojiano nae kuwa, afisi ya Waziri Mkuu, afisi ya Waziri wa Mambo ya ndani na Afisi ya raisi wa Chama (BJP) wako nyuma yake (wanamuunga mkono)
Baada ya chama cha BJP kuona joto la Ummah wa Kiislamu dhidi ya kashfa hii nchini India na ulimwenguni kote, hadi baadhi ya nchi za Waislamu kuanza kampeni ya kususia bidhaa za India, chama cha BJP eti kilijitenga na kadhia hii, kwa kumsimamisha kazi katibu wake mwanamama Nupur Sharma na kumfukuza kazi Naveen Jindal, na Wizara ya Mambo ya Nje ya India ikatoa kauli kuwa, matusi na kashfa hizo hayawakilishi maoni na mtazamo wa serikali.
Hata hivyo, hata baada ya chama cha BJP kumsimamisha kazi Bi. Nupur Sharma bado alitetea matamshi yake ya kashfa kwa Mtume SAAW, kwa kusema kuwa ilimbidi kutoa kauli ile ili kutetea mungu Shiva wa mabaniani kutokana na kutusiwa na kuvunjiwa heshima yake mara kwa mara.
Hisia za Umma
Ummah wa Kiislamu unachukua hatua mbali mbali juu ya uovu huu wa kumkashifu mbora wa viumbe Mtume SAAW, wako wanaofanya maandamano, jumuiya kadhaa ulimwenguni zilipaza sauti kuonesha hisia zao, baadhi ya nchi za Waislamu kususia bidhaa kutoka India nk.
Kiini cha matukio kama haya:
Tangu kuangushwa Khilafah, maadui wa Uislamu na Waislamu wamepata ujasiri zaidi na zaidi kufanya uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wanavamia nchi za Waislamu, wametugawa, wamezikata mapande biladi za Waislamu kwa jina la utaifa, wanavamia kuharibu thaqafa, kuiba rasilmali, kuuwa na kutesa, kuasisiwa vita ddhidi ya Uislamu (ugaidi) wanavunja heshima za mabanati na kukashifu matukufu yetu ikiwemo Quran, misikiti na Mtume SAAW.
Kinachojiri India sasa ni mazoea ya mabaniani wa India kukashifu matukufu ya Waislamu huku Waziri wao Mkuu Narendra Modi akiangalia na kufurahishwa na mambo hayo kwa kuendesha kampeni haswa kuwalenga Waislamu kupitia chama chake cha BJP kwa kuwatesa, kuwabagua, kubaka wanawake wa Kiislamu, kuwavunjia majumba yao, kuathiri na kupiga moto biashara zao ikiwemo pia kuingilia majumba yao ya ibada kama kinachoendelea sasa kuhusu msikiti wa Gyanvapi na mengi yaliyotangulia kama ubomoaji wa Masjid Babri mwishoni mwa 1992 nk.
Matukio kama haya ya kashfa dhidi ya Mtume SAAW yamekuwa yakifanywa na makafiri kwa makusudi kwa kujirejearejea ulimwenguni. Kwa mfano, mwaka 2006 gazeti la Jylllands Posten la Denmark, 2019 nchini Malaysia, 2020 ndani ya Ufaransa nk. Makafiri hutenda haya kutokana na mambo matatu:
a.Uadui wao wa kimaumbile dhidi ya Uislamu
b.Kushindwa hoja dhidi ya Uislamu, hivyo hutapatapa kwa kudandia matusi
c.Kuwazoesha Waislamu waone matusi dhidi ya Uislamu, Quran na Mtume SAAW ni mambo ya kawaida.
Kisingizio cha ‘uhuru’
Kashfa na matusi dhidi ya Mtume SAAW, Quran na Uislamu kwa jumla huhalalishwa kwa kisingizio cha kulinda kinachoitwa haki ya binadamu ya ‘uhuru wa maoni’. Dhana ambayo ni uwongo, kwa kuwa nchi hizo licha ya kuhubiri ‘uhuru wa maoni’ lakini zina mipaka mbalimbali katika uhuru huo ikiwemo suala la usalama wa taifa nk. Kama ni ‘uhuru’ mbona unawekewa mipaka katika mambo yao, lakini katika kuutukana na kuukashifu Uislamu, Quran na Mtume SAAW ndio hutajwa kuna uhuru wa maoni.
Fikra ya ‘uhuru’ ni uwongo wa wazi. Uhuru unaohubiriwa ni ule ambao sio tishio katika maslahi yao, na pale ambapo huwa tishio huzuiwa. Sisi katika Uislamu hatuna dhana ya ‘uhuru wa maoni’. Kwa kuwa mwanadamu anawajibika kwa kila kauli na kitendo anachokitenda.
Uislamu unatuwajibisha kumpenda Mtume SAAW
Uislamu katika aqida yake unatuwajibisha Waislamu kumpenda Mtume SAAW kuliko chochote au yoyote, kwa kuwa yeye ndio kiongozi na kigezo chetu katika maisha yetu. Hivyo, tunawajibika kumtetea na kusimama kidete kukataa kila chenye sura ya kumkashifu, kumtukana au kuharibu haiba, hadhi na heshima yake. Allah Taala anasema:
النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ
‘Nabii ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao” (Surat Ahzab : 6)
Na Mtume SAAW anasema kupitia Hadithi ya Anas bin Malik ra.:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم
لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ
“Hatoamini kikweli mmoja wenu mpaka mimi niwe ananipenda zaidi kuliko watoto wake, baba yake na watu wote” Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 15, Ṣaḥīḥ Muslim 44
Hukmu ya kumtukana na kumkashifu Mtume SAAW
Hukmu ya anayemtukana au kumkashifu Mtume SAAW ni kuuwawa mtu huyo lau kuna dola ya Kiislamu ya Khilafah, kama alivyotuma kikosi Mtume SAAW kuuliwa waovu kama hao kama Kaab bin Ashraf, Nadhru bin Harith, Uqbat bin Abii Muiit nk.
Pamoja na kuwa Uislamu umekataza kumuua mwanamke katika vita, lakini endapo mwanamke huyo akijaribu tu kumtukana Mtume SAAW atauawa kama alivyouliwa mwanamke wa kiyahudi aliyekuwa akimtukana Mtume (SAAW). Kadhalika, Uislamu katika hali ya kawaida umetoa fursa ya kuomba msamaha kwa mwenye kutenda makosa ya kustahiki kuuliwa kabla ya kuuliwa kwake, na atafutiwa adhabu hiyo ya kifo. Mathalan, kama mtu aliyeritadi nk.
Lakini hali ni tofauti kwa anayemtukana Mtume SAAW, kwa kuwa anaemkashifu Mtume SAAW huwa amefanya makosa mawili: Kwanza, amekufuru na pili kumvunjia heshima Mtume SAAW.
Hivyo, mkosaji atapewa muda wa kutubia kosa hilo la kwanza la kukufuru kwani huwa ameritadi kwa tendo hilo, amma kwa kwa kosa la kumtukana Mtume SAAW atauwawa tu, kwa sababu ukimvunjia heshma mtu au kula haki yake, mwenye haki ya kusamehe ni yule uliyemfanyia uovu, na leo Mtume SAAW hayupo, hivyo mtoa kashfa na matusi dhidi yake atauwawa tu, kwani mwenye haki ya kumsamehe hayupo (Ibn Taimiyah)
Mtume SAAW anasema: ‘Atakaenitukana mimi basi muuweni’
Mwito kwa Ummah wa Kiislamu
Umma wa Kiislamu kwanza tushikamane na ufahamu wetu wa asili juu ya kuiweka haiba ya Mtume SAAW nafasi yake kuwa ni katika misingi ya Uislamu. Ikiwa na maana kutusiwa Mtume SAAW maana yake ni kutusiwa Uislamu wote kwa kuwa yeye ndie aliyepokea wahyi wa Uislamu na kutufikishia sisi. Pia Waislamu tuondokane na fikra chafu za kikoloni za kuona kama jambo halikutokea katika nchi zetu au karibu na sisi kana kwamba halituhusu. Uislamu ni dini moja, Mtume SAAW ni mmoja kwa Waislamu wote. Aidha, tuachane kabisa na fikra ngeni na batil za kidemokrasia za ‘uhuru’ kwa kuwa fikra hizi kwanza ni uwongo, lakini ndio hudandiwa kuwahalalishia makafiri kumtukana Mtume SAAW, Quran na Uislamu kwa jumla.
Mwisho, Ummah wa Kiislamu ufanye kazi ya ulinganizi wa kiulimwengu kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah inayopaswa kuanzia katika nchi kubwa za Waislamu ili kuinusuru na kuhifadhi Heshima ya Mtume (SAW) na Uislamu kwa jumla.
Isimamisheni Khilafah ihifadhi Heshima ya (Mtume SAAW)
Imetolewa na Wanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania
16 Juni 2022 M / 17 Dhu al-Qi’dah 1443 Hijri
#Isipokuwa_mtume_wa_allah_ewe_modi
#إلا_رسول_الله_يا_مودي
#KhilafahSilencesBlasphemy
Maoni hayajaruhusiwa.