Njia Za Kukuza Uchamungu Katika Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani

بسم الله الرحمن الرحيم

Tukiwa bado tupo katika masiku matukufu, masiku ya dhahabu kwa ummah wa Kiislamu, masiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, ni vizuri tukaweka bidii katika kukuza uchamungu wetu (taqwa) na kuzidisha kumpenda (mahabbah) Allah. Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kutupelekea kufanikisha hili;
Kwanza, ni kusoma Quraan, kuizingatia, na kuifanyia kazi.
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ: ((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ
Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (RA) kwamba Mtume(SAW) amesema: “mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha” (Bukhaari)
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ: ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (RA) kwamba Mtume (SAW)amesema: “Allaah anao watu wake kati ya wanaadamu, wakamuuliza: ni nani hao? akasema: ni watu wa Qur-aan na ni watu wa Allaah na wateule Wake” (Ahmad, Ibn Maajah)
Hivyo kwa kusoma Quraan, kuizingatia na kuifanyia kazi tutakuwa watu bora, vipenzi na wateule wa Allah.
Jambo lingine muhimu ni kujisogeza karibu na Allah kwa kufanya ibada za sunnah mara baada ya kutekeleza ibada za wajibu.
«إن ﷲ سبحانه قال: من أهان لي ولياً فقد بارزني في العداوة، ابن آدم لن تدرك ما عندي إلا بأداء ما افترضته عليك، ولا يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه ،فأكون قلبه الذي يعقل به، ولسانه الذي ينطق به، وبصره الذي يبصر به، فإذا دعاني أجبته، وإذا سألني أعطيته، وإذا استنصرني نصرته، وأحب عبادة عبدي إلي النصيحة»
“Hakika Allah Subhanahu anasema: Yeyote anaemdhalilisha kipenzi changu basi amejitokeza kwangu na uadui, mwanaadamu hutaweza kuyafikia yaliyoko kwangu ila kwa kutekeleza yale niliokufaradhishia juu yako, wala hatawacha mja wangu kujikurubisha kwangu kwa sunnah mpaka nitampenda, na nitakua moyo wake ambao anatafakari nao, na ulimi wake anaozungumza nao, na macho anaonea nayo, na iwapo ataniita nitamuitikia na akiniomba nitampatia, na akitaka usaidizi nitamsaidia na ibada bora ya mja wangu mbele yangu ni nasaha” ameileta Tabrani katika Al Kabir.
Kuendelea na kumtaja Allah(dhikr) kwa moyo na ulimi katika hali zetu zote kwani jinsi tunavyomtaja ndivyo jinsi tunavyojenga mapenzi juu yake na yeye Allah kutupenda sisi, kuturidhia na kupata utulivu wa nyoyo zetu. Anasema Allah;
الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ ﴿٢٨﴾
Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah. Tambueni kwa kumdhukuru Allah nyoyo hutulia! (Ar-Ra’d 28)
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي ، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ ، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري , مسلم, الترمذي و ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Allaah Ta’aalaa, Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye Anaponikumbuka katika nafsi yake, Ninamkumbuka katika nafsi Yangu, anaponikumbuka katika hadhara, Ninamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamwendea mbio)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]
Mambo mengine ni pamoja kutanguliza mapenzi ya Allah juu ya mapenzi ya viumbe na kujiepusha na matamanio, kufanyia kazi majina na sifa za Allah, kukumbuka na kushukuru fadhila na neema alizotujaalia Mwenyezi Mungu, kuwa mpole na kujidhalilisha mbele ya Allah, kuwa karibu na kukaa vikao vya watu wema wachamungu wenye kumtaja Allah, nk
Kwa kufanya mambo hayo na mengine tutaweza kumpenda Allah, kupendwa na Allah na kukuza uchamungu wetu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na hata baada ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Baadhi ya mambo haya ameyataja Imamu Ibn Qayyim al-Jawziyya katika kitabu chake “Madārij al-Sālikīn”, pia Hizb ut Tahrir imefafanua kwa upana katika kitabu chake “Miongoni mwa mambo yanayokuza Nafsiyah ya Kiislamu” https://hizb.or.tz/4-miongoni-mwa-mambo-yanayokuza…/
Said Bitomwa
“Quran Muongozo wetu na chimbuko la Thaqafa Yetu”

Maoni hayajaruhusiwa.