Minasaba Mwezi wa Swafar

1.Jaribio la kumuuwa Mtume SAAW.
Viongozi wa Makureish walikutana kujadili ajenda ya hatari katika tareekh kwa kuchagua kijana mmoja kutoka kila kabila la kikureish ili vijana hao kwa pamoja washirikiane kumuuwa Mtume SAAW. (26 Saffar, Mwaka wa 14 wa Utume)

2.Ghazwatu al- Abwa /Waddan
Kwa mara ya kwanza tangu Mtume SAAW asimamishe dola aliongoza kikosi cha watu 70 katika Muhajiriina kwa lengo la kudhoofisha uchumi wa Makureish na kuandaa mazingira ya vita dhidi yao (2. AH kabla ya Vita vya Badr)

3.Sarriya ya Aban bin Said
Kikosi hiki kilitumwa kwenda Najd kuwatia khofu mabedui wa huko. Kiliporudi Waislamu tayari wameshaifungua Khaybar (Mwaka wa 7AH)

4.Tukio la msiba wa Al-Rajii
Kuuwawa kwa khiyana na kikatili kwa Masahaba 7 au 10 na makabila ya Adal na Qaara kwa kula njama na kabila la Bani Lihyan baada ya kumtaka Mtume SAAW awape watu hao wakawafundishe dini kwao (Mwaka wa 8AH baada ya Vita vya Uhud)

5.Msiba wa kisima cha Mauna
Watu wa Najd chini ya dhamana ya Abu Barai Amir bin Malik waliomba wapewe masahaba wakalinganie kwao. Watu hao wakapewa maswahaba 40 au 70 . Kwa khiyana makabila ya Uswaya, Dhakwan na Raali wakawazunguuka maswahaba hao na kuwauwa wote (Mwaka wa 8AH baada ya Vita vya Uhud)

6.Kutumwa kikosi cha Ghalib bin Abdillah
Kikosi cha watu 200 kilitumwa eneo la wafuasi wa Bashir bin Saad katika mji wa Fadak (Mwaka wa 8.AH)

7.Kutumwa kikosi cha Qutba bin Amir
Mtume Saaw alituma kikosi cha watu 20 kwa kabila la Khaitham lilioko Tabala karibu na Turba. Qutba alikufa shahid katika vita hivi (Mwaka wa 9AH)

8.Kusilimu kwa Msafara wa Udharah
Ujumbe wa watu 12 wa kabila la Bani Udharah ulikuja kusilimu Madina ( 9 AH)

9. Kuandaliwa kwa kikosi cha Usamah bin Zaid
Mtume SAAW aliandaa kikosi hiki siku chache kabla ya kufariki kwake ili kupambana na Warumi (Mwaka wa 11 AH)

10. Kutumwa kikosi cha Ghalib binAbdillah Al-laith
Kikosi hiki kilitumwa kwa kabila la Bani Al-Muluh kukabiliana na uchokozi wao. Waislamu waliweza kuwauwa wengi wao na kupata ngawira nyingi. (Tukio hili lilitokea amma katika Safar au Rabiul Awwal Mwaka wa 7AH)

11.Kuibuka kwa Vita vya Siffin (1 Saffar Mwaka wa 36 H)

12.Kuuwawa kwa Amar bin Yassir (9 Saffar Mwaka wa 37 AH)

13.Kufariki dunia Muhammad bin Abu bakar (7 Saffar Mwaka wa 50 AH)

14.Kufariki Imam Hassan bin Ali (7 Saffar Mwaka wa 50 AH)

Maoni hayajaruhusiwa.