Msisitizo wa Trump Juu ya OPEC, Hususan Juu ya Saudi Arabia, ili Kuongeza Uzalishaji na Kupunguza Bei za Mafuta

Swali:

Mnamo 2 Oktoba 2018, wakati wa mkutano wa uchaguzi wa muhula wa kati katika eneo bunge la Mississippi, Trump aliitishia Saudi Arabia na kuwaonyesha wafuasi wake kuwa alikuwa akipambana na bei za juu za mafuta: “… Na vipi kuhusu mikataba yetu ya kijeshi ambapo tunalinda mataifa tajiri na hatulipwi, vipi kuhusu hiyo mali “kwa maana ya mafuta”? Ambayo pia inabadilika… Tunailinda Saudi Arabia. Je, mutasema kuwa wao ni matajiri? Na nampenda Mfalme, Mfalme Salman. Lakini nilisema ‘Mfalme – sisi tunakulinda – huenda usiwepo hapo mamlakani kwa wiki mbili bila ya sisi – ni sharti ulipe kwa ajili ya ulinzi wako.’” (Khaleej Online, 03/10/2018).

Swali langu sio ni kwa nini watawala wa Saudi Arabia wanasalia kimya juu ya tusi hili, bali wamesalia watiifu kwa Amerika, ni kwa sababu ni wadogo machoni mwao wenyewe, na hivyo wamekulia wakizoea fedheha. Lakini swali langu ni kipi kinachomfanya Trump kuifuatilia Saudi Arabia kwa pupa ili kuongeza uzalishaji na kupunguza bei; ingawa Amerika ni mzalishaji mkubwa na inaweza kudhibiti upunguzaji bei yeye peke yake? Sasa kwa nini inasisitiza wakati huu? Na hatimaye, kwa nini, licha ya shinikizo hili lote la Amerika bei ya mafuta haijapungua?  Na Allah akulipe kheri.

 Jibu:

Ndiyo, umesema ukweli, anaye fedheheshwa amezoea kufedheheshwa, taarifa za Trump kuhusu watawala wa Saudi Arabia zatosha kuyaangamiza mahusiano na Amerika, ikiwa si juu ya hilo, bali ikiwa wanamuonea haya Allah, Mtume wake na waumini, lakini hawana haya, na Mtume wa kweli (saw) amesema:

« إِنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلَمِ النُّبُوَّةِ إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ »

“Hakika, miongoni mwa yale ambayo watu wameyatambua kutoka katika maneno ya mitume ni: ikiwa huna haya, basi fanya utakavyo.”[Al-Bukhari]

Ama kuhusu jibu la swali lako au maswali yako, ni kama ifuatavyo:

  1. Pindi Trump alipoingia afisini mnamo Januari 2017, bei za mafuta zilikuwa takriban $57 kwa pipa. Kufikia Juni 2017, bei za mafuta zilishuka hadi $45 kwa pipa, lakini tangu hapo zimeendelea kupanda. Leo, bei ya mafuta ni $86 kwa pipa la mafuta ghafi na baadhi ya wadadisi wanatarajia bei za mafuta kufikia $100 kwa pipa!

Mnamo 5/7/2018, Trump aliandika katika mtandao wa Twitter: “Shirika la kikiritimba la OPEC ni lazima

likumbuke kuwa bei za gesi ziko juu na wanafanya juhudi chache kusaidia. Kama kuna chochote, basi

wanazisukuma bei juu zaidi huku Amerika ikiwatetea wengi wa wanachama wake (yaani wanachama wa OPEC) kwa dolari chache. (Uhusiano) huu ni lazima uwe wa pande mbili (yaani tunawasaidia kwa badali ya bei ya chini ya mafuta) … PUNGUZENI BEI  SASA!” Kabla ya hapo mnamo 30 Juni 2018 alisema katika maandishi yake katika mtandao wa Twitter: “Hivi punde nimezungumza na Mfalme Salman wa Saudi Arabia na kumweleza kuwa, kwa sababu ya ghasia na sokomoko nchini Iran na Venezuela, naiomba Saudi Arabia iongeze uzalishaji mafuta, pengine hadi mapipa 2,000,000, ili kufidia tofauti … Bei ziko juu sana! Amekubali!” (Al-Hura: 30/6/2018)

Mnamo 25/9/2018 Raisi wa Amerika aliishambulia OPEC katika hotuba yake katika Kongamano Kuu la UN na kusema: “OPEC na mataifa ya OPEC, kama kawaida, yanauvuna ulimwengu wote, na hili silipendi. Hakuna yeyote anayepaswa kulipenda hili. Tunayapa ulinzi mengi ya mataifa haya bure bilashi, na kisha kututumia kwa kutupa bei za juu za mafuta … tunawataka waanze kupunguza bei … Hatutazivumilia tena bei hizi mbaya.” (Sputnik, Septemba 25, 2018), na mnamo 27/9/2018, Trump aliandika katika mtandao wa Twitter “Tunazipa ulinzi nchi za Mashariki ya Kati, haziwezi kuwa salama kwa muda mrefu bila ya sisi, na huku zinaendelea kusukuma bei za mafuta juu na juu zaidi! Tutakumbuka. Shirika la kikiritimba la OPEC ni lazima lishukishe bei sasa!”

Kama ilivyoelezwa katika jibu la swali mnamo 2/10/2018 katika muhula wa kati wa mkutano wa kampeni ya uchaguzi katika eneo bunge la Mississippi, Trump ameitishia Saudi Arabia na kuwaonyesha wafuasi wake kuwa anakabiliana na ongezeko la bei: “… Na vipi kuhusu mikataba yetu ya kijeshi ambapo tunayalinda mataifa tajiri na hatupati malipo, vipi kuhusu bidhaa hiyo “yaani mafuta”? Hilo pia linabadilika wenzangu … Tunailinda Saudi Arabia. Je, utasema wao ni matajiri. Na nampenda Mfalme, Mfalme Salman. Lakini nilimwambia ‘Mfalme – sisi tunakulinda – huenda usiweko mamlakani kwa wiki mbili tu bila ya sisi – ni lazima ulipie ulinzi wako.” (Khaleej Online, 03/10/2018).

 Yote haya yamaanisha kuwa kinachomtia wasiwasi Trump, ni hali zilizoko sasa, katika kuongeza uzalishaji, lakini kutoka OPEC, hususan kutoka Saudi Arabia.

  1. Ndiyo, Amerika ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi, kwa mujibu wa Idara ya Habari za Kawi ya Amerika (EIA), shirika la Amerika linayokusanya takwimu za kawi. Mwishoni mwa 2017, EIA ilichapisha jedwali la uzalishaji wa mafuta duniani, ambapo wakati huo ilikuwa ni mapipa milioni 95 kwa siku. Kwa mujibu wa jedwali hilo, nchi saba zinazoongoza kwa uzalishaji ni kama zifuatazo:

Amerika: mapipa milioni 14.46 kwa siku ya jumla ya uzalishaji wote duniani, Saudi Arabia: milioni 12.08, Urusi: milioni 11.18, Canada: milioni 4.87, Iran: milioni 4.67, Iraq: milioni 4.48, China: milioni 4.45.

 Amerika inabakia kuwa mzalishaji mkuu wa mafuta duniani, ikifuatiwa na Saudi Arabia na Urusi

3 – Na ndiyo, Amerika inaweza kuongeza uzalishaji kama ipendavyo, hususan kwa kuwa ina akiba kubwa ya mafuta ya shale, lakini kuna kitu kinachoizuia kufanya hivyo:

a – Kudumisha akiba na hifadhi zake

b – Kuna Ruwaibidha (watawala waovu) wanaotekeleza maagizo yake hata kama wanatusiwa katika jambo hili. Wao hata hutekeleza hili huku likiwa na madhara kwao, kama ilivyo kwa watawala wa Saudi Arabia!! Amerika inaitaka Saudi Arabia kupunguza bei za mafuta ili kuwapa watu wake bei za chini kabisa baada ya bei ya mafuta ghafi ya Brent kufikia kiwango cha kiulimwengu cha takriban $80 kwa pipa katika mwezi wa tisa mwaka huu. “Mnamo 14/9/2018 kiwango cha kiulimwengu cha mafuta ghafi ya Brent kiliongezeka na kuwa $78.21 kwa pipa, ongezeko la juu zaidi tangu 22/5/2018” … (Reuters 14/9/2018). Tambua kuwa “uzalishaji wa OPEC uliongezeka hadi mapipa milioni 32.79 kwa siku. Saudi Arabia, iliyo ahidi dhamira ya ongezeko katika uzalishaji wake, ilisema kuwa uamuzi huo utapelekea ongezeko la uzalishaji kwa takriban mapipa milioni moja kwa siku” (Reuters, 31/8/2018). “Pindi mafuta ghafi ya Brent yalipokuwa yakielekea $80 kwa pipa, Saudi Arabia ililiarifu soko kuhusu kuongeza uzalishaji wake mwezi uliopita mapema kuliko tarehe ambayo habari hiyo kwa kawaida hutangazwa,” imenukuliwa kutoka chanzo chake.

Serikali ya Saudi ni kibaraka imara wa Amerika na iko kuihudumia. Saudi Arabia daima imecheza dori muhimu sana katika kuimarisha soko la mafuta … Saudi Arabia, inahitaji bei za juu za mafuta wakati huu, ambapo uchumi wake uko katika shinikizo hatari la kiuchumi tangu kuanguka kwa bei ya mafuta mnamo 2014. Hususan kwa kuwa mafuta ndiyo pato kuu katika bajeti ya Saudi Arabia. Ni maarufu kuwa katika nchi ambazo mapato ya mafuta yanajumuisha zaidi ya nusu ya mapato yao, wanahitaji bei za mafuta ziwe juu ya $80 kwa pipa kuweka uzani sawa wa bajeti yao – mapato ya kutosha ya mafuta ili kumudu matumizi ya bajeti – hali iko vipi ikiwa bajeti ya Saudi Arabia imejengwa kikamilifu juu ya mapato ya mafuta? Bei maridhawa iko juu ya $80, hata karibu na $100 ili kuweka mizani sawa bajeti yake, na kuimarisha uchumi wake, kwani kwa sasa unayumba. Lakini, mtawala wake anakubali kuongeza uzalishaji ili kupunguza bei, bila ya kujali madhara yanayofanyiwa nchi hiyo ili kumridhisha Trump, ambaye amemtusi mtawala wa Saudi hadharani, kuwa lau si Amerika, utawala wake ungekuwa umeporomoka!! Wanalifungia macho hili na mfalme wao mtarajiwa kusema kuwa Saudi Arabia iko tayari kufidia upungufu wa Iran! Mnamo 6/10/2018 Shirika la Habari la Bloomberg liliripoti taarifa za mfalme huyo mtarajiwa Bin Salman: Alisisitiza kuwa Saudi Arabia imetimiza ahadi yake ili kufidia kutoweka kwa usambazaji mafuta ghafi wa Iran,” na akasema: “Saudi Arabia kwa sasa inazalisha takriban mapipa milioni 10.7 kwa siku – karibu na rekodi – na kuongeza milioni 1.3 zaidi endapo soko litahitajia hilo …”

Maadamu kuna kibaraka wa Amerika aliye tayari kujidhuru ili kufikia matakwa ya Trump ya kuongeza uzalishaji, ni kwa nini basi Amerika itumie hifadhi zake?

4- Kwa nini msisitizo huu wa Trump kwa OPEC, na hususan Saudi Arabia ili kuongeza uzalishaji na kupunguza bei? Ni kwa sababu kuna vitu viwili vinavyo jumuisha kizungumkuti cha haraka kwa Trump ambaye anataka kitatuliwe kwa haraka, vyenginevyo Trump haathiriwi na ongezeko la bei … Amerika yaweza kudhibiti ongezeko hilo kupitia kuchapisha dolari mpya, kama ilivyo fanya pindi kulipokuwa na ongezeko la nyuma la bei kwa takriban $150. Tulitoa katika jibu la nyuma la swali mnamo 16/5/2009: “kwamba Amerika yaweza kuchapisha noti, kwa idhini ya Hazina ya Fedha Ulimwenguni (IMF) au kwa siri, “hata hadharani” bila ya ridhaa yake, kwa kuwa ina ushawishi imara katika Hazina hiyo, na yaweza kuonyesha sababu za kirongo na kuficha ukweli wa mambo, na yaweza kupata usaidizi wa Hazina hiyo! Lakini uchapishaji wa noti kwa njia hii hupelekea kushuka thamani kwa dolari, na mkurupuko wa bei, yaani ongezeko la bei. Hii ndiyo sababu Amerika haichukui hatua hii isipokuwa ikiwa ina maslahi ndani yake. Kwa mfano, imeripotiwa kuwa Amerika ilichapisha kati ya “trilioni 2 – trilioni 4” wakati wa shauku ya mafuta, iliyo sababisha ongezeko la bei kwa karibu $150 kwa pipa, “na Amerika haikuwa mbali na shauku hiyo”. Amerika ilichapisha noti hizi ili kununua kiwango kikubwa kabisa cha mafuta kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja ili kuongeza akiba yake, ililiona hili kuwa la manufaa kuliko bei za juu na kuporomoka kwa dolari …” lakini kwa sababu inachukua muda kupangilia uzalishaji wa “mandhari” hii! Na kwa sababu kadhia mbili hizi zahitaji suluhisho la haraka au vyenginevyo Trump ataanguka ndani ya matatizo kama tulivyo taja awali. Hivyo, Trump alighadhabishwa na OPEC, na hususan Saudi Arabia …

Hivi ndivyo vizungumkuti viwili:  

Cha kwanza: Kadhia ya vikwazo juu ya Iran:

Iran ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa mafuta ghafi katika OPEC baada ya Saudi Arabia na Iraq, uzalishaji wake ni takriban mapipa milioni 4 ya mafuta ghafi kwa siku. Vikwazo hivyo vitapelekea uhaba wa usafirishaji mafuta ya Iran, hususan mnamo Novemba, ambapo vikwazo vinaongezeka ikiwemo Iran pamoja na waagizaji mafuta kutoka Iran. Amerika imeziagiza kampuni kukata uagizaji mafuta kutoka Iran kwanza, na kisha kufutilia mbali mikataba yao na Iran Novemba ijayo, itakayo pelekea kupungua kwa ushafirishaji bidhaa ng’ambo wa Iran. Lakini Saudi Arabia yaweza kuongeza uzalishaji wake wa mafuta endapo kuna haja, maana yake ni kuwa imejitayarisha kufidia uhaba wa usambazaji wa Iran. Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Mohammad bin Salman alisema: “Hivi karibuni tunasafirisha kadri ya mapipa mawili kwa pipa lolote linalopotea kutoka Iran,” mwanamfalme huyo alisema. “Kwa hivyo tumefanya kazi yetu na zaidi.” Kwa sasa Saudi Arabia inatoa takriban mapipa milioni 10.7 kwa siku – karibu na rekodi – na yaweza kuongeza milioni 1.3 zaidi endapo soko litahitaji hilo.” (https://www.akhbarak.net, 08/10/2018).

Mnamo 4/11/2018, Amerika inapanga kuongeza vikwazo dhidi ya Iran, ikilenga usafirishaji mafuta ng’ambo na kuzitia shinikizo serikali na makampuni kote ulimwenguni kuzingatia na kupunguza ununuzi kutoka Iran. Hii yamaanisha kuwa usambazaji mafuta utapungua katika soko la kiulimwengu. Kama ilivyo taarifa ya nchi saba kuu za uzalishaji mafuta iliyotajwa juu, Iran ilikuwa ikizalisha zaidi ya mapipa milioni 4 ya mafuta kwa siku” na sasa hii imeshuka.” Nusu ya mafuta hayo ndiyo yanayo zalishwa, China, India na Uturuki, hupokea kutoka kwake karibia mapipa milioni 2. Trump anataraji hatua za vikwazo hivyo zitaondoa milioni 2 hiyo. Amerika inataka kuifidia kupitia Saudi Arabia na nchi nyengine za OPEC kufidia upungufu huo unaotarajiwa, ili Amerika iweze kuwasilisha kadhia ya Iran kando na Ulaya, Urusi na China baada ya kutangaza kujiondoa kwake mnamo 8/5/2018 kutoka katika makubaliano ya nuklia yaliyotiwa saini miaka mitatu iliyopita na nchi hizi. Ilikubali makubaliano na Iran pekee. Raisi wa Amerika ametangaza kuwa tayari kwake kufanya makubaliano kama hayo, lakini masharti yake ni lazima yaundwe ndani ya Iran. Hili laweza kuchukua muda mrefu … Trump anataka kufidia uhaba huu hadi pale atakapo weza kuandaa makubaliano kati ya Amerika na Iran bila ya kuihusisha Ulaya, endapo uhaba huo utaendelea kuwepo bila ya fidia na kisha bei kuongezeka, hili litamueka yeye matatani. Kwa sababu yeye ndiye aliyeunda vikwazo hivyo kwamba ukosefu wa mafuta ya Iran kama natija ya vikwazo hivyo itafidiwa na vitisho vyake kwa OPEC, hususan Saudi Arabia … kwa maana nyengine, Amerika inataka kuwasilisha kadhia ya ukosefu wa usambazaji wa mafuta na kuhakikisha kuwa hautokei hadi matatizo haya na Iran yatatuliwe, kwa sababu hili huenda lisiwe kwa haraka.

Hivyo basi, Trump anaisisitiza OPEC na kimsingi Saudi Arabia kufidia upungufu wa usambazaji wa Iran, ambao utakuwa dhahiri mnamo 4/11/2018, ikiongezewa na upungufu uliosababishwa na vikwazo mnamo 21/05/2018 vilivyo wekwa na Trump juu ya Venezuela, hata kama ushawishi wake ni mchache. uzalishaji wake wa sasa ni mapipa milioni 1.5 kwa siku.

Cha pili ni uchaguzi wa Amerika:

Kupandisha bei za mafuta humsababishia Donald Trump, ambaye atasimamia uchaguzi wa muhula wa kati mnamo Novemba. Bei za juu za mafuta zitawaweka wafuasi wake afisini, hususan kwa kuwa kura nyingi za maoni zaonyesha kuwa Democrats watalidhibiti Bunge. Ili kuwaonyesha wapiga kura wa Amerika kuwa anaiweka Amerika mbele, anaweka lawama na shinikizo juu ya Saudi Arabia na wanachama wa OPEC ili kuongeza uzalishaji. Wakati huo huo, utawala wa Trump unailazimisha China, India na Uturuki kuvunja mafungamano na Iran na kutafuta mafuta ghafi kwengineko. Ongezeko la bei za mafuta pia la athiri kiasi cha bei ambayo wanunuzi wa Amerika wanalipia mafuta. Kwa uchaguzi huu wa muhula wa kati, hili halitakuwa jambo la kushindia. Hisia za Waamerika kwa ongezeko la bei za mafuta ziko juu, na hawawezi kukubali kuwa serikali yao iongeze bei za mafuta, kwa hivyo Raisi Trump anarusha lawama ya bei za juu kwa dola za Ghuba na OPEC na kuzishambulia ili kuwaonyesha Waamerika kuwa anatetea maslahi yake na anaweza kuishinikiza Saudi Arabia na OPEC ili kupunguza bei. Ameshughulishwa na kushukisha bei hiyo, hususan katika kipindi cha uchaguzi wa Amerika. Hili ni muhimu leo kwa Raisi wa Amerika na mahitaji ya chama chake cha Republican ili kupata kura za wapiga kura wa Amerika katika uchaguzi wa muhula wa kati wa Novemba 6, 2018 hususan kwa kuwa kura za maoni zinawafadhilisha Democrats.

5- Ni kwa nini bei za mafuta zaendelea kuongezeka licha ya vitisho vya Trump na shinikizo lake na jibu la Saudi Arabia? Sababu ni kuwa kuna wahusika wengine katika OPEC wafuasi wa Ulaya na katika mzozo na Amerika, na kuna Urusi vile vile, na pande hizi, hususan zile zinazo nasibishwa na Ulaya, si rahisi kuijibu Amerika isipokuwa kwa kiwango ambacho hakitafikia matarajio ya Trump kwa haraka kama anavyotaka. Saudi Arabia ni ala kuu ya Amerika ndani ya OPEC, lakini kuna wengine ndani ya OPEC wana maslahi maalumu, wakiwemo wale wafuasi wa nchi kubwa za Ulaya, na huenda wasiitii Amerika kwa urahisi, pamoja na kuwa kuna nchi washirika wa OPEC kama Urusi zilizo na maslahi maalumu. Amerika haiwezi kulazimisha matakwa yake kikamilifu.

Katika jaribio la kupunguza bei, raisi aliagiza kuongezwa kwa uzalishaji. Lakini, OPEC na washirika wake katika uzalishaji hawakufikia makubaliano katika mkutano wao nchini Algeria mnamo 23/9/2018 juu ya kuongeza zaidi katika uzalishaji wa mafuta, kinyume na wito wa Trump. Ama kuhusu Urusi, Amerika ilifaulu mnamo 2017, na hadi leo kuitumia Saudi Arabia ili kuishinikiza Urusi na kuifedhehesha na kuijibu kwa kuongeza uzalishaji na kisha kupunguza bei … Ni mara ya kwanza kwa mfalme wa Saudi kuzuru Urusi ili kuhudhuria mkutano mnamo Oktoba, 2017 kati ya OPEC na wanachama wasio wa OPEC, hususan Urusi, mnamo Oktoba 2017, mfalme Salman alizuru Urusi na kuhudhuria mkutano wa OPEC. Bei za mafuta kisha zilianza kumakinika juu ya $60 kwa pipa kabla ya kuongezeka tangu katikati ya mwaka wa 2018, kama ilivyo elezwa awali. Lakini, Saudi Arabia na Urusi ziling’ang’ana kufikia matakwa ya mapipa milioni 2 kwa siku yaliyo agizwa na Trump. Bali, wadadisi huru pamoja na Shirika la Kimataifa la Kawi (IEA) wanashuku kuwa Saudi Arabia na Urusi huenda wakaongeza mapipa milioni 2 kwa siku. Shirika la Kimataifa la Kawi (IEA), kampuni iliyo na makao yake Paris inayo wakilisha nchi wanunuzi, hivi majuzi ilikadiria kile ilichokiita “usambazaji kwa mahitaji madogo” kutoka Mashariki ya Kati, ikiwemo Saudi Arabia, kwa mapipa milioni 1.14 kwa siku.

Urusi huenda ikaongeza hadi mapipa 400,000 kwa siku, wadadisi wanasema. Mwishowe, chini ya shinikizo la kudumu kutoka Amerika, Saudi Arabia ilifikia makubaliano na Urusi mnamo Septemba kuongeza uzalishaji wa mafuta. “Makubaliano hayo yanaeleza kuwa Urusi na Saudi Arabia zinaendelea kutoa uamuzi wa sera za uzalishaji mafuta kabla ya kuwashauri wanachama wengine wa OPEC,” duru hizo zilisema kuwa Waziri wa Kawi wa Saudi Khalid al-Falih na mwenzake wa Urusi Alexander Novak walikubaliana wakati wa misururu ya mikutano juu ya kuinua uzalishaji kuanzia Septemba hadi Disemba, huku bei ya mafuta ghafi ikiwa takriban $80 kwa pipa. Duru hiyo ilisema: “Warusi na Wasaudi wamekubaliana kuongeza uzalishaji mafuta sokoni kimya kimya, ili wasionekane kana kwamba wanatekeleza maagizo ya Trump kwa kuzalisha mafuta zaidi.” Duru nyengine ilisema: “Waziri wa Saudi alimwambia Waziri wa Kawi wa Amerika Rick Perry kuwa Saudi Arabia itaongeza uzalishaji endapo wateja wake watahitaji mafuta zaidi.” (www.reuters.com).

Pengine mtu anashangaa ni kwa nini Urusi ijiunge na Amerika katika kuzuia bei za juu za mafuta, hata ingawa bei za juu ni kwa manufaa ya Urusi? Ili kujibu swali hili, uchunguzi wa ukweli huu waonyesha kuwa Urusi inaunga mkono bei ya mafuta ya $65 kwa pipa, kwa sababu hii ndiyo bei ya mizani sawa ya sekta ya mafuta ya Urusi, bei za juu zitazifanya nchi zinazo agiza mafuta kushindwa kumudu kuyanunua hatimaye kupelekea kuporomoka kwa upande wa kuyahitaji, ambayo itaidhuru sekta ya mafuta ya Urusi.

Kwa hali yoyote ile, Urusi haiko katika hatari kubwa katika hesabu hii, lakini kile kinacho athiri kihakika hesabu hii ni wale wanachama wa OPEC wa mrengo wa Ulaya. Si rahisi kutekeleza yale ambayo Trump anaagiza isipokuwa kwa shinikizo kubwa sana … Lakini, bei hazitarajiwi kuongezeka hadi 100, kwa kuwa nchi zinazo agiza mafuta haziwezi kuhimili hilo, na mahitaji yatashuka na kisha ongezeko hilo kusimama na kuanguka … hamu ya Trump ni kupunguzwa kwa bei wakati wa kipindi cha uchaguzi na baada yake, yaani kufikia mwishoni mwa mwaka huu ambapo haitarajiwi kuwa kadhia ya makubaliano ya nuklia itakuwa imeanza kuelekea katika makubaliano ya pande mbili kati ya Iran na Amerika bila ya Ulaya, na shinikizo la Amerika juu ya ongezeko la uzalishaji litamalizika na hivyo bei kuzunguka katika $80 kwa pipa … Kinachotia uchungu zaidi ni kuwa nguvu kutoka nje utumia rasilimali za ulimwengu wa Kiislamu kucheza michezo dhidi ya wao kwa wao, huku watawala wetu Ruwaibidha wakifuata kiupofu sera hizi na pasi na heshima yoyote kwa hadhi ya Umma huu. Tambua kuwa hifadhi nyingi za mafuta ya kiulimwengu ziko katika ardhi za Kiislamu, ima biladi za Kiarabu, Iran, barani Afrika, kama Nigeria au Asia ya Kati kama vile Kazakhstan, Turkmenistan au Caucasus, kama nchini Azerbaijan, lakini usafirishaji huo wa mafuta ng’ambo hauko mikononi mwa watu wake, ambao wengi wao wanateseka na umasikini na uchochole. Watawala, familia zao na wapambe wao wanayafuja na kuficha pesa ng’ambo. Pindi Amerika ilipoiomba Saudi Arabia mwaka jana wakati wa ziara ya Trump nchini Saudi Arabia mnamo 21/5/2017, kima cha dolari bilioni 460 familia ya Saud ilikuwa tayari kutekeleza matakwa yake na kulipa kiwango hicho. Hivyo basi, Waislamu hawataokoka na janga hili isipokuwa kupitia kwa Khalifa muongofu mithili ya Al-Farouq, Omar Ibn al-Khattab aliye gawanya utajiri kwa watu kwa usawa, na akaanza na masikini na kumalizia na Khalifa, ambaye ndiye wa mwisho kuchukua na kula. Mtume, mkweli (saw) amesema:

« كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ الِْمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ »

“Nyote ni wachungaji na nyote mutaulizwa juu ya mulivyo vichunga. Imam (mtawala) ni mchungaji na ataulizwa juu ya raia wake” [Bukhari]

Yeyote anaye wahadaa watu wake, adhabu yake ni kali kama alivyo sema Mtume (saw) katika Hadith iliyo simuliwa na At-Tabarani katika Al-Kabeer:

« مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَُّ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ غَاشّاً لِرَعِيَّتِهِ إِلا حَرَّمَ اللَُّ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ »

 “Hakuna mja yeyote anayetawalishwa na Allah kwa raia, akafa siku ya kufa kwake akiwa amewadanganya raia wake, isipokuwa Allah atamuharamishia Pepo juu yake.”

Hawa ndio watawala Ruwaibidha; wachache wa kufikiri na kudiriki!

11 Safar Al-Khair 1440 H

20/10/2018 M

Inatoka Jarida la Uqab: 23    https://hizb.or.tz/2018/12/01/uqab-23/

Maoni hayajaruhusiwa.