Kusimamisha ukoloni wa kichina pembeni ya ukoloni wa kimagharibi haitakua suluhisho

Mnamo tarehe 12 mwezi wa 11 2018, iliripotiwa kwamba ” mkataba wa makubaliaono [  Memorandum  of Understanding  (MOU) ] ulisainiwa na Mr. Khan kupitia safari yake iliyolenga kuweka misingi ya kuvutia uwekezaji wa china sambamba na msaada wa kitaalamu katika jumla ya sekta za kilimo .”  mbali na kufanya mazungumzo na IMF, Pakistan inailenga zaida China kwa ajili msaada wa kifedha kwa baadae. Tayari China imeshakua mkopeshaji mkubwa wa Pakistan . Pakistan imeazimwa zaidi ya dola  $20  billion,  ambayo ni sawa  20%  ya jumla ya pesa zake, kutoka China.  Ongezeko la madeni linakuja katika muda ambao taifa lipo katika hali mbaya, kama inavyoshuhudiwa kwa kupitia kushuka thamani kwa pesa muda huu,  deni la serikali, na madeni ya nje. Utawala wa  Bajwa-Imran unaelekea upande wa magharibi na haswa haswa katika shirika la fedha la ulimwengu kwa ajili  ya kukopa mkopo wa pili na kulipa mkopo wa mwanzo_na mara zote hizo jicho likiwa limeelekea kwenye mikopo ya  Beijing, hivyo basi Pakistan inajiwekea mazingira mazuri ya kuwa chakula cha mabeberu pamoja na kuwa koloni la china la baadae.

kinachoendelea hivi sasa juu ya uingiaji wa China katika nchi zinazoendelea ni kwamba haulengi kusaidia uchumi wa chini au mdogo mdogo. Pia kuna mahitaji yanayohitajiwa na China katika uingiliaji huo. hayo ni pamoja na mgao mkubwa wa faida katika kile kinachoendelea na kujulikana kama  mpango wa CPEC, ambao hulenga kuamua mustakbali wa mkopeshwaji,  pia kupata soko la miradi na makampuni ya kichina.  Sri Lanka kuna bandari inaitwa Hambantota ipo katika tatizo hilo hivi sasa, ambapo China imechukua na kuweka  mkataba wa miaka 99 baada ya nchi kushindwa kulipa deni la mkopo. Waziri mkuu wa Malasia aliechaguliwa Mahathir amesitisha  $22  billion zilizokuwa tayari kwa ajili ya miradi ya kichina , huku akihoji usawa wa kiuchumi na ukubwa wa deni , akipinga kile kinachoitwa ‘ toleo jipya la  kikoloni ‘ mifano hii inaonyesha kwamba masharti ya mikopo kutoka China hulenga zaidi kupora nguvu za dola kujiamulia mambo yake

Kana kwamba uchumi wa China hautoshi, mipango ya IMF imekua ikiwekwa kwa ajili ya ya kutatua mgogoro wa malipo. Hili pia litafungua mistari ya kifedha kutoka Benk ya dunia na Benk ya maendeleo ya Asia, ambazo ni ndugu katika taasisi za kibeberu. Mipango hiyo itaonekana vizuri kwa wakopeshaji, ambao wanatafsiri jambo hili kama fursa ya kuongeza madeni kupitia mikopo. Zaidi ya hayo, Mipango ya IMF haiwezi kufanikiwa bila urasimishaji wa kipesa kupitia na utungaji sera za kipesa , pia itahitajia kupandisha kodi, viwango vya tozo na  riba. Ambapo itapelekea ukuaji na udororaji mkubwa wa uchumi kama ilivyotokea mwanzo. Hivyo, tatizo lilianzia katika usawa wa malipo kwa hilo sasa ndio kupelekea upungufu kuwa ni mgogoro wa kuendelea kuongeza madeni. Kwakuwa uchumi haujiwezi, mikopo imeendelea kuwa ni kivutio cha wawekezaji wa kigeni  na kuja na riba kubwa inayohakikisha nchi kuendelea kubaki katika madeni .Hili kupelekea mikopo ya mataifa kudharau uchumi na uhuru wa kisiasa katika nchi.  Allah  (swt)  anasema;

 “O  enyi mlio amini, mcheni Allah na muache kile kinachobakia katika riba, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya hivyo basi fahamuni mtakua na vita na Allah na Mtume wake .Na mkiwa mmetubu basi mtapata”

Kuondoa tatizo hilo ,  inahitajika urejeshwaji wa khilafah kupitia njia ya Utume. Kupitia utabikishaji wa uislamu , utahakikisha uwekaji wa mipango na sera  imara za  kiuchumi katika kilimo, biashara, na viwanda . Na zaidi, uislamu unafaradhisha hazina kuweka mipango imara ya kiuchumi.

#UislamuNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.