Miezi Mitatu Mitukufu Inafuatana: Tujipindeni Kufanya Kheri ikiwemo Kheri Kubwa ya Kufanya Kazi ya Kuleta Mageuzi Msingi

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّہُورِ عِندَ ٱلَّلِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَہۡرً۬ا فِى ڪِتَٰبِ ٱلَّلِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٲتِ وَٱلَۡرۡضَ مِنۡہَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُ مۚ ذَٲلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّ مۚ فَلَ تَظۡلِمُواْ فِيہِنَّ أَنفُسَڪُمۡ)

“Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mitukufu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu.” [At-Taubah: 36]

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakr (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:

“Mgawanyiko wa wakati umerudi katika asili yake kama ilivyo sasa namna Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili kati ya hiyo minne ni mitukufu. Mitatu inafuatana Dhul-Qa’da, Dhul-Hijja na Muharram, na wa nne ni Rajab (wa kabila) la Mudar unaokuja baina ya Jumada II na Shaaban.”

[Sahih Bukhari]

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’eed (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:

“Leo sio siku tukufu katika siku zenu tukufu, mwezi huu sio mtukufu katika miezi yenu mitukufu, ardhi hii sio tukufu katika ardhi zenu tukufu? Damu zenu na mali zenu ni tukufu kama ilivyo siku yenu hii ya leo ndani ya mwezi huu wenu. Je nimefikisha (ujumbe)?’ Wakajibu: “Ndio.” Akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu, shuhudia.”

[Ibn Majah]

Tukijaaliwa kufika Ijumaa ijayo tutakuwa tumo ndani ya mwezi mtukufu wa Dhul-Qa’da ambao ukimalizika unakuja Dhul-Hijja mwezi wa mwisho katika kalenda yetu tukufu ya Kiislamu nao pia ni mtukufu. Na baada yake utafuata mwezi wa kwanza wa Muharram nao pia ni mtukufu. Hakika itakuwa ni fursa ya kipekee kuweza kuishuhudia miezi hiyo ambayo ndani yake kila jema unalolifanya linakuwa na ubora mara dufu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Na miongoni mwa mema ya kupatiliza ni kuiendea mbio kadhia nyeti ya kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kufanya kazi ya kusimamisha serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa

njia ya Utume ndani ya moja ya nchi za Waislamu katika ulimwengu wa Waislamu. Mbio hizi ni pamoja na kuusoma Uislamu kwa sura ya kimfumo, kuufahamu, kuutekeleza na kuulingania ili uweze kuchukua nafasi ya mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali unao tawala dunia leo na ambao unaendeleza ukandamizaji, umwagaji damu na uporaji wa rasilimali za Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika kila pembe ya dunia.

Ni katika miezi hii mitukufu sisi Waislamu ndipo tunapotakiwa kuzidisha juhudi zetu za ulinganizi wa kusimamisha Khilafah kwa kuwa ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na bishara kutoka kwa Mtume (saw). Kinyume chake ni hasara kubwa kwa kila ambaye yuko mbioni kuweka vikwazo kwa da’wah hii ikiwemo kushirikiana na watawala vibaraka ndani ya ulimwengu wa Waislamu na usiokuwa wa Waislamu ili kuwapotosha watu ili wabakie katika kiza cha ukafiri na kutawaliwa kwa mujibu wa sera na sheria zilizochorwa kwa mikono ya wakoloni Wamagharibi na kupitishwa na mabunge au mabaraza ya vibaraka wao duniani kote kwa sura ya kupambana na Ugaidi au Magaidi, Uislamu/Waislamu wenye Siasa Kali au au Uislamu/Waislamu wenye Misimamo Mikali. Ni hasara iliyoje kutangaza vita na Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya miezi yake mitukufu kwa kwenda kinyume na ahadi yake na bishara ya mtume wake!

Hakika ni kupitia kusimama kwa Khilafah ndipo Waislamu na wasiokuwa Waislamu ulimwenguni watakapohisi kwa mara ya kwanza utulivu, maendeleo na ufanisi wa kweli baada ya takribani miaka 98H sawa na 95M tangu kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah mnamo 28 Rajab 1342H sawa na 3 Machi 1924M kwa mikono ya vibaraka wa Wamagharibi hususan kina Sharif Hussein na Mustafa Kamal, aliyekuwa myahudi kafiri.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imetoka jarida la uqab: 31 https://hizb.or.tz/2019/08/01/uqab-31/

Maoni hayajaruhusiwa.