Maana ya Hadithi ya ‘Mujaddid’ Kila Karne

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Baraakallahu Bika Sheikh wetu na Mwenyezi Mungu auharakisha ushindi mikononi mwako na Mwenyezi Mungu atufaidie kwa ujuzi wako.

Kutoka kati ya Saheeh Ahaadeeth inayojulikana ambayo ilikuwa inayohusiana na Sahaabah Mheshimiwa Abu Hurairah (ra) kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwamba alisema:

إِنَّ اللَّهَ يَبْعَثُ لِهَذِهِ الْأُمَّةِ عَلَى رَأْسِ كُلِّ مِائَةِ سَنَةٍ مَنْ يُجَدِّدُ لَهَا دِينَهَا

Hakika Mwenyezi Mungu hutuma juu ya Ummah huu katika kichwa cha kila miaka mia moja mtu atakaye boresha upya Dini kwa ajili yake.

[Imepokewa na Abu Daawood (4291) na kuthibitishwa kama Saheeh na As-Sakhaawiy katika ‘Al-Maqqsid Al-Hasanah’ (149) na Al-Albaaniy katika ‘As-Silsilah As-Saheehah’ (599)]

Na swali ni: Je, neno ‘Man’ (ambaye) aliyotajwa katika Hadithi linatambua kwamba Mujaddid ni mtu binafsi au kikundi? Na je, inawezekana kuwaorodhesha kutoka kwenye karne zilizopita?

Kutoka kwa Abu Mu’min Hamaad

Jibu:

Wa Alaikum as-Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu,

Ndio, Hadeeth ni Saheeh na kuna masuala matano yanayohusiana nayo:

1) Ni tarehe gani mia (miaka) huanza? Je, ni kutoka kuzaliwa kwa Mtume wa Allah (saw) au kutoka wakati wa Ba’tha (ujumbe) au kutoka wakati wa Hijrah au kutoka wakati wa kifo chake?

2) Je! Mwanzo wa kila mwaka unamaanisha mwanzoni mwa mia moja, au wakati wa mia kila moja au mwisho wa kila mia moja?

3) Je, neno ‘mtu’ (ambaye) linamaanisha mojawapo ya watu au inamaanisha kundi ambalo linaboresha upya Deen kwa Deen kwa watu?

4) Je, Kuna ripoti yoyote iliyo na kumbukumbu sahihi kuhusiana na idadi ya Mujaddidina katika karne zilizopita?

5) Je, inawezekana kujua katika karne ya kumi na nne ambayo ilimalizika mnamo tarehe 30 ya Dhul Hijjah 1399 AH mtu aliye boresha upya Deen ya watu?

Nitajaribu kwa kadri ya uwezo wangu kutaja kile ninachoamini kuwa mtazamo wenye nguvu (Raajih) kuhusiana na masuala haya bila kuchimba na kutumbukia ndani ya nukta za Ikhtilaaf (tofauti).

Kwa hiyo nasema na kwa Mwenyezi Mungu ni Tawfeeq na Yeye Subhaanahu ni Al-Haadi (Mwenye kuongoza) katika njia iliyo nyoka:

1) Ni tarehe gani miaka mia huanza?

Al-Munaawiy alisema katika utangulizi wa ‘Fath ul-Qadeer’: [Na wametofautiana kuhusiana na kuanza kwa mwaka, huchukuliwa kutoka kuzaliwa kwa Mtume, Ba’tha (mwanzo wa ujumbe), Hijrah au kifo chake (saw) …?

Na rai yenye nguvu (Raajih) kwa maoni yangu ni kwamba inachukuliwa kutoka wakati wa Hijrah. Hii ni kwa sababu ni zama ambapo Waislamu na Uislamu walipewa heshima na nguvu (‘Izzah) na kusimamishwa serikali yake. Na kwa sababu hii, pindi Umar (ra) alipo wakusanya Maswahaaba kukubaliana kuhusu kuanza kwa kalenda walitegemea (tukio la) Hijrah. At-Tabari katika ‘Taareekh’ yake asema: “Abdur Rahman ibn Abdullah Bin Abdul Hakam aliniambia: Alisema: Nu’aim Bin Hammaad alituambia: Alisema: Ad-Daraawardiy alituambia kutoka Uthmaan Bin Ubaidullah Bin Abi Raafi” ambaye alisema: Nimesikia Sa’eed Bin Al-Musayyib akisema: Umar bin Al-Khattaab aliwakusanya watu akawauliza: “Tuanze kunakili kuanzia siku gani?” Ali akasema: “Kuanzia siku ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu sallahu alaihi wassallam alifanya Hijrah kutoka kati ardhi ya ushirikina. Hivyo ndivyo Umar (ra) alivyofanya. Na Abu Ja’far akasema: “Mwaka wa kwanza wa Hijrah unachukuliwa kutoka Muharram wa mwezi huo, yaani kabla ya Mtume wa Allah (saw) kuwasili Al-Madina kwa miezi miwili na siku kadhaa kwani kuwasili kwa Mtume wa Allah (saw) kulikuwa tarehe 12 ya Rabee ul-Awwal].

Kutokana na hili uwezekano mkubwa ni kuanza hisabu ya miaka mia kuanzia tarehe ya Hijrah (uhamiaji) ambayo kwayo Maswahabah (ra) waliitabanni.

2) Ama kuhusu kuanza kwa karne rai yenye nguvu (Raajih) ni mwishoni mwake, yaani, mboreshaji (Mujaddid) mwanachuoni (Aalim) maarufu mcha Mungu atakuwepo mwishoni mwa miaka mia moja na kifo chake kitakuweko mwishino mwake na wala si nusu yake au kwa muda wote. Ama kuhusiana na rai niliyo chukua yenye nguvu zaidi ni kwa sababu zifuatazo:

  1. a) Imethibitishwa kwa kupitia riwaya Saheeh ambazo Umar Ibn Abdul Aziz alikuja mwanzoni (Ra’s) mwa miaka mia moja ya kwanza na kufariki mwaka wa 101 Hijri akiwa na umri wa miaka arubaini huku Ash-Shaafi’i akija mwanzoni (Ra’s) mwa karne ya pili na kufa mwaka wa 204 Hijri akiwa na umri wa miaka hamsini na nne.

Kwa hiyo, ikiwa tunachukua tafsiri nyingine ya mwanzo (Ra’s) wa kila miaka mia moja kwa kufafanua kuwa ni mwanzo wa miaka mia moja ya kwanza basi Umar Ibn Abdul Azeez hatakuwa mboreshaji upya (Mujaddid) wa karne ya kwanza kwa sababu alizaliwa katika mwaka wa 61 Hijri. Na Ash-Shaafi’i hatakuwa Mujaddid wa karne ya pili kwa sababu alizaliwa mwaka wa 150 Hijri.

Hii inamaanisha kwamba mwanzo (Ra’s) wa mwaka uliotajwa ndani ya Hadeeth inahusu sehemu ya mwisho ya karne na si mwanzo wake. Kwa hiyo yeye (Mujaddid) anaweza kuzaliwa ndani yake (yaani miaka ya kati) na kisha akawa mwanachuoni Mujaddid maarufu katika sehemu yake ya mwisho na akafa mwisho wake.

  1. b) Kwa ushahidi unaoonyesha kwamba Umar ibn Abdul Azeez alikuwa Mujaddid wa karne ya kwanza na Ash-Shaafi alikuwa Mujaddid wa karne ya pili, ambaye alijulikana miongoni mwa Ulamaa wa Ummah huu na Imaam wake. Az-Zuhriy na Ahmad bin Hanbal miongoni mwa maimamu wengine wa kale na baada yao walikubaliana kuwa katika Mujaddideen wa mwanzo (Ra’s) wa karne ya kwanza alikuwa Umar ibn Abdul Azeez (rh) na wa mwanzo (Ra’s) wa karne ya pili alikuwa Imam Ash- Shaafi’iy (rh). Umar Ibn Abdul Azeez alifariki mwaka wa 101 Hijri akiwa na umri wa miaka arubaini na muda wa Khilafah yake ulikuwa miaka miwili na nusu huku Ash-Shaafii akifariki mwaka wa 204 Hijri akiwa na umri wa miaka 54. Na Al- Haafizh Ibn Hajar alisema katika ‘Tawaaliy At-Ta’sees’: [Abu Bakr Al-Bazzaar akasema: “Nimemsikia Abdul Maalik Bin Abdul Hameed Al-Maymooniy akisema: Nilikuwa pamoja na Ahmad Bin Hanbal wakati Ash-Shaafii alipo tajwa basi nikamuona Ahmad akiinua kichwa chake na kunasibisha kutoka kwa Mtume (saw) kwamba Allah (SWT) anachagua mtu mwanzoni (Ra’s) mwa kila karne mtu ambaye angewafundisha Deen yao. Akasema: Umar Ibn Abdul Azeez alikuwa mwishoni mwa karne ya kwanza na natumaini kwamba Ash-Shaafii ndiye aliye kuwa mwishoni mwa ya pili].

Na kwa njia ya Abu Sa’eed Al-Firbaabiy alisema: Ahmad Bin Hanbal alisema: Hakika Mwenyezi Mungu huwachagulia watu katika karne mtu atakayewafundisha watu Sunan na akapinga kumzulia Mtume uongo, kwa hivyo tumepima tukagundua kwamba Umar ibn Abdul Azeez ndiye aliye kuwa katika kichwa (Ra’s) cha karne ya kwanza huku Ash-Shaafi’i akiwa mwishoni mwa kichwa (Ra’s) cha karne ya pili.

Ibn Addiy alisema: Nilimsikia Muhammad bin Ali Bin Al-Husein akisema: Niliwasikia wenzetu wakisema: Katika karne ya kwanza alikuwa ni Umar ibn Abdul Aziz na katika ya pili alikuwa Muhammad Bin Idrees Ash-Shaafi’i.

Na Al-Haakim aliandika katika ‘Mustadrak’ yake kutoka Abu ul-Waleed ambaye alisema: [Nilikuwa katika mkusanyiko pamoja na Abu-l-Abbaas Bin Shuraih wakati Sheikh alipo kuja kwake na kumsifu. Kisha nikamsikia akisema: Abu At-Tahir Al-Khawlaani alituambia na pili Abdullah Bin Wahb: Sa’eed Ibn Abi Ayyoob aliniambia kutoka Shuraaheel Bin Yazeed kutoka Abu ‘Alqamah kutoka Abu Hurairah (ra) kwamba Mtume wa Allah (saw) amesema:

إِنَّ اللَّهَ يَبْعَثُ ِلهَذِهِ الْأُمَّةِ عَلَى رَأْسِ كُلِّ مِائَةِ سَنَةٍ مَنْ يُجَدِّدُ لَهَا دِينَهَا

Hakika Mwenyezi Mungu hutuma juu ya Ummah huu katika kichwa cha kila miaka mia moja mtu atakaye boresha upya Dini kwa ajili yake.

Kwa hivyo pokea bishara njema O Kadhi hakika Allah alimtuma mwishoni mwa karne ya kwanza Umar ibn Abdul Azeez na mwishoni mwa karne ya pili Muhammad ibn Idrees Ash-Shaafi’i …].

Al-Haafizh Ibn Hajar amesema kuwa hii yadhihirisha kwamba Hadeeth hii ilijulikana sana (Mash’hoor) wakati huo.

  1. c) Inaweza kusemwa kuwa mwanzo (Ra’s) wa kitu kilugha yamaanisha sehemu ya mwanzo au ya kuanzia fulani ina maana ya kwanza au sehemu ya mwanzo, sasa vipi basi tunaweza kuona kama rai yenye nguvu kuwa Ra’s katika kila mwaka ni mwisho wake na si mwazo wake mwanzo? Jibu la hili ni kwamba kama vile ra Ra’s ina maana ya kuanza kwa kitu lugha (katika lugha ya Kiarabu) pia inamaanisha sehemu yake ya mwisho. Imesemwa katika ‘Taaj Al-Aroos’ (kamusi): Ra’s ya kitu ni ukingo wake na husemwa ni sehemu yake ya mwisho. Na imesemwa katika ‘Lisaan Al-Arab (kamusi): Mjusi alitoka shimoni kwa Ra’s yake (Muraa’san) ambayo ina maana kwamba kichwa kilitokea kwanza au labda mkia kwanza yaani sehemu ya kwanza ya sehemu ya mwisho. Kwa hivyo Ra’s ya jambo au kitu inaweza kulingana na lugha yaweza kumaanisha mwanzo kama vile pia yaweza kumaanisha ya ukingo wake ima hii imaanishe mwanzo au mwisho. Kwa hivyo tunahitaji Qareenah (kidokezo / dalili) ambayo itatilia uzito maana ambayo inalengwa katika Hadeeth ‘Ra’s ya miaka mia’. Je, ni mwanzo wake au mwisho wake? Na Qareenah hii iko katika riwaya zilizotangulia zinazo mkadiria Umar ibn Abdul Azeez Mujaddid wa karne ya kwanza na alifariki mwaka 101 Hijri na kumkadiria Ash-Shaafi’I kuwa Mujaddid wa pili na alifariki mwaka wa 204 Hijri. Yote haya yanatilia uzito maana ya Hadeeth kumaanisha sehemu mwisho ya karne na si sehemu yake ya mwanzo.

Kwa hiyo, kwa kuzingatia mambo ambayo yameelezwa hapo juu, ninazidi kupata nguvu kuwa uwezekano mkubwa wa maana ya: ‘Ra’s ya miaka mia moja’ kama ilivyo patikana katika hadith, ni sehemu ya mwisho ya kila karne.

3) Kwa maana neno ‘Mtu’ (ambaye) linamaanisha mtu au kikundi: Kisha Hadeeth anasema hivi:

يبعث لهذه الأمةمن يجدد لها دينها

“Hakika Mwenyezi Mungu hutuma juu ya Ummah huu ….mtu atakaye boresha upya (Man Yujaddidu) Dini kwa ajili yake.” na kama ‘Man’ (ambaye) inaashiria kikundi basi kitenzi hicho kingekuwa katika muundo wa wingi (yujaddidoona). Lakini kitenzi kimetajwa katika muundo wa umoja na hii ni licha ya kuwa neno ‘Man’ (ambaye) pia ina beba maana ya wingi hata kama kitenzi baada yake kina muundo wa umoja. Lakini mimi naona kama rai yenye nguvu zaidi kwamba hapa linaashiria mtu binafsi kwa sababu ya Qareenah ‘yujaddidu’ (yaani, umoja wa kitenzi). Na nasema rai yenye nguvu kwa sababu neno hili hapa kamwe halimaanishi mtu binafsi hata kama kitenzi baada yake kiko katika muundo wa umoja. Kutokana na haya kuna baadhi ambao wametafsiri neno “Man” kama kikundi na wameliorodhesha katika riwaya vikundi vya wanazuoni waliokuja katika kila karne. Hata hivyo maoni haya yamezidiwa nguvu na yale  mengine yaliyotangilia kutajwa.

Kwa kumalizia, maoni yenye nguvu ni kwamba ‘Man’ (ambaye) inaashiria mtu binafsi na kwamba Mujaddid aliyetajwa katika Hadeeth ni mtu binafsi mwenye uchaji Mungu na mwanachuoni asiye mchafu.

4) Ama kuhusu orodha ya majina ya Mujaddideen katika karne zilizopita; ripoti zimeonyesha, kuwa orodha iliyojulikana zaidi ni kwa njia ya mashairi ya As-Suyooti hadi karne ya tisa na akamuomba Allah (swt) kuwa Mujaddid wa karne ya tisa. Sasa nitarejelea sehemu kutoka kwa beti zake:

Hivyo basi katika karne ya kwanza ilikuwa Umar Khaleefah muadilifu kama alivyo afikiwa na kubaliwa.

Na Ash-Shaafi’i alikuwa wa pili kutokana na elimu yake mkubwa.

Na wa tano alikuwa Al-Ghazaali kwa hoja alizomiliki.

Na wa saba aliyeinuliwa kwa daraja alikuwa Ibn Daqeeq Al-Eid kama ilivyokubaliwa.

Na huyu ni wa tisa iliyekuja na yule anayeongoza mwenye kuongoza havunji ahadi na mimi nimetaraji kuwa Mujaddid wake kwa sababu fadhila za Mwenyezi Mungu haziishi.

Na kuna maelezo mengine yanayoendelea.

5) Na je, inawezekana kwetu kujua ni nani mboreshaji upya (Mujaddid) wa Deen kwa watu kwa karne ya 14 iliyo malizika tarehe 30 ya Dhul Hijjah 1399?

Ulinijia utambuzi wa ni nani aliye kuwa maarufu au aliye julikana zaidi miongoni mwa wanazuoni waheshimika pindi walipo ashiria kuwa Ra’s ya mwaka ilikuwa sehemu yake ya mwisho. Umar Ibn Abdul Azeez alizaliwa katika mwaka wa 61 Hijri na alikufa katika Ra’s ya karne ya kwanza katika mwaka wa 101 Hijri na Ash-Shaafi’iy alizaliwa katika mwaka wa 150 Hijri na kufa katika Ra’s ya karne katika mwaka wa 204 Hijri.

Hii ina maana kwamba kila mmoja wao alizaliwa katikati ya karne na akajulikana zaidi katika sehemu yake ya mwisho. Na kama nilivyo sema tafsiri ninayoiona kuwa yenye nguvu nikiona na ambayo inajulikana zaidi na wanazuoni waheshimika kuhusiana na Umar ibn Abdul Azeez kuwa Mujaddid wa karne ya kwanza na Ash-Shaafii kuwa Mujaddid wa karne ya pili. Kutokana na msingi huu basi, ninaona kama rai yenye nguvu zaidi kwamba mwanachuoni mkuu Taqiudeen An-Nabahani (rh) alikuwa Mujaddid wa karne ya kumi na nne. Alizaliwa mwaka wa 1332 Hijri na akajulikana sana katika sehemu ya mwisho ya karne ya kumi na nne na hasa wakati alipoanzisha Hizb ut Tahrir katika Jumada al-Thani mwaka wa 1372 Hijri na alifariki mwaka wa 1398 Hijri. Dawah yake kwa Waislamu ilihusiana na suala la nyeti, kuregesha maisha kamili ya Kiislam kupitia kusimamisha kwa serikali ya Khilafah Rashida na ilikuwa na athari kubwa juu ya maisha yao na bidii na jitihada mpaka Khilafah imekuwa matakwa jumla wa Waislamu leo.

Kwa hivyo rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Abu Ibrahim na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya ndugu yake Abu Yousuf aliyekuja baada yake na Mwenyezi Mungu atawakusanya pamoja na manabii, Wakweli, Mashahidi na Wema na hao ndio marafiki wema.

Hayo ndio ninayoyaiona kama rai yenye nguvu ndugu yangu Abu Mu’min na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi yaliyo sahihi na kwake Yeye ndio maregeleo bora zaidi.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

14 Shaban 1434 H / 23 Juni 2013 M

Inatoka: http://hizb.or.ke/sw/2017/10/04/627/

Maoni hayajaruhusiwa.