Kukosekana kwa ujenzi wa Kimfumo ndiyo chanzo cha Migogoro na Mabadiliko yasiyokwisha ndani ya vyama vya Siasa

2

Mnamo  tarehe  12/03/2017  chama  cha  mapinduzi (CCM) nchini, kilipitisha mabadiliko ya  16 ya  katiba, kanuni za  uchaguzi, na  jumuiya  zake huku  ikiwafukuza  wanachama  12 na  kuwaonya  wengine  12 siku moja kabla yaani 11/03/2017,

Tukio  hili  lilivuta  hisia  za  wengi ndani  na  nje  ya  Tanzania, hivyo  kuliweka  wazi  ni  jambo  muhimu.

  1. Sababu za  mabadiliko  na  mkutano 

Tukiliangazia  tukio  hili  kwa  hakika  tunaona  nukta zifuatazo kuwa  miongoni  mwa  sababu  za  mabadiliko  haya  kutokana  na  ushahidi  wa  kukatikiwa.

  1. Kumaliza mabaki  ya  kambi ndani  ya  Katika  kuelekea uchaguzi  mkuu  mwaka  2015 na hata baada ya uchaguzi huo, CCM ilijikuta imegawanyika  katika  kambi mbili kubwa zilizojiegemeza kwa Edward Lowasa na Benard  Membe ikimjumuisha pia Rais mstaafu Kikwete. Kambi ya Membe ndio iliyopata Baraka zaidi kutoka viongozi waliokuwa madarakani na  kama  si  wafuasi  wa  lowasa  walioamua kumkwamisha basi safari yake kuelekea ikulu ilikuwa nyepesi zaidi. Mbali na kumkwamisha Membe kambi ya Lowasa ilisababisha mpasuko zaidi ndani ya CCM kufuatia uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA.
  • Viongozi mbalimbali  wa  CCM,  walianza  kuwatuhumu  wafuasi  wa  lowasa  ndani ya  CCM  kama  “mamluki” au  mapandikizi, nk  huku  wakiashiria  ulazima  wa  kuwaondoa ndani ya chama.  Katika  maadhimisho  ya  miaka  39 ya  CCM mjini  Singida  februari  2016  Kikwete aliweka wazi kuwa! “Tuwaondoe  viongozi  wenye  sifa mbaya……ambao wakishindwa  uchaguzi  wanahama   chama” (Tanzania kwanza, 06/02/2016) na  akaashiria  hayo  Magufuli  katika  hotuba  yake 12/03/2017 pale  aliposema: “mtakumbuka  kikao  kilichopita  wakati  wajumbe  waliposimama  na  kuimba  wana  imani  na  mtu gani  sijui (Lowasa) (mwananchi 13/03/2017).
  • Tunaona mara  tu  baada  ya  fukuza fukuza ya hivi karibuni  ndani  ya  CCM, Lowasa  aliwataja  waliofukuzwa kuwa  ni  “ hawa  walikuwa  mashujaa wa kutetea  haki” (mwananchi 13/03/2017).
  • Wengi miongoni  mwa  viongozi  na  wanachama  waliofukuzwa  au  kulengwa  kufukuzwa  na  kupewa  maonyo  ni  wale  waliokuwa  kambi  ya Lowasa  mwaka  2015, kama  Sofia Simba, Nchimbi,Vuai, n.k.
  • Kuna uhusianao  kati  ya  mabadiliko  hayo na  uchaguzi  wa  mwaka  2015 ambao  Lowasa  aliihama  Pamesemwa  wazi  kwamba mabadiliko haya yametokana  na  “taarifa  ya  tathimini ya  uchaguzi  mkuu  uliopita “(Mwananchi 13/03/2017).

Hivyo, licha ya mabadiliko kuwalenga watu wa Lowasa ni wazi kuwa Magufuli atatumia kuwaondoa na kuwadhoofisha wafuasi wa kambi nyengine ili kuondoa upinzani ndani ya chama.

2 . Kukidhibiti chama. Mabadili haya yanaashiria kulenga kubakisha  maamuzi  ya  chama  kwa  watu  wachache zaidi  na  kuondoa  upinzani katika kufikia  maamuzi.  “ wajumbe  wa  kamati  kuu  kupunguzwa  kutoka  34 hadi 24 na  wale  wa  halmashauri  kuu  nao wakipunguzwa  kutoka  388 hadi 158” ( ITV tanzania  12/03/2017). Hii  inamaanisha  maamuzi  yatakuwa  sasa  yakifanywa  na  watu wachache  zaidi wanaodhibitika.

  1. Muunganiko wa sababu hizo mbili ndiyo unaofanya sababu ya tatu ambayo ni kile kilichoitwa “kuimarisha chama”
  1. Tunayojifunza kutokana na Mkutano na Mabadiliko  hayo:

Mkutano  na  mabadiliko  hayo  ya CCM  yanatupa  ufahamu  ufuatao kuhusu CCM na vyama vya siasa vya  kibepari  na  kidemokrasia  kwa  ujumla.

  1. Migogoro ya  kimaslahi  ni  jambo  la  kutarajiwa  katika  vyama hivi.
  • Inaonyesha kuna mgogoro  wa  ndani  katika  CCM ambao  ndio  uliopelekea kufukuzwa  wanachama  na  kufanyika kwa mabadiliko haya, mgogoro  ambao  bila  shaka  asili  yake  ni  maslahi  binafsi  ya  mtu  au  kikundi cha watu
  • Hatua hizi zilizochukuliwa na CCM ni zaidi ya kuimarisha chama bali ni dhihirisho la migogoro ya kudumu ya kimaslahi iliyomo ndani ya vyama vya kidemokrasia. Ndani ya kipia migogoro kadhaa ndani ya CCM na vyema vyengine vya upinzani ikiwemo: Mgogoro  ndani  ya  CUF ulioanza  2015 kati  ya  Seif  na  Lipumba, mgogoro  wa  2015 ndani  ya  CHADEMA  kati  ya  Mbowe  na  Slaa  na  ule  wa  2013 kati  ya  Mbowe  na  Zito, mgogoro  wa  TLP  2009  kati  ya  Mrema  na  Benedict Ntungirei, mgogoro  katika  NCCR 1998 kati  ya  Mrema  na  Mabele Marando, n.k . Yote hiyo ni migogoro ya kimaslahi ikiwa na lengo la kumnufaisha mtu fulani au kikundi cha watu fulani.
  1. Mabadiliko haya  yanaashiria  kushindwa, kuchokwa  kwa  CCM  na  demokrasia  kiujumla: Kwa  kushindwa  kwake  kutatua  matatizo  ya  wananchi  kama  njaa, bei  juu  za  vyakula, na  umaskini  kiujumla  “ akasema  Magufuli  kuwa  mabadiliko  haya  yanalenga  “kukipeleka  chama  kwa  wananchi “( Mtanzania  13/03/2017). Hii  inamaanisha  hakipo  kwa  wananchi, yaani wananchi  wamekata  tamaa nacho, na  hali  ya  CCM  ndiyo  hali  ya  vyama  vyote  vya  kibepari
  1. Kukithiri kwa ufisadi ndani ya chama. Tukio hii na mfano yanayoendelea kujikariri ndani ya vyama vya siasa hapa chini na kwengineko duniani linadhihirisha jinsi vitendo vya ufisadi vilivyokithiri ndani ya vyama vya kidemokrasia na hivyo  kusababisha  hujuma na migogoro. Amekiri hili Rais Magufuli pale aliposema” kuna wanaosema wanapangisha kwa sh50,000 kumbe wanapangisha kwa sh milioni moja”(Mtanzania 13/03/2017). Hii ni kwa sababu msingi wa vyama hivi ni maslahi binafsi.
  1. Matajiri kukihodhi chama. Mabadiliko hayo  yanatupa  taswira  ya  wazi  kuwa  vyama  hivi  huendeshwa  na  matajiri   wachache  amabo  hutumia  wanasiasa  kufikia  malengo  Na  hapa  tunaona  kuna  mgogoro wa  wazi  kati  ya  CCM  na  baadhi  ya  matajiri  wake. Akagusia  hili  raisi  alivyosema  kuhusu  CCM  “kupokea fedha  kutoka  kwa  watu  wasiostahili” (Mtanzania 13/03/2017). Hali  hii  si kwa  nchi  changa  pekee kwani  hata  Amerika  ambaye  ni  kiranja  wa  demokrasia, bado vyama  vyake  hutegemea  matajiri. Obama  katika  kampeni  zake  za  uraisi  alichangiwa  dolari  za  Amerika  1,006,159 kutoka  Citi Group, 1,123,759 kutoka  Time  Warner, 1,295,955 kutoka  Goldman  Sachs, 1,628,122 kutoka Google na Microsoft corp 1,680,787 (opensecrets.org 01/02/2017 )
  1. kuwahamisha watu  kutoka  katika  mjadala wa  Vyeti  vya  Mkutano kibinafsi umemsaidia Makonda katika kashfa zinazomkabili. Kufuatia  vita  iliyoshindwa  ya  dawa  za  kulevya iliyoanzishwa  na  Makonda 02/02/2017 jijini  Dar es  salaam, kulipelekea  kuibuka  kwa  taarifa  tatanishi kuhusu  Paul  Makonda. Ikiwemo  mali  anazomiliki  na  hili  la  sasa  la  kutumia  vyeti  bandia. Akasema  Gwajima! “kosa  la  kwanza  la  Makonda  ni  kughushi cheti  ambacho  kinaonesha  yeye  ni  Paul Makonda  wakati  akifahamu  kuwa  yeye  ni  Daudi  Bashite  “ (Mwananchi 12/03/2017).

Licha  ya  kupata  fursa  nyingi  na  waandishi  wa  habari Makonda  hajakanusha  hadharani  tuhuma  hizi  hali inayopelekea  kuleta  mashaka  na  taharuki  miongoni mwa  wananchi  kwa  namna  anavyofahamika  juu  ya  wepesi wake  wa  kujibu  tuhuma.

Amma  vyombo  ambavyo  vimekuwa  mstari  wa  mbele  kukamata  watu  kwa  tuhuma  kama polisi  na  baraza  la  mtihani  kukaa  kimya  juu  ya  hili  kunaleta  taswira  hasi  juu  ya  tuhuma  hizi, kuwa  huenda  zina  ukweli.

Tuhuma  hizi  zimeambatana  na  matukio  kama  uteuzi  wa  Salma  Kikwete  01/03/2017 na  kuachiwa  huru  Lema  03/03/2017 na  katika  muda  huo huo  mfupi  yanakuja  mabadiliko  haya  12/03/2017 inaleta  picha  kuwa  matukio  haya  yanahusiana.

  1. C. Hitimisho:
  2. kwa kifupi tunasema  mambo  yaliyotokea  CCM, ni  ya  kutarajiwa  katika  vyama  vya  kidemokrasia  duniani  kote  kwani  msingi  wa  vyama  hivi  ni  maslahi  ya  kibinafsi  na  pindi  yanapokiukwa  na  upande  mmoja  basi  hutokea  mgogoro  na  mabadiliko  katika  vyama  hivi  kama  tulivyoeleza.

2 . Tofauti ya vyama vya kidemokrasia vya Afrika na Ulaya ni kuwa vyama vya Ulaya vina udhibiti  na uelewa bora mfumo vinavyosimama juu yake, lakini hivi vya Afrika ni vitupu kwa upande wa mfumo bali kila mtu anaeiingia madarakani huwa yeye ndiye mfumo wenyewe. Hii itaendelea kusababisha migogoro mingi kila uchao.

3  Amma mfumo  wa  uislamu, ni tofauti kabisa  na  mifumo hii ya kikafiri (ubepari  na  ujamaa)  ambapo  huruhusu vyama  vya  siasa  vya kiislamu vyenye  itikadi (aqeeda /creed) ya  uislamu kulingania   uislamu ili  utawale  lakini humsaidia  mtawala  (khalifah) kwa  kumkosoa  na  kumpa  ushauri katika uendeshaji wanchi wa mujibu wa mafundisho ya Uislam na  huwa  jambo  hili  ni  mbali  na  maslahi  ya  mtu  binafsi.  Kwa msingi huu ndiyo imebuniwa Hizb ut tahrir kulingania Uislamu kwa lengo la kurejeshwa serikali ya Kiislamu.

Saidi Bitomwa

2 Comments
  1. Diabetic neuropathy socks says

    I think the admin of this website is genuinely working hard in support of his web site, since here every data is quality based material.

  2. Darris says

    I used to be able to find good info from your blog articles.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.