Kampeni ya Kumbukizi ya Miaka 100 ya Kuangushwa Khilafah Yaanza Kwa Kishindo Tanzania

بسم الله الرحمن الرحيم

Katika sehemu ya kuanza kampeni ya kiulimwengu ya kumbukizi ya miaka 100 ya Kuangushwa Khilafah inayoendeshwa na Hizb ut Tahrir, wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Tanzania leo tarehe 01 Rajab 1442 H – 13 Februari 2021 M nje ya misikiti ya mikoa mbalimbali nchini walifanya kisimamo maalumu (picketing) kilichoambatana na mabango ya kampeni, bendera za Mtume (Saw) na kalima fupi.
Katika kalima hiyo wanaharakati hao waliwakumbusha Waislamu na walimwengu kwa jumla juu ya msiba mkubwa wa kuanguka Khilafah uliotokea ndani ya mwezi wa Rajab 1342 (Machi 1924), maafa na majanga yaliyofuatia na mwisho kuwataka wajifunge na wajibu wa kushirikiana na Hizb ut Tahrir kufanya kazi ya kuirejesha dola ya Khilafah inayopaswa kuanzia katika nchi kubwa za Waislamu kwa kutumia manhaj/ njia ya Mtume SAAW isiyohusisha nguvu, mabavu wala silaha.
Miongoni mwa maeneo yaliyozinduliwa kampeni hiyo kwa kisimamo ni Msikiti wa Kichangani Magomeni, Msikiti wa Mtoro Kariakoo, Msikiti wa Idrisa Kariakoo na Masjid Nuru Mbagala yote ya Dar es Salaam, Pia Zanzibar Msikiti wa Mchangani Msikiti wa Mbuyuni, yote ya Darajani pamoja na Masjid Qatar Chakechake Pemba, mengine ni Msikiti wa Ijumaa Mwanza mjini, Tanga mjini nk.
Kampeni hiyo ya Hizb ut Tahrir imezinduliwa leo rasmi kimataifa, itaendelea ndani ya mwezi wote wa Rajab na itahusisha harakati mbalimbali ulimwengu mzima katika maeneo ambayo Hizb ut Tahrir inafanya harakati zake.
Matukio kwa Picha. 

Maoni hayajaruhusiwa.