Neno ‘Ummah’ kwa Mujibu wa Magwiji wa Lugha

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali

Katika Kielelezo cha Katiba, Kifungu cha 21, tumesema: “Na neno kundi hapa ni jina la aina, kwa maana nyengine, neno kundi hutumika na lile linalo kusudiwa kwalo ni aina …”

Nina maswali mawili:

  1. Sio vyema kusema: “Na neno ‘Ummah’ أُمَّةٌ) hapa ni jina la aina” badala ya “na neno kundi …” kwa sababu linahusiana na maana ya ibara ya aya kwa hivyo ni lazima litimiwe kama lilivyo?
  2. Imetajwa katika machimbuko mengi ya kilugha kuwa neno ‘Ummah’ (kama maneno ‘jama’ah (kundi), ‘qawm’ (watu), ‘rah’t’ (familia) na ‘ta’ifa’ (pote) …) ni nomino (ismu) mgando na sio jina la aina. Ni kwa nini tunayakadiria maneno ‘Ummah’ na ‘kundi’ (Jama’ah) kuwa majina ya aina na sio nomino (ismu) mgando?

Jibu

  • Kwa swali la kwanza, jibu ni kama lifuatavyo:

1- Neno ‘Ummah’ أُمَّةٌ) ni neno maarufu; lina maana nyingi, ikiwemo:

  1. Kundi: (تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ) “Hao ni watu walio kwisha pita” [Al-Baqara: 134] Ikimaanisha kundi. (أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْر) “Umma unao lingania kheri” [Al-i-Imran: 104] Ikimaanisha kundi linalo lingania kheri.
  2. Ikimaanisha pote moja ima katika Iman au upotovu, (كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً) “Watu wote walikuwa ni Umma mmoja” [Al-Baqara: 213], yaani pote moja katika njia moja ya upotovu.

 (وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً) “Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu” [Yunus: 19] yaani pote moja watangazaji wa tawhid.

  1. Kumaanisha dini au Shariah (وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً) “Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja.” [Al-Mu’minun: 52] yaani dini yenu na Shariah yenu.
  2. Kumaanisha wakati au muda (وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ) “akakumbuka baada ya muda” [Yusuf: 45] yaani baada ya muda fulani.
  3. Kumaanisha mtu anaye tenda kama kundi katika kheri (إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً) “Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema” [An-Nahl: 120] Yaani, imam au kiigizo chema, atendaye kama mjumuiko katika kumuabudu Mwenyezi Mungu.
  4. Kwa hivyo, ‘Ummah’ ni neno maarufu, hivyo basi, katika kufafanua aya maana yake katika aya hiyo ndio hutumika, ambayo ni ‘kundi’, na hivyo basi tumetumia maana hiyo katika ufafanuzi ulio wazi zaidi kuliko kutumia neno Ummah, kwa sababu neno hili lina maana nyingi, na maadamu ni kwa ajili tu ya kufafanua aya hiyo, basi ni wazi zaidi kutumia maana hiyo na kwa hivyo tumesema: (neno kundi hapa ni jina la aina) kwa sababu ikiwa tutasema (neno Ummah hapa ni jina la aina), kungekuweko na mkanganyiko katika maana zake; je ni Umma katika maana ya Imam au kiigizo chema, au ni Ummah kwa maana ya kundi, au ni Ummah kwa maana ya wakati, au taifa la Kiislamu … Hivyo, kutumia neno “kundi” ni wazi zaidi kwa sababu ndio maana iliyo kusudiwa katika aya hii(وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ) “Na uwe kutokana na nyinyi Umma”. [Al-i-Imran: 104]
  • Ama swali la pili, jibu ni kama ifuatavyo:

Inaonekana kana kwamba umesoma katika baadhi ya vitabu vya lugha vigawanyo vya jina (al-Ism) ni jina jumla na jina la wingi … Na kwamba neno linalo ashiria wingi na halina umoja wake huitwa jina la wingi kama vile qawm na rah’t … Kana kwamba umeelewa kuwa vigawanyo hivi ndivyo pekee vya majina. Na kwamba ufafanuzi wa jina la wingi hauna ikhtilafu, na hivyo kushangaa ni kwa nini tumesema Ummah na kundi kuwa majina jumla, ingawa yanaashiria wingi na hakuna muundo wa umoja kwa maneno yake…?

Ndugu yangu, swali la majina jumla na majina ya wingi lina utafiti mpana … na ikhtilafu kuhusu vigawanyo … bali kuna ikhtilafu katika kutekeleza hukmu zinazo fafanua jina jumla na jina la wingi kwa mujibu wa mbinu za magwiji wa lugha katika kugawanya nomino, ikiwemo:

Kwanza: kuna baadhi ambao huigawanya nomino (al Ism) katika nomino (ismu) mgando na nomino kusanyishi …

  1. Nomino (ismu) jumla imegawanyika katika:
  2. Ile inayo kusudia maana ya wingi, lakini nomino yake haina muundo wa umoja, lakini umoja wake uko katika maana yake, kama vile: qawm (watu), rah’t (familia), jeshi …
  3. Ile ambayo ni kinyume na miundo ya wingi, ambapo ni kuwa na muundo wa umoja wa neno lake, lakini kinyume na miundo inayo julikana ya wingi usio pangika, kama vile: rukkab ni wingi wa rakib (abiria).
  4. Ile ambayo huenda ikaambatanishwa nayo, ambapo ni kuwa na muundo wa umoja wa neno lake na kukubaliana na miundo ya wingi usio pangika, bali sawia na muundo wa umoja katika kuambatanishwa nayo, kama vile: rikaab katika uzani wa (Fi’aal) wa miundo ya wingi usio pangika, na ina muundo mmoja tu wa neno lake “rukuba” lakini imenasibishwa nayo kama umoja “rikaabi”, hivyo basi ni nomino ya wingi.
  5. Nomino (ismu) mgando imegawanyika katika:
  6. Nomino (ismu) jumla mgando ni ile inayo ashiria wingi katika maana ikikusudia ujumla na ina muundo wa umoja ambao ni wa kipekee kutokana nayo katika alama mbili:

– Taa marbuta “ah” kama vile: Nah’l (bees): Nah’lah, maneno (kalam): Kalimah, Tufah (matufaha): Tufaha, Shajar (miti): Shajarah, and Tamr (tende): Tamrah.

– Yaa “i” ya umilikaji, kama vile: Arab: Arabi, na Turk: Turki, na Zinj: Zinji.

  1. nomini jumla za kibinafsi, zinazo ashiria ujumla zilizo halali kwa uchache na wingi, kama vile: maji, maziwa, hivyo ni nomino (ismu) mgando ya kibinafsi.
  2. Nomino (ismu) mgando ya umoja kama vile simba, mbwa mwitu, mtu.
  3. Kama nilivyo kutajia mwanzoni, kuna ikhtilafu katika utekelezaji wa hukmu hizo za juu katika kuamua nomino (ismu) jumla na nomino (ismu) mgando, kwa mfano:
  4. Imekuja katika (al-Bahr al-muhit fi usul al-fiqh) 4/115: (Tatu: nomino (ismu) mgando ambayo hutofautishwa kutokana na hali ya umoja wake kupitia herufi Taa, sio shina wala haikuvuliwa kutokana nalo, kama vile tende (Tamr) na mti (Shajar), hii ndio maarufu; Namaanisha kuwa nomino (ismu) mgando. Al-Ghazali anaiita wingi, na Ibn Malik anaiita nomino (ismu) jumla, kwani ameikadiria kuwa katika nomino (ismu) jumla, lakini katika Sharh Kafiyah ameiita nomino (ismu) mgando…). Kama unavyoona katika vigawanyo hapo juu, wingi wa tende (Tamr) na mti (Shajar) ni Tamrah na Shajara mtawalia, yaani ni nomino (ismu) jumla, lakini hapa kuna tofauti baina ya maarufu (nomino (ismu) mgando), al-Ghazali (Wingi) na Ibn Malik (nomino (ismu) jumla).
  5. Imekuja katika Al-Sharh al-Kabir li-Mukhtasar al-Usul (uk. 155): [(Sheikh ametaja hapa kuwa neno (Al-kalimah) umoja wa Al-kalem. Na ambalo ni mashuhuri kwa wasomi wengi wa nahau ni kuwa al-kalem ni wingi wa al-kalemah na sio al-kalaam…

Wasomi hao wametofautiana katika “Al-kalem” je ni (nomino (ismu) mgando unganishi) au ni (nomino (ismu) mgando): al-Suyuti asema katika “Ham’ al-hawami'” (1/55): (Katika kufafanua at-tasheel cha Nadhir al-jaish, wasomi wa nahau wametofautiana katika neno (al-kalem), kundi moja akiwemo al-Juriani wanasema kuwa ni (wingi) wa al-kalimah huku al-Farsi na wachunguzi wengineo wakisema ni (nomino (ismu) mgando yake). Kama tulivyo sema katika nambari (a) tunasema tena hapa, kadhia hii inahusiana na wingi (kalem) ambao unatofautishwa na umoja wake (kalemah) kupitia Taa “ah” na bado kuna tofauti: kwa mujibu wa vigawanyo vya juu ni (nomino (ismu) mgando unganishi), lakini kwa mujibu wa al-Juriani ni (wingi) wa neno (al-kalimah) na ni (nomino (ismu) mgando) kulingana na al-Farsi.

Kama unavyoona, kuna ikhtilafu miongoni mwa magwiji wa lugha kwa kutegemea mtazamo wao katika vigawanyo vya nomino (ismu).

Pili: Kuna wale ambao hugawanya nomino katika jumla na ilivyo vuliwa:

1- Katika kitabu (Al-mahsool) cha mwandishi wake Abu Abdullah al-Taymi Razi aliyepewa lakabu ya Fakhr al-Din al-Razi Khatib Al-Ray (aliyekufa: 606 H)

(… Ama nomino ima ni thabiti (alam) au iliyo vuliwa (mushtaq) au nomino (ismu) mgando, lakini nomino thabiti sio majazi kwa sababu sharti la majazi ni iwe yaweza kugeuzwa kwa uhusiano baina ya asili na tagaa, ambalo hilo halipatikani katika nomino thabiti. Lakini, nomino iliyo vuliwa, isipokuwa ikiwa majazi inazungumzia neno lililovuliwa kutokana nayo, hayazungumzi lililovuliwa ambalo halina maana, bali ni kitu kilicho tokea kwa lililovuliwa kwayo, hivyo basi majazi kimsingi hayazungumzii isipokuwa nomino (ismu) mgando, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi).

2- Katika al-Bahr al-Muhit fi Usul al-Fiqh cha Abu Abdullah Badr al-Din Mohammed bin Abdullah bin Bahadur Zarkashi (aliyekufa: 794 H):

[Rai ya pili] [(nomino) jumla imegawanyika kwa mujibu wa muonekano wake katika iliyo vuliwa na nyenginezo]

“Kwa mujibu wa muonekano wake ima inaashiria dhati iliyo na sifa, katika hali hii basi itakuwa ni nomino iliyo vuliwa, kama “nyeusi”, hii huitwa “Sifah” katika msamiati wa magwiji wa nahau. Au haiashirii hilo, katika hali hii basi ikiwa itaashiriwa kupitia dhati hiyo hiyo pekee kuliko ilivyo kama nomino (ismu) mgando… Al Isfahani asema: kiashiria cha ujumla kimegawanyika katika nomino (ismu) mgando kama Simba (Asad), na nomino (ismu) mgando thabiti kama Usama (Simba), lakini haya si maneno yaliyo na maana sawa (mutaraadif), kwa sababu nomino (ismu) mgando imeundwa kwa ajili ya dhati jumla, na nomino (ismu) mgando thabiti imeundwa kwa ajili ya dhati hiyo kama inavyo jitokeza akilini…

3- Imekuja katika al-Muhadhab fi Ilm Usool al-Fiqh al-Muqaarin cha: Abdul Kareem bin Ali bin Mohammed al-Namlah (wa sasa)

Nomino (ismu) mgando pia imegawanyika katika: “nomino (ismu) mgando” na “nomino uliovuliwa”:

– Nomino (ismu) mgando ni: nomino inayo ashiria kitu maalumu, kama “farasi” na “mtu”.

– Nomino (ismu) iliyo vuliwa: ni nomino inayo ashiria sifa maalumu, pasi na ufafanuzi wa dhati hiyo kama vile: “mwendesha farasi”, na “msomi”, hii yaashiria kitu kilicho sifiwa na uendeshaji farasi na elimu.

Nomino (ismu) isiyo kamili imegawanyika katika “iliyo huru” na “isiyo huru”. Nomino huru isiyo kamili ni: nomino thabiti (ism alam) kama “Zaid”, ambayo haihitaji kufichika… nomino isiyo kamili na isiyo huru ni: dhamiri kama “mimi”, “wewe” na “yeye”.

Tatu: Katika kitabu Shakhsiya ya Kiislamu, Juzuu ya III, mlango wa “Maneno ya Kilugha na Vigawanyo vyake – Nomino (al Ism)”, tumegawanya nomino (ismu) katika njia hii, na kueleza:

(… Nomino ni ima jumla au isiyo kamili, kwa sababu ufahamu yake wake ima waweza kushirikisha (vitu) vingi  au usio ushirika, ikiwa ni aina ya kwanza, basi ni jumla, na ikiwa ni aina ya pili; ni isiyo kamili…

Nomino (ismu) jumla iko katika aina mbili: nomino mgando na nomino iliyo vuliwa (mushtaq), kwa sababu

– Ikiwa inaashiria kitu maalumu, kama farasi, mtu, na mengineyo ambayo yanaashiria dhati fulani, basi ni nomino mgando,

– Na ikiwa nomino jumla inaashiria kitu kilicho na sifa maalumu, basi ni nomino iliyo vuliwa (al mushtaq), kama nyeusi, mwendesha farasi, na mifano yake.

– Ama nomino isiyo kamili, ni aina mbili: nomino thabiti (ism alam) na dhamiri, nayo ni,

– Ikiwa neno litatoa maana kwa njia huru, bila ya kuhitaji chochote kuifafanua, basi hiyo ni nomino thabiti, kama Zaid na Abd Allah…

– Na ikiwa nomino isio kamili itakuwa haiko huru, yaani inahitaji kitu kuifafanua, basi hiyo ni (nomino) fiche (dhamiri), kama: yeye mwanamume na yeye mwanamke…) Mwisho

Kutokana na haya, neno linalo beba maana jumla linagawanyika sehemu mbili:

Ikiwa linaashiria kitu kisicho maalumu, bali linaashiria dhati fulani kama farasi, mtu na giza, basi ni nomino mgando… Na ikiwa nomino jumla inaashiria kitu kilicho na sifa maalumu, basi ni nomino iliyo vuliwa, kama nyeusi, mwendesha farasi na msomi, hivyo, nyeusi husifiwa kwa giza na mwendesha farasi husifiwa kwa uendeshaji farasi na msomi kwa elimu…

Kutokana na hayo, maneno (Ummah na kundi katika hali hii) huashiria vitu visivyo maalumu, Ummah yoyote, na kundi lolote… hakuna lolote kati yao lililo na sifa maalumu … hivyo basi ni nomino mgando na sio nomino zilizo vuliwa kwa mujibu wa ufafanuzi ambao tayari ushatajwa … Hili ndilo tunalolitabanni kuhusiana na vigawanyo vya nomino (jina), na kisha tumesema kuwa kundi na Ummah ni nomino mgando (jina lililo ganda) kama ilivyo elezwa katika ufafanuzi wa Kifungu cha 21 cha Kielelezo cha Katiba:

[Dalili yake ni maneno ya Mwenyezi Mungu (swt)

(وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Al-i-Imran: 104]. Upande wa kutumia aya hii kama dalili ya kuasisi vyama vya kisiasa ni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amewaamuru Waislamu kuwa na kundi linalo beba Da’wah kwa Uislamu miongoni mwao, na vilevile linalo tekeleza uamrishaji mema (Ma’ruf) na kukataza maovu (Munkar), hivyo maneno Yake (swt)

(وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ) “Na uwe kutokana na nyinyi Umma.” ni amri ya kuanzisha muundo wa kundi lililo na sifa ya kundi miongoni mwa makundi ya Waislamu, kwani Yeye (swt) amesema “miongoni mwenu”, na madhumuni ya maneno Yake ( swt)

(وَلْتَكُن مِّنكُمْ ) “Na uwe kutokana na nyinyi” ni kutaka kuibuke kundi miongoni mwa Waislamu na sio kuwa Waislamu wawe kundi; kwa maana nyengine, kuibuke Ummah miongoni mwa Waislamu, na maana yake sio kuwa Waislamu ndio wawe Ummah.

Hii ni kwa sababu neno “miongoni” (min) katika aya hii ni baadhi (tab’idh) na sio ufafanuzi wa nomino mgando, njia ya kutazama hilo ni kuwa neno “baadhi” (ba’dh) lapaswa liwe na uwezo wa kulibadilisha, hivyo yaweza kusemwa “Na paweko [paibuke] miongoni mwenu ummah (pote la watu)” huku neno ‘Min’ haliwezi kubadilishwa kwa “baadhi” katika aya hii (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ)  “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu” [An-Noor: 55] kwani haiwezi kusemwa kuwa “Mwenyezi Mungu amewaahidi baadhi walioamini miongoni mwenu” na hivyo katika hali hii ni kwa ajili ya kufafanua nomino mgando: katika maana nyengine, ni kuwa ahadi haikufungika na zama za maswahaba pekee (Mwenyezi Mungu awe radhi nao) bali ni kwa wale wote walioamini na kufanya matendo mema.

Haiwezi kusema kuwa aya hii inasema “Ummah”, kwa maana nyengine, chama kimoja, na kwamba hii yamaanisha kutokuweko na vyama vingi. Hili haliwezi kusemwa kwa sababu aya haikusema “Ummah moja”, hivyo haikutaja kundi moja bali imesema “Ummah” kwa muundo usiojulikana na pasi na sifa yoyote. Hiyo yamaanisha kuasisi kundi moja ni faradhi. Endapo kundi moja litaasisiwa basi faradhi hio itakuwa imetimizwa, lakini haiharamishi kuasisi makundi mengi au mapote mengi.

Utekelezaji wa faradhi ya kutosheleza kupitia kundi moja ambalo pekee linatosha katika kutekeleza, hakuharamishi kuwepo zaidi ya moja kutekeleza wajibu huo. Na neno kundi hapa ni jina la mgando, kwa maana nyengine, neno kundi limetumika na linalo kusudiwa kwalo ni mgando na sio mjumuiko mmoja; Mwenyezi Mungu (swt) asema

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ)  “Nyinyi mmekuwa bora ya Umma” [Al-i-Imran: 110]. Na lile linalo kusudiwa na mgando.

Na sambamba na hilo ni maneno ya Mtume (saw)

«مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ» “Yeyote anayeuona uovu (munkar) basi na aubadilishe” (imeripotiwa na Muslim kupitia Abu Sa’id Al-Khudri), hivyo madhumuni sio Munkar mmoja bali mgando wa Munkar, na kuna mifano mingi kama hiyo. Hivyo linabeba ukweli wa kundi moja na pia makundi mengi kutokana na mgando huo. Kutokana na hayo, hairuhusiwi kuzuia kuasisiwa kwa vyama vingi vya kisiasa. Hii ni kwa mujibu tu wa vile vyama vilivyo asisiwa juu ya msingi wa yale yaliyotajwa na aya hii; yaani kulingania kheri, kuamrisha mema (Ma’ruf) na kukataza maovu (Munkar) ambayo inajumuisha watawala na kuwahisabu watawala.] Mwisho.

Kwa taarifa hiyo, kuna magwiji wa lugha ambao wamesema kuwa neno (Ummah) ni nomino mgando (jina lililo ganda), na hivyo hivyo neno (Jama’ah) ni nomino mgando:

Inasemwa katika “Al Muharrer al-Wajeez fi Tafseer al-Kitab Al Aziz 1/488 m” na Ibn Atteyh Al-Andalusi (aliyekufa 542 H): “na wafasiri wametofautiana katika maana ya maneno Yake (swt): (كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ  أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ)  “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu.” [Al-i-Imran: 110]. Al Hassan bin Abi Hassan na kundi la wanazuoni wamesema: maana ya aya hii ni hotuba kwa Ummah kuwa wao ni taifa bora lililotolewa kwa watu, hivyo, neno Ummah (taifa), kwa msingi wa ufahamu huu ni nomino mgando kama ambao wameambiwa nyinyi ni taifa bora zaidi, na ufahamu huu unatiliwa nguvu kupitia wao kuwa mashahidi wa wanadamu… Qadi Abu Muhammad: Ummah (taifa) kwa msingi wa ufahamu huu ni nomino mgando …] Mwisho.

Natarajia jambo hili liko wazi sasa, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi na Yeye ni Mwingi wa hekima.

2 Muharram 1441 H

01/09/2019 M

Maoni hayajaruhusiwa.