Tangazo la Kuzinduliwa rasmi Matangazo ya Chaneli ya Alwaqiyah TV

0

Taarifa kwa vyombo vya habari

Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir inafuraha kubwa kuwatanganzia kuperusha hewani matangazo ya  chaneli ya Tv “Al Waqiyah” kabla ya kuanza mwezi wa Ramadhani. Hayo ni  baada ya kukamilika  muda wa matangazo ya  majaribio kwa mafanikio makubwa kwa msaada wa Allah (swt)

Aidha, tunapenda kuwajuulisha kuwa Tv Al- Waqiyah  ndani ya Ijumaa 26 Mei 2017 itapeperusha hewani matukio mawili makubwa: Kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan  na  uzinduzi wa Tv hiyo rasmi. Kwa munasaba wa matukio yote mawili Mwanachuoni gwiji na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah atatoa khutba. Zaidi ya hayo, Tv pia itakuwa na utaratibu wa kuwaweka hewani wasomi wenye kuheshimika na wanasiasa.  Matokeo ya kuonekana au kutoonekana mwezi kwa mwaka huu 1438 AH pia yatarushwa hewani.

Tv “Al-Waqiyah” ni chaneli ambayo katika hatua ya sasa inategemea urushaji wa matangazo yake na utoaji wa vipindi vyake kupitia mtandao wa  Internet  na ala za kisasa za mawasiliano pamoja na mitandao ya kijamii kueneza ujumbe wake kwa ulimwengu kwa ujumla, haswa kwa Waislamu, waarabu na wasiokuwa waarabu.  Huku Tv ikienda sambamba na mchakato wa maendeleo ya kiteknolojia kwa upande mmoja,  na  kuwa karibu na hadhira kwa upande wa pili. Katika ulimwengu wa leo ambapo habari ni bidhaa, na upotosha ukweli ni fani, na kuijaza uwongo  public opinion/’rai amma’ ni taaluma. Tv hii  imezinduliwa ili  iwe tunda  la kuiepusha hadhira yake kutokana na kuburuzwa na( uwongo) na kuuwasilisha ukweli kama ulivyo,  kwa kunyoosha mstari ulionyooka  ubavuni mwa mstari uliokwenda kombo.

Al-WaqiyahTv iko sambamba na mfumo wa Ummah,  na huo ndio msimamo wake, kwa kudhihirisha msingi wa ukweli uliojengewa juu yake,  na daima itabakia kuwa muaminifu kwa mfumo huo.  Al-Waqiyah kamwe haidai kuwa ni chombo kisichokuwa upande wowote. Kama vilivyo vyombo vingi vya habari, ambavyo kisha hujigonga na kujikanganya, kama inavyodhihirika kwa vyombo vingi kama si vyote kamwe , vikiwemo tv, redio au magazeti. ambazo zote ziko dhidi ya Uislamu. Sisi Al-Waqiyah tuko upande wa Uislamu, tena Uislamu wote kwa ujumla wake. Sisi tutakuwa upande wa Uislamu pale ulipo. Hii ni ahadi na kiapo tunachojifunga nacho. Al-Waqiyah ni  chaneli ambayo ni kinga ya kimedia/ kihabari inayofungamana na qadhia nyeti za Umma na kuziwasilisha kwa uwezo mkubwa na ushujaa ili kuchangia kujenga kwa uimara hali ya mwamko wa kisiasa miongoni mwa watoto wa Umma.

Wakati Al-Waqiyah ikisonga mbele katika hatua ya pili ya urushaji matangazo na vipindi vyake, tunawaalika wadau wote wa habari kufuatilia kwa karibu matunda ya chaneli hii. Wasambaze vipindi vyake ili vimfikie kila mtu, kwa sharti tu, udhati wa matangazo na  vipindi hivyo na kila kinachotolewa na Tv ya Al-Waqiyah kibakie kama kilivyo bila ya kugeuzwa.

Wakati tukitumia fursa adhimu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, matangazo yataendelea kama kawaida ndani ya kila Jumatatu na Alkhamis ya kila wiki. Hata hivyo,  kwa munasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kutakuwepo vipindi vya kila siku

Tunamuomba Allah (swt) Aitakabalie amali yetu hii, aibariki na kuifanya ni yenye kukubalika  ndani ya vifua vya Umma. Aidha, Allah (swt) aifanye amali hii kuwa nuru inayon’garisha njia kwa walinganizi wanaotaka kurejesha tena maisha ya Kiislamu kwa kurejesha dola ya (Khilafah) kwa kupitia manhaj/njia ya Utume. Basi wape bishara njema Waumini.

Anuani rasmi za tovuti na kurasa za Al-Waqiyah ni kama zifuatazo:

The official website of Al-Waqiyah Channel: www.alwaqiyah.tv

Al-Waqiyah Twitter page: twitter.com/AlwaqiyahTV

Al-Waqiyah Facebook page: www.facebook.com/alwaqiyah.tv

Al-Waqiyah page on Google plus: plus.google.com/+AlwaqiyahTv

A-Waqiyah Youtube page: www.youtube.com/AlwaqiyahTv

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.”>Pepe: alwaqiyahtv@outlook.com

Dr. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir

Kumb: 1438 AH /044

22 Sha’aban 1438 H              

19 Mei 2017 M

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.