Tarekhe ya Ummah wa Kiislamu na Mustaqabal wake

Ummah wa kiislamu ulianza kidogo ndani ya Makka ukiwa dhaifu sana. Allah akaupa nguvu, akaupa Izzah kwa nusra yake, wakawa na Dola ya kwanza ndani ya Madina Munawwara. Dola ikatoa jeshi la ufunguzi, likasimamisha dini ya kiislamu katika Bara Arab, kisha likatolewa jeshi kuelekea Sham, Iraq, Afrika, Asia na Ulaya. Likiwapelekea kheri watu wote humo. Waislamu wakadhoofika katika dini yao. Wakatabikisha vibaya sheria za uislamu, dunia ikaingia ndani ya nyoyo zao, hatimae umoja wao ukagawika.  

Wakapigwa vita vya msalaba, ikatekwa Baitul Maqdis. Wakapigwa vita  na Tatar wakauteka mji mkuu  (Baghdad) wa dola ya Khilafah. Waislamu wakajizuia kupigana. Lakini Allah (swt) anakataa kutawanyika  Ummah wa kiislamu. Waislamu wakainuka kutoka mporomoko wao, wakashikamana upya katika Kamba ya Allah (swt), wakainuka mashupavu wao waumini kuwaongoza, vikatokea vita ikakombolea Baitul Maqdis wakawashinda Tatar. Wakadhofika tena waislamu, umoja wao ukagawika, Khilafah ikaangushwa, uislamu ukapotea katika maisha ya waislamu, Mayahudi wakaichukua Baitul Maqdis waislamu wakajizuia tena kupigana.

 Lakini kwa idhini ya  Allah (swt) ummah wa kiislamu utainuka tena, utashikamana na Kamba madhubuti, utarejea kama ulivyoanza, chini ya kivuli cha khilafah kwa njia ya Mtume (saw) utasimamisha dini, utamaliza makafiri wakoloni, na wataeneza kheri ulimwenguni kote

Amesema Mtume (saw):

ثم تكون الخلافة على على منهاج النبوة

“Kisha itarudi tena Khilafah kwa njia ya Utume”

Maoni hayajaruhusiwa.