Kareti 18 Zina Thamani na Hutolewa Zaka

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

Swali:

(Kichwa cha habari nambari 836 “Zakat huwa ni dhahabu safi”

Je kareti 18 za dhahabu zina thamani ya kimada) Mwisho

Jawabu

Hakika maoni yako yaliyotajwa ni kuhusu kichwa cha habari nambari 836 ambacho ni sehemu ya jawabu la swali la tarehe 2 Safar 1437H sawa 14/11/2015. Na haya hapa ni maelezo yaliyokuwemo kwenye maudhui hiyo:

(Hakika ya hukmu ya zaka katika dhahabu ni hasa kwa dhahabu safi ya kareti 24, na pia hukmu ya zaka katika fedha ni hasa kwa fedha safi. Kwa hiyo dhahabu ikichanganyika na kitu chengine au fedha ikichanganyika na kitu chengine, basi kitatolewa hicho kitu chengine katika kipimo, halafu kitakachobakia baada ya kutoa hicho kitu chengine kiwe kimefikia nisabu (yaani hiyo dhahabu au fedha iwe imefikia nisabu). Kwahiyo mtu akimiliki gramu 85 za dhahabu ambayo ni dhahabu ya kareti 18, huyo huwa hamiliki nisabu , kwasababu dhahabu safi humo ni chache kuliko gramu 85… Kwani zaka ya pande la dhahabu la kareti 24 ni tofauti na zaka ya pande la dhahabu la uzito huo huo wa kareti 18, na hukadiriwa dhahabu safi wakati wa mahisabu ya nisabu kuwa nisabu ya dhahabu ya kareti 24 ni gramu 85.

Lakini nisabu ya dhahabu ya kareti 18 ni zaidi ya hiyo kwasababu imechanganyika na kitu chengine kwa kiwango cha robo ambacho si dhahabu, yaani dhahabu ya kareti 18 ambayo ina dhahabu safi sawa na robo tatu ya dhahabu ya kareti 24. Kwahiyo, nisabu  ya dhahabu ya kareti 18 ni moja na thuluthi ya nisabu ya dhahabu safi ambayo ni gramu 113.33. Kwahiyo, yule anaemiliki gramu 85 za dhahabu safi ya kareti 24 atakuwa amemiliki nisabu  na ikipitiwa na mwaka atatoa zaka yake ya 2.5% katika kipimo chake. Lakini anaemiiki gramu 85 za dhahabu ya kareti 18 huyu hamiliki nisabu mpaka anachokimiliki kifikie gramu 113.33 na ikipitiwa na mwaka atatoa zaka yake ya 2.5% katika kipimo chake. Ni wazi hapa kwamba cha kuzingatia katika zaka ni dhahabu safi.) Mwisho.

Nimeshangaa kwa maoni yako kwasababu yanafahamika kwamba sisi katika jawabu tumeporomosha thamani ya dhahabu ya kareti 18 hatukuifanya kuwa na thamani, wakati ambapo ni wazi katika jawabu kwamba dhahabu ya kareti 18 ina thamani na hutolewa zaka, lakini thamani yake ni ndogo kuliko thamani ya dhahabu ya kareti 24 ikiwa kipimo (uzito) ni mmoja, kwasababu hiyo ndio tumebainisha nisabu  hasa ya zaka ya dhahabu ya kareti 18  kwamba (moja na thuluthi ya nisabu ya dhahabu safi ambayo ni gramu 113.33. Kwahiyo, yule anaemiliki gramu 85 za dhahabu safi ya kareti 24 atakuwa amemiliki nisabu  na ikipitiwa na mwaka atatoa zaka yake ya 2.5% katika kipimo chake.

Lakini anaemiiki gramu 85 za dhahabu ya kareti 18 huyu hamiliki nisabu mpaka anachokimiliki kifikie gramu 113.33 na ikipitiwa na mwaka atatoa zaka yake ya 2.5% katika kipimo chake), kwahiyo, thamani ya dhahabu ya kareti 18 haijaporomoshwa katika jawabu bali thamani yake ni thabiti na hutolewa zaka ikifikia nisabu timilifu kama inavyotolewa zaka dhahabu ya kareti 24 inapofikia nisabu , kwa jumla ni kwamba kiwango cha nisabu cha kila moja kati ya hizo mbili hutofautiana na kiwango cha nisabu cha nyengine, kwasababu dhahabu ya kareti 18 imechanganyika na madini nyengine kwa kiwango cha robo.

Na sifahamu sababu ya maoni yako, isipokuwa ikiwa umelisoma (jawabu) kwa pupa la jambo lako! Kwa hiyo, rejea kulisoma kwa mazingatio Allah akurehemu… Na namuomba Allah uongofu kwa wote kwenye jambo lililonyooka zaidi.

Ndugu yenu Atta Ibn Khalil Abu Rashtah

01 Dhulqada 1440H

04-07-2019

Maoni hayajaruhusiwa.