Tunasimama Thabiti na Familia za Mahabusu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kufuatia mkutano wa wanahabari na wawakilishi wa familia za mahabusu watatu: Omar Salum Bumbo, Ramadhan Moshi Kakoso na Waziri Suleiman Mkaliaganda uliofanyika mnamo tarehe 09 Julai 2020 Magomeni Makuti, Dar es Salaam wakiwasilisha kilio, huzuni na masikitiko yao makubwa kufuatia wanafamilia wao hao watatu kuwa mahabusu kwa karibu miaka mitatau bila ya kesi yao kusikilizwa, sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunasimama kidete kwa mshikamano na familia hizo kudai haki za (mahabusu hao watatu) ambao ni wanachama wetu wa Hizb ut Tahrir Tanzania.
Kwa mara nyengine tena, sisi Hizb ut Tahrir / Tanzania tunasimama kuzitaka taasisi zote husika na utoaji wa haki ndani ya Tanzania kushikamana ipasavyo na mchakato wa kimahkama, amma kwa kuwasilisha ushahidi dhidi ya mahabusu hao mahkamani tayari kuanza kusikiliza kesi zao, lau wanao ushahidi huo, amma kuwapatia mahabusu hao dhamana, au kuwaachia huru mara moja.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.