Ngorongoro Katika Jicho la Insafu

بسم الله الرحمن الرحيم

Msingi wa tatizo la Ngorongoro ni sera chafu za uchumi wa mfumo muovu wa kibepari ambazo huruhusu kubinafsisha mali za Umma, kuruhusu unyonyaji wa rasilmali kwa jina la uwekezaji. Bali kubwa zaidi ni mfumo unaopima kila kitu kwa kipimo cha maslahi. Hivyo, takriban wanasiasa na watendaji wote katika ubepari huwa mbioni kukimbilia maslahi awe atakayekuwa. Watatofautiana katika mbinu na uhodari wa kughilibu watu.
Waislamu wanapokuwa katika nidhamu ya kibepari kimaumbile hutekeleza sera za kibepari, katika hali hiyo chondo chonde usilaumiwe Uislamu, rangi zao wala asili yao, kwa kuwa hawapo hapo kuwakilisha Uislamu, bali ulaumiwe mfumo wa kibepari ambapo katika hali ya mshangao kwa kutoelewa au kwa makusudi wale wanaopaza sauti kutetea Ngorongoro ndio hao hao wanaoupambania mfumo huo ukite na kutamalaki.
‘Ukipenda waridi upende na mti wake.’
Sera ya Uislamu iko mbali na yanayotendeka, na imeweka wazi kuwa maeneo ya mbuga ni maeneo ya Umma, hayaruhusiwi kubinafsishwa kwa mtu binafsi, taasisi wala kuwa mali ya serikali.
Anasema Mtume SAAW :
“Watu ni washirika katika mambo matatu:
Maji, malisho ya wanyama ( mbuga za wanyama) na moto ( vyanzo vikubwa vya umeme)” Abu Daud
Tusimame pamoja kuukataa ubepari na sera zake na kutandika mfumo mbadala wenye imani na uadilifu kwa wanadamu wote.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania HT Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.