Kila Mmoja ni Lazima Abebe Ulinganizi kwa Kadri ya Uwezo Wake

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, Amiri wetu. Nataka kuuliza kuhusu dori yangu katika kufanya kazi ya kusimamisha Dola, je, wakati ikiwa sina uwezo wa kufanya hivyo?

Nasubiri jibu lako.

Nataka muongozo kutoka kwako, kwani nimechanganyikiwa, sijielewi mimi ni nani, nakuomba kwa jina la Mwenyezi Mungu nifanye nini?

Jibu:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ndugu yangu, Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi isipokuwa kwa [lile lililomo ndani ya] uwezo wake. Watu hutofautiana katika uwezo wao na katika umahiri wao wa vitendo vya Dawah na ujuzi wao mzuri katika kufikisha ulinganizi. Vilevile hutofautiana katika mafanikio yao ya kielimu na kifikra na hekima katika kuwasilisha kadhia, pia hutofautiana katika elimu yao ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw) … Hivi ndivyo vitu ambavyo vipo miongoni mwa wanadamu, na kukalifishwa (takleef) katika kitendo kunategemea uwezo, hili liko wazi katika aya tukufu za Qur’an na Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

 (لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا) “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo” [Al-Baqara: 286]. Allah (swt) says:  (لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا) “Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa” [At-Talaq: 7]

Mtume (saw) amesema: «لَا تَحْقِرَنَّ مِنْ الْمَعْرُوفِ شَيْئًا وَلَوْ أَنْ تَلْقَى أَخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْق» “Msidharau jema lolote hata kama ni kukutana na ndugu yako kwa uso wa bashasha.” (Muslim). Mtume (saw) amesema: «بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً» “Fikisheni kutoka kwangu hata kama ni aya (ya Qur’an)” (Bukhari).

Kutoka kwa Zaid Ibn Thabit: kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema:

«نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا حَدِيثًا فَحَفِظَهُ فَبَلَّغَهُ، فَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ لَيْسَ بِفَقِيهٍ» “Mwenyezi Mungu amtie nuru mtu ambaye amesikia kutoka kwetu Hadith, akaihifadhi kisha akaifikisha kwa wengine. Na huenda mbebaji wa Fiqh akawa si Fafihi.” (Imepokewa katika in Al-Kabeer na At-Tabarani)

Hivyo ndugu yangu, waweza kuamrisha mema na kukataza maovu kwa kadri ya uwezo wako, na waweza kufikisha aya moja au aya mbili. Sio sharti kwamba ni mpaka uwe miongoni mwa waliohifadhi Qur’an Tukufu na Sunnah Tukufu, ndio uweze kuamrisha mema na kukataza maovu, bali unapaswa kufanya hili kwa kadri ya uwezo wako, na kutafuta msaada kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kumtegemea Yeye, na Mwenyezi Mungu (swt) huangalia uchaMungu.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

24 Ramadhan 1441 H 17/5/2020 M

 

Maoni hayajaruhusiwa.