Maneno Zaidi ya Dhahabu

Marehemu Ibrahim Ibnu Taqiyudin Nabahani aliyefariki karibuni, akiwa mtoto wa Sheikh Taqiyudin, mwasisi wa Hizb ut Tahrir (Allah awarehemu) alitembelewa na vijana wa Hizb ut Tahrir nyumbani kwake kabla ya kufariki kwake, wakamuomba : “twataka picha ya baba yako Sheikh Taqiyudin. “

Ibrahim Taqiyudin akawajibu vijana wale:
“Hakika baba yangu amewachia jambo kubwa zaidi ya picha, amewacha fikra adhimu na amewacha na chama (hizb) imara na daawah iliyoenea ulimwenguni mashariki na magharibi. Daawah ya kurejesha tena Khilafah. Na Mimi nina yaqin juu ya ahadi ya Allah (SW) ya kusimamisha Khilafah na kuwamakinisha Waislamu”

Maoni hayajaruhusiwa.