Rushwa ya Ngono Vyuoni

Dokta Vicensia Shule ameibua suala la kushamiri kwa vitendo vya rushwa ya ngono chuo kikuu cha Dar es Salaam (Udsm)

Rushwa ya ngono vyuoni sio msingi wa tatizo, bali msingi wa tatizo ni nidhamu ya kielimu inayodhaminiwa na mfumo mbovu wa kisiasa yaani demokrasia na ubepari wake.

Na udhaifu huo kwenye mfumo wa elimu hasa kwenye nchi za dunia ya tatu unaonekana katika sehemu hizi.

1. Mfumo wa elimu haumuandai mwanafunzi kuwa mjuzi, bali unamfanya mwanafunzi awe ni maktaba ya kukariri nadharia za wasomi. Kwa hivyo kinachopatikana ni mashindano ya kukariri nadharia hizo. Na Hata wale waosoma elimu ya sayansi bado wanakariri tu nadharia hizo. Na ndio maana wakipelekwa kwenye utendaji wa kivitendo huonekana hawawezi kabisa au wanaonekana na uwezo duni sana.

2. Mfumo wa uendeshaji wa masomo wa vyuo vikuu umejengwa katika hali mbovu na kutoa mwanya wa rushwa za ngono. Kuwekwa kiwango cha alama/ maksi takriban 40 kuwa chini ya umiliki wa mkufunzi. Mfumo huu umewapa wakufunzi wengi wenye ulevi wa ngono kutumia upenyo huo kugawa alama /maksi hizo kwa wanafunzi wanaowataka kufanya nao zinaa. Na kwa mwanafunzi akigawiwa alama/maksi hizo bila ya shaka huwa ashajiepushe na kufeli somo hilo.

3. Wanafunzi wa kike wamekuwa ni chachu ya rushwa hiyo kutokana na ugumu wa mtaala na kutokana na uvivu wao wa kusoma. Na kujikuta wakirahishia kwa wakufunzi ili wapate alama/ maski bila ya kupasuka kichwa kukariri masomo hayo. Na pia kujihushisha na mambo mengine kama vile umalaya au mambo mengine na kutaka wawe ni wanaufaulu mzuri kwenye vyeti vyao. Na wengine pia hufanya kutokana na ugumu wa maisha.

4. Mazingira ya vyuoni yametengenezwa kuwa ni kichocheo cha ngono kwa wanafunzi na wakufunzi. Vyuoni kumekuwa ni sehemu ambayo hakuna nidhamu hasa katika maingiliano kati ya jinsia mbili. Kuanzia kwenye malazi, mavazi, mchanganyiko, vyuo vimekuwa ni ukanda huria/ free zone kiasi cha mwanafunzi kufanya atakavyo. Vyuo ndio vimekuwa kambi ya zinaa, usagaji, ushoga, ulevi…. Wanafunzi asilimia zaidi ya 60 wanaingia wakiwa wana maadili lakini wanaomaliza wakiwa na maadili mazuri ni asilimia 0.1%.

5. Kuweka mazingira magumu kwa vijana kuingia katika ndoa wakiwa masomoni. Hasa kwa mabinti ambao ndio wahanga wakubwa wa rushwa hiyo. Kikawaida unapopiga vita ndoa unafungua milango ya zinaa bila ya shaka. Vijana wakiwa masomoni haina maana wanaondoshewa matamanio ya kimwili. Na kwakuwa wakufunzi ni binadamu na wana matanio na wanafunzi. Katika mazingira hayo tuliyoyaelezea ngono kati ya wanafunzi na wanafunzi na kati ya wanafunzi na wakufunzi ni mambo yasioepukika. Ukikataa ndoa umefungua milango ya zinaa.

Suluhisho la kweli ni kuondosha mfumo mbovu wa kielemu sambamba na kuondosha mfumo mbovu wa kisiasa yaani demokrasia na Ubepari wake. Na kuleta mfumo mbadala ambao bila ya shaka ni Uislamu.

Na.

Sheikh Khatibu Imran ibrahim (Abuu Khaliil) 0714244930 whatsapp.

Maoni hayajaruhusiwa.