Sha’aban sio mwezi wa ‘uhuru’ wala ramadhani sio mwezi wa dhiki

0

Tayari kuna matayarisho ya vitendo vya ‘vunja jungu’. Matendo haya ya vunja jungu  husukumwa na fikra mbili kubwa: Kwanza, fikra ya Uhuru wa Kibinafsi (personal freedom)  ambayo ni miongoni mwa nguzo za mfumo wa kidemokrasia na ambayo hulingania kuwa mtu atende atakalo. Pili, ni fikra ya hatari ambayo lau sio ujahili wa Waislamu wanaotenda haya, basi huritadi. Kwa kuwa  ‘vunja jungu’ humaanisha kwamba Ramadhani ni jambo zito, la dhiki, usumbufu na  lenye kunyima raha na utamu wa maisha. Kiasi kwamba huona wakomoe kwa mara ya mwisho ndani ya hatima ya mwezi wa Shaaban.

Hizi zote mbili ni fikra chafu, hatari na hazina nafasi katika Uislamu wala katika hali halisi. Uislamu umetuwekea wazi kwamba sisi ni waja wa Muumba na hatuna letu ila kunyenyekea Kwake tu. Na pia Uislamu ni dini inayowafikiana na maumbile ya mwanadamu, na kamwe haikuja kumtia uzito wala dhiki mwanadamu katika kushibisha mahitaji yake ya kibaologia kama chakula, maji nk. Na wala haikuja kumpa mashaka katika kushibisha mahitajio yake ya kighariza kama ya  kiibada, kuendeleza kizazi, ambayo ndani yake hupatikana matamanio ya kijinsia nk. Bali Uislamu umekuja kupanga utaratibu mwanana na mzuri kwa wanaadamu ili  wakidhi mahitajio yao yote bila ya pingamizi.

Tuingieni katika Ramadhani kwa furaha, moyo mkunjufu na uchamungu. Na tuiage Shaaban kwa furaha na tusijiingize katika maovu. Tukivuruga ndani ya Shaaban ndio kuvuruga ndani ya Ramadhani.

ْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Na wala(Mwenyezi  Mungu) hakuweka  juu yenu uzito katika dini”

(TMQ 22:78)

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.