Oktoba 14 Siku Ya Mashujaa au Siku Ya Mabalaa?

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia nafasi ya wakoloni wa kale yaani Uingereza na Ufaransa ilidhoofika kimataifa. Badala yake dola ya Marekani ikaja juu kiushindani kuondosha athari ya madola mawili hayo kiulimwengu.

Uingereza ikaja na mikakati kadhaa kuhami ubwana wake katika makoloni yake, kama vile mbinu ya kumakinisha Jumuiya yake ya Madola pia kumakinisha mtandao wake wa elimu katika mashule na vyuo ili kuzalisha vibaraka atakaowapa uhuru bandia ili kuhifadhi athari yake.

Mabingwa wa kiengereza katika tasnia ya elimu ndani ya makoloni ya Uingereza kama Lord Crommer ndani ya Misri na Lord Macaulay ndani ya India waliweka bayana kwamba dhamira ya mfumo wa elimu ya kiengereza ni kuwabakisha wazawa wa makoloni yao kuwa wazawa katika rangi tu, lakini wabadilishwe kuwa waingereza katika kila mtazamo wao.

Chuo cha Makerere cha Uganda katika Afrika ya Mashariki ni kimoja katika mifano mingi ya mkakati huo. Aidha, Nyerere ni mmoja wapo wa vibaraka wengi ndani ya mchakato huo. Ndio maana Uingereza ilikuja haraka kumnusuru Nyerere mwanzoni mwa miaka ya sitini palipofanywa jaribio la kumpindua.

Vile vile Nyerere kwa kushirikiana na Zubeiri Mtemvu ndio waliotumwa na Uingereza kwenda haraka Zanzibar kufanikisha muungano wa jumuiya za Afro na Shirazi kisha kuzaliwa chama cha kisiasa cha Afro Shirazi Party.

Chama cha Afro Shrazi ndicho kilichofanikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa agizo la Uingereza. Na vile vile chama hicho kwa agizo la Uingereza kilipandikiza chuki na husuma baina ya Waislamu wa Zanzibar.

Kwa upande wa Tanganyika Nyerere kwa agizo la Uingereza aliwafanya Waislamu kuwa raia wa daraja duni. Lakini kubwa zaidi Nyerere akaibakisha nchi katika himaya ya Uingereza kwa jina la uhuru bandia. Huku akiwapa mambwana zake kila fursa katika kuzoa rasilmali za nchi , ilhali raia wa kawaida miongoni mwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu wakihangaika kwa dhiki na mashaka.

Uingereza ilipoona haiwezi kuhimili mikikimikiki ya Marekani ndani ya Tanzania ilimuamuru kibaraka wake aondoke asije akadhalilika, na akijifanya kang’atuka. Na mara baada ya kung’atuka Tanzania ikatoka katika himaya ya Uingereza na kuingia rasmi katika himaya ya Marekani hadi leo hii.

Maoni hayajaruhusiwa.