Kauli (Aswalatu Khayrum- minannaum) kuwa ni Sunna

بسم الله الرحمن الرحيم

 Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh,

Natanguliza maamkizi mema; ama baada ya hayo, nina swali na ninatamani jawabu la moja kwa moja.

Je kauli (Aswalatu khayrum minannaum – swala bora kuliko usingizi) katika adhana ya alfajiri ni bida’a?

Jibu:

Waalaykum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,

Swali lako ni tangazo la kujirejea, nalo: (Kuzidisha muadhini ibara ya “Aswalatu Khayrum minannaum” mara mbili baada ya Hayya ‘alaa mbili katika adhana ya alfajiri), nayo si bid’a bali ni Sunna. Zimepokelewa kuhusu hili hadithi kadhaa kutoka kwa Mtume (SAAW):

– أخرج أبو داود في سننه عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبِي مَحْذُورَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ عَلِّمْنِي سُنَّةَ الْأَذَانِ؟ قَالَ: فَمَسَحَ مُقَدَّمَ رَأْسِي، وَقَالَ: «تَقُولُ: اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ، تَرْفَعُ بِهَا صَوْتَكَ، ثُمَّ تَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، تَخْفِضُ بِهَا صَوْتَكَ، ثُمَّ تَرْفَعُ صَوْتَكَ بِالشَّهَادَةِ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، فَإِنْ كَانَ صَلَاةُ الصُّبْحِ قُلْتَ: الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ، الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ، اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ»، قال الألباني هذا الحديث صحيح. وأخرج نحوه ابن خزيمة في صحيحه، ولكن عن طريق ابْنِ جُرَيْجٍ قال: أَخْبَرَنِي عُثْمَانُ بْنُ السَّائِبِ، عَنْ أُمِّ عَبْدِ الْمَلَكِ بْنِ أَبِي مَحْذُورَةَ، عَنْ أَبِي مَحْذُورَةَ، وكذلك أخرج نحوه الدارقطني

1-Ametoa Abuu Daud katika Sunan yake kutoka kwa Muhammad bin Abdil Malik bin Abi Mahdhuura, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allah nijulishe sunna ya adhana. Akasema: Akapangusa komo langu akasema: “Utasema:

للَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ

Utanyanyua kwayo sauti yako, kisha utasema:

أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ،

Utahafifisha kwayo sauti yako, kisha utanyanyua sauti yako kwa Shahada

أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ .

Ikiwa sala ya asubuhi utasema:

الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ، الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ، اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ

Albani amesema hadithi hii ni sahihi, na ameitoa mfano wake Ibn Khuzaima katika sahihi yake lakini kwa njia ya Ibn Juraij amesema: Amenieleza Uthman bin Saaib, kutoka kwa Umm Abdil Malik bin Abi Mahdhuura kutoka kwa Abi Mahdhuura, na vilevile ameitoa mfano wake Al Daruqutni.

2-Na katika riwaya nyengine ya Abi Daud  kwa njia ya Ibn Juraij, nah ii hapa nass yake:

حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ وَعَبْدُ الرَّزَّاقِ عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ قَالَ أَخْبَرَنِي عُثْمَانُ بْنُ السَّائِبِ أَخْبَرَنِي أَبِي وَأُمُّ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبِي مَحْذُورَةَ عَنْ أَبِي مَحْذُورَةَ عَنْ النَّبِيِّ e نَحْوَ هَذَا الْخَبَرِ وَفِيهِ: «الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنْ النَّوْمِ الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنْ النَّوْمِ فِي الْأُولَى مِنْ الصُّبْحِ…» أي ليس في الإقامة وهي ما يطلق عليها الأذان الثاني. كما جاء في الحديث الصحيح الذي أخرجه البخاري قال: حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ قَالَ حَدَّثَنَا كَهْمَسُ بْنُ الْحَسَنِ عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ e «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ ثُمَّ قَالَ فِي الثَّالِثَةِ لِمَنْ شَاءَ».

Ametueleza Al Hassan bin Ally, ametueleza Abu ‘Aswim na Abdu Al Razak kutoka kwa ibn Juraij amesema amenieleza Uthman ibn Saaib amenieleza baba yangu na Umm Abdil Malik ibn Abi Mahdhuura kutoka kwa Abi Mahdhuura kutoka kwa Mtume (SAAW) mfano wa hadithi, na mna humo

الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنْ النَّوْمِ الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنْ النَّوْمِ

ya mwanzo wakati wa asubuhi…” yaani si katika iqama nayo ni ile inayoitwa adhana ya pili, kama ilivyokuja katika hadithi sahihi aliyoitoa Bukhar kasema: ‘Ametueleza Abdullah ibn Yazid amesema ametueleza Kahmas ibn Al Hassan kutoka kwa Abdillah ibn Buraida kutoka kwa Abdillah ibn Mughafal amesema: Amesema Mtume (SAAW): “Kati ya kila adhana mbili pana sala, kati ya kila adhana mbili pana sala kisha akasema mara ya tatu kwa anayetaka”

3-Na ametoa Al Nasai katika Sunna yake kasema: Ametueleza Ibrahim ibn Al Hassan amesema ametueleza Hajaj kutoka kwa ibn Juraij kutoka kwa Uthman ibn Saaib kasema amenieleza baba yangu na Umm Abdi Al Malik ibn Abi Mahdhuura kutoka kwa Abi Mahdhuura kasema: “Wakati Mtume (SAAW) alipotoka Hunain… Akaniweka kitako Mtume (SAAW) mbele yake akapangusa utosini pangu kisha akaniombea baraka mara tatu kisha akasema nenda ukaadhini katika nyumba tukufu (Baitil Haram), nikasema: vipi ewe Mjumbe wa Allah? Akanifundisha kama hivyo munavyoadhini hivi sasa.”

الله أكبر الله أكبر الله أكبر الله أكبر أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله حي على الصلاة حي على الصلاة حي على الفلاح حي على الفلاح الصلاة خير من النوم الصلاة خير من النوم )-في الأولى من الصبح…

-ya mwanzo wakati wa asubuhi…) Albani kasema: sahihi. Na kama tulivyotaja punde tu, yaani sio katika iqama, nayo ndio inayoitwa adhana ya pili.

4-Ametoa Al Baihaqi katika Al Sunanul Kubra kutoka hadithi ya ibn ‘Ajlaan kutoka kwa Nafi’i kutoka kwa ibn Umar kasema: “Ilikua adhana ya mwanzo baada ya mara mbili”. Amesema Ibn Hajar: sanad yake ni nzuri. Na kasema Al-Ya’amuri: Na isnad hii ni sahihi.

Na kama tulivyosema punde tu, maana ya adhana ya mwanzo yaani adhana ya asubuhi na sio adhana ya pili yaani iqama, kwani hapasemwi katika iqama.

5-Amepokea Ibn Khuzayma na Al Daruqutni kutoka kwa Anas kwamba amesema: Katika Sunna atakaposema muadhini katika alfajiri aseme:

الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنْ النَّوْمِ،

kasema Ibn Sayyid Al Naas Al Ya’amuri: Nayo ni isnaad sahihi.

6-Na ametoa Ibn Hibban katika sahihi yake: Ametueleza Alfadh-lu ibn Alhabaab Aljumuhi, amesema: Ametueleza Musadad ibn Masrahad amesema: ametuelezea Alharith ibn Ubaid, kutoka kwa Muhammad bin Abdil Malik bin Abi Mahdhuura kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kasema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allah (SAAW) nifundishe Sunna ya adhana, akasema: Akapangusa komo langu na akasema: “Utasema hivi:

الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر

Akanyanyua kwayo sauti yake, kisha utasema:

أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله، أشهد أن محمدا رسول الله،

Na hafifisha kwayo sauti yako, kisha utanyanyua sauti yako kwa ajili ya shahada:

أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله،

Na ikiwa sala ya asubuhi utasema:

الصلاة خير من النوم، الصلاة خير من النوم، الله أكبر، الله أكبر، لا إله إلا الله

Na hivi ndivyo inavyodhihirika kwamba tangazo la kujirejea katika sala ya alfajiri kuwa ni Sunna iliyothibiti. Na ikiwa kuna yanayosemwa katika baadhi ya riwaya, basi zipo riwaya wamezitaja kuwa ni sahihi baadhi ya wenye elimu mashuhuri na wakazichukua wengi katika mafuqaha, yaani kuwa tangazo la kujirejea lilikua wakati wa Mtume (SAAW) na Makhalifa waongofu na mpaka siku zetu hizi. Nalo si bid’a bali ni Sunna iliyothibiti zimepokelewa kwajili yake dalili sahihi… Kama tulivyobainisha hapo juu.

Nataraji jibu hili kuwa linatosha na limetosheleza.

Ndugu yenu Ata Ibn Khalil Abu Rashta

23, Jamadul Akhir 1440H

28, February 2019

Maoni hayajaruhusiwa.