Siri ya Mapenzi, Huruma na Heshima Katika Maisha ya Ndoa.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Moja kati ya mahusiano ya kipekee ambayo Allah (swt) ameyatengeneza kwa mwanadamu ni uhusiano kati ya mme na mke. Haya ndio mahusiano ya kiasili ukilinganisha na mahusiano mengine ambayo huunda muundo wa familia. Na hili ni jambo kubwa ambalo latakiwa kuendewa kiustaarabu na kwa taratibu maalum. Allah  (swt)  amesema;

 ﴾ هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ﴿

“yeye ndio yule aliekuumbeni kutokana mtu mmoja , na akaumba kutoka kwa mtu huyo mke wake, ili afurahie maisha pamoja na huyo mkewe ”.

[7:189]

Allah (swt)  ameweka kanuni katika mambo yote ya kiubinadamu, hivyo basi hutafuta njia za kutokumuuzi. Watafanikiwa au watafeli katika hii dunia, na hivyo wataadhibiwa au watapata mema huko akhera kulingana na utiifu wao juu ya hizi kanuni.

Moja ya sababu kwamba kwanini muundo wa kifamilia wa kiislamu hufanya kazi ni kutokana na usahihi wa muundo wake, ambapo kila mwanafamilia katika nyumba anajua majukumu yake ni yapi. Kitu kizuri kuhusu mahusiano ya mtu na mtu mwingine katika uislamu ni kwamba kila mmoja anadumisha mahusiano kwa ajili ya Allah (swt),  kuwa katika mahusiano kati ya mke na mume, wazazi na watoto au familia kwa ujumla. Kukidhi mahitaji ya wote kulingana na maamrisho ya Allah (swt) ni jukumu muhimu katika uislamu na hali hiyo itazalisha mapenzi, huruma na heshima katika ndoa na katika muundo wote wa familia. Mtume (saw)  alikuwa na uhusiano wa karibu zaidi na wafuraha zaidi  kwa wake zake na familia yake..  Allah  (swt)  amesema;

﴾لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْْخِرَ وَذَكَ رَ اللَّهَ كَثِيرًا﴿

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.

 [33:21]

Ibn  Maja  ameripoti kwamba, Mtume  (saw) alisema:

» خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِي »

“watu bora  kati yenu ni wale wabora kwa wake zao.”

Katika ndoa ya Mtume (saw) kulikua na mapenzi, huruma na heshima. Mtume (saw) alikuwa ni mwema kwa wakeze na hakuwa dikteta, hivyo haki ni jukumu kwa mwanaume kwenda kwa mkewe. Alikuwa na mahusiano bora kabisa na wao, alicheza nao, alifanya nao utani, aliwasaidia kazi za nyumbani pale alipoweza , na kuwafunza mambo tofauti tofauti.

Imesimuliwa katika sahihi al bukhari

“Alikua mara nyingi akijumuika kataika shughuli za nyumbani na alikua wakati mwingine akiripea nguo zake, viatu vyake na kufagia.alikua anakamua na kuwalisha wanyama wake chakula na kufanya shughuli nyingine za nyumbani”

Mtume (saw)  alikuwa ni mlinzi na mlezi kwa wake zake kama Allah (swt) alivyosema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ﴾﴿

“wanaume ni wasimamizi wa wanawake”

[4:34]

Pia  Mtume (saw)  amesisitiza heshima na ukarimu kwa watoto na wazee,  amesema  (saw):

«لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَمْ يَرْحَمْ صَغِيرَنَا وَيَعْرِفْ شَرَفَ كَبِيرِنَا»

“yoyote yule asie onyesha huruma kwa watoto wetu, au asiheshimu wakubwa zetu sio miongoni mwetu.” 

(Abu Dawood,  Al-Tirmidhi)

na Allah  (swt) amesema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلاَهُمَا فَلاَ تَقُل لَّهُمَآ أُفٍّ وَلاَ تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلاً كَرِيمًا * وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا

 “watendee wema wazazi, ikiwa mmoja au wote watazeeka katika uangalizi wako usiseme neno kwao la kuwaudhi. Wala usiwakemee, bali eseme na nao kwa msemo wa heshima na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma na useme : mola wangu warehemu wazee wangu kama walivyonilea katka utoto” [Quran 17:23-4]

Sifa nzuri na ya muhimu kuhusu mke ni kwamba ndio sehemu pekee ambayo mtu hupata furaha na amani katika imani yake. Mtume (saw) amesema:

«تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لأَرْبَعٍ لِمَالِهَا وَلِحَسَبِهَا وَلِجَمَالِهَا وَلِدِينِهَا فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ»

Mwanamke huolewa na moja kati ya sababu nne: utajiri wake, hadhi yake, uzuri wake na dini yake. oweni wanaoshika dini, vinginevyo utapoteza”

(Saheeh Al-Bukhari)

Mke mtambuzi huona jambo la muhimu zaid katika ndoa yake ni utiifu na kumtuliza mume wake, kwani Allah (swt) amempa hilo kama jukumu lake, na wala haimaanishi kwamba mke hana nafasi ya kutoa mawazo yake na hawezi kujadiliana na mme wake wala kutoa ushauri katika mambo. Bali anachotakiwa ni kumkubali mme wake kama mtoaji wa maamuzi katika nyumba na anaejitahidi kufikia malengo. Jukumu hili wala halimdogeshi mwanamke, bali ni jukumu linamtaka mwanamke akubali zawadi ya Allah, kama ambavyo mume atalipwa kwa wema wake, namna anavyoishi vizuri na mkewe , namna anavyomhudumia na kumjali kwa uwezo wake wote

Mtume Muhammad (saw) amesema:

» إذا باتت المرأة هاجرة فراش زوجها لعنتها الملائكة حتى تصبح «

“Kama mwanamke atajitenga usiku mzima mbali na mme wake katika kitanda cha mme wake basi malaika watamlaani mpaka amrudie mme wake.”

Na pia Mtume (saw) alimuuliza mwanamke:

   ،:  : » أَذَاتُ بَعْلٍ أَنْتِ ؟  » قُلْتُ : نَعَمْ ، «….قَالَفَإِنَّه جَنَّتُكِ  وَنَارُكِ «

“ Je una mume?” mwanamke akajibu: ‘ndio.’ Mtume akasema: “….basi huyo mume ndio pepo yako (Jannah) na ndio moto wako (Nar).”

Ni ushahidi kutoka kwa masimulizi ya Mtume kwamba kutekeleza haki na majukumu kati ya wanandoa ndio  jibu la mafanikio ya ndoa  na ndio matokeo amani ya maisha ya familia pamoja na watoto wanaotarajiwa na muunganiko wa familia nzima .  Hivyo Mtume (saw) ni kigezo chema kwa waislamu  katika mambo yao yote ya kimaisha, kwasababu Mtume (saw) ameonyesha kwamba uchamungu na wema ni kushikamana na sheria ya Allah katika njia ya sawa sawa. Mtume (saw) ametuonyesha namna ya kuwa tayari kujitoa muhanga na sio kuwa mtumwa wa matamanio binafsi na vile avipendavyo. Hivyo kama muislamu, akiwa ni mume au mke akatekeleza majukumu katika ndoa na akatekeleza haki zote kwa mwenzi wake, basi Allah (swt) atapenyeza mapenzi , huruma na heshima katika ndoa yao. ﴿ ربلا نكلو برغملاو قرشملا لبق مكهوجو اولوت نأ ربلا سيل  ىتآو نييبنلاو باتكلاو ةكئلاملاو رخلْا مويلاو هللاب نمآ نم باقرلا يفو نيلئاسلاو ليبءاسأبلا يف نيرباصلاو اودهاع اذإ مهدهعب نوقتملا مه كئلوأ﴾

“Sio wema pekee kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi katika kusali, bali wema haswa ni wale wanaomuamini Allah na siku ya mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na wanawapa mali juu ya kuwa wanaipenda kwa jamaa, mayatima na masikini na wasafiri walioharibikiwa  na waombao na katika kuwakomboa watumwa na wakawa wanasimamisha swala na kutoa zaka , na watakeleza ahadi zao pindi wanapoahidi na wavumiliao katika shida na madhara na wakati wa vita, hao ndio waliosadikisha uislamu wao na hao ndio wamchao Allah.”

[2, 177]

Imeandikwa na kituo cha ofisi ya habari ya  Hizb ut Tahrir na  Amanah Abed

http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/site-sections/articles/analysis/16268.html

Maoni hayajaruhusiwa.