Tufungeni Siku ya Ashuraa

Ni sunna kufunga mwezi wa Muharram ndani ya siku ya Taasua na Ashura. Yaani tarehe tisa na kumi ya mwezi huu. Ni Jambo muhimu kuweka azma ya dhati ya kufunga siku hizo InshaAllah.

Mwezi huu wa Muharram pamoja na kutukumbusha mengi, pia unatukumbusha ni namna gani Nabii Musa AS alivyopambana kifikra na kisiasa dhidi ya utawala dhalimu wa Firaun. Licha ya Mussa As kulelewa na Firauni alipopewa unabii alikalifishwa na Mwenyezi Mungu kutekeleza jukumu zito mno nalo ni kuwakomboa Banu Israil kutokamana na kila aina ya dhulma, mateso na madhila makubwa walizotendewa na Firaun.

Musa AS pasina kusita akapambana kufa na kupona dhidi ya utawala batili wa Firaun, akikosoa sera zake mbovu, ukandamizaji na dhulma alizokuwa akizitenda hadi mwisho akafaulu kuwakomboa Bani Israil.

Leo tunaishi katika mfumo wa kifiraun wa ukandamizaji na dhulma (ubepari) unaongamiza nafsi, kizazi na hata mimea….

Mfumo wa kibepari unaongozwa na Marekani unaotumia mabavu dhidi ya Waumini na wanadamu jumla. Kwa tukio la kuangamizwa kwake lazima tufahamu historia hujirejea.

Ni wajibu na muhimu kwa Umma wetu kuenzi amali tukufu ya Nabii Musa AS, kwa kukosoa sera mbovu za ubepari, kufichua aibu na urongo wake kwa lengo la kukomboa Waislamu na wanadamu jumla kutoka dhulma hizi. Na hili halitopatikana hadi pale tutakapokuwa na chombo cha kusimamia, kama Mtume SAAW anavyosema:

“Walikuwa Bani Israili wakisimamiwa kisiasa na Manabii, kila alipokufa Nabii akifuata nabii mwengine, hakika baada yangu hakutotokea tena Nabii ispokuwa watakuja makhalifa na watakuwa wengi….”

Maoni hayajaruhusiwa.