Hukmu Kuhusiana na Uigizaji na Kutazama Filamu Zinazo Igiza Mitume na Maswahaba

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

Swali:

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh Ewe Shaikh.

Ni ipi Hukmu kuhusiana na kutazama filamu na vipindi vinavyo igiza mitume na maswahaba?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Filamu na vipindi katika uhalisia wake wa sasa haviruhusiwi kwa mujibu wa shari’ah, kwa sababu vinajumuisha kudanganya, vimejaa mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake, na uchi kuonekana kwa sababu wanaume wa kando (wasiokuwa mahram) wanachukuwa dori za waume na Mahram, na kisha uchi wa wanawake unadhihirishwa kwao. Hivyo basi, ukiukaji wa hukmu za kishari’ah unatendeka moja baada ya nyingine. Kwa hivyo, filamu na vipindi hivi haviruhusiwi kwa mujibu wa Shari’ah kwa sababu ya ukiukaji huo wa kishari’ah. Ule ukiukaji ambao ni mkubwa na hata mkubwa zaidi wa shari’ah ni pindi maswahaba wanapoigizwa. Kisha dhambi baya na kubwa zaidi ni pindi mtu wa kawaida anapo wakilisha manabii na mitume, pasi na aibu au hofu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Nyuma tulitoa Jibu la Swali kuhusu mada hii mnamo 23/09/2009 na tutakutajia tena kwa manufaa zaidi:

(Ama kuhusu uigizaji na vipindi, vimejaa ukiukaji mwingi wa shari’ah:

A- Zinajumuisha kudanganya, kwa sababu mtu hujifanya kuwa mtu mwengine na kuzungumza maneno ya mtu huyo mwengine anaye mwakilisha, kwa hivyo husema na kusema hata kama itahitajika kwake kuapa kwa kuwa mtu anaye mwakilisha aliapa naye anaapa, na juu ya hayo tangazo la talaka hupitia mdomoni mwake endapo huyo mtu mwengine ametaliki. Na mtu huhisabiwa kwa yale anayo tamka kwa urongo, hata kama anafanya mzaha.

B- Zinajumuisha mchanganyiko, kwani wanaume na wanawake wako pamoja pasi na haja iliyo ruhusiwa na shari’ah,

C- Kudhihirisha uchi, kwa sababu wanaume wa kando wasio Mahram huwakilisha dori za waume na Mahram, kwa yale yanayohitaji kutofinikwa uchi kama inavyo pasa mbele ya wasiokuwa Mahram, pamoja na yale yanayo tendeka juu ya kustiri uchi, kama vile mahusiano mengine kati ya wanaume na wanawake wanao wakilisha dori za waume na Mahram.

Ni wazi kutokana na ukiukaji huu mkubwa wa sheria. Na lile ambalo ni kubwa zaidi kuliko hilo na hatari zaidi katika ukiukaji wa shari’ah ni pale ambapo dori za mitume huwakilishwa, kwani mitume wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia Utume na risala, na ni fadhla kwake yeye pekee, na si kwa mtu yeyote mwengine. Hivyo basi, uwakilishaji wa Nabii au Mtume aliye teremshiwa wahyi kupitia mtu wa kawaida ni kufanya uovu dhidi ya ujumbe huo, na kufeli kuupa Utume haki yake, na kutoupa ujumbe huo thamani yake, na hiyo ni dhulma kubwa kwa ujumbe na Mtume huyo. Hii ni ikiongezewa na ukiukaji mwingine wa shari’ah ulioenea hatua zote za uigizaji wa mahusiano ya wanaume na wanawake …nk.

Hivyo basi, vipindi na tamthilia hizi haviruhusiwi. Ama kuhusu msimamo wa dola ya Khilafah wakati itakapo simamishwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, haitaruhusu uwakilishaji na vipindi vinavyo husisha ukiukaji wa shari’ah, lakini kuhusu maelezo ya hilo, na namna jambo hili litakavyo kuwa wakati huo kuhusiana na vitendo hivyo, tutaelezea wakati huo, InshaAllah. Mnamo 23/09/2009). Nataraji hili linajibu swali lako kwa kutosheleza, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi Mwingi wa hekima.

Zingatia:

Kwa kaka na dada wote waliochangia maoni katika Jibu la Swali kuhusu utazamaji na kusema kuwa jibu lilikuwa kuhusu uigizaji na sio utazamaji Mimi nasema: tayari nimejibu uharamu wa uwakilishi uliotajwa katika swali (yaani kuonyesha watu wanao wawakilisha Mitume na Maswahaba) na nimesema kuwa hili haliruhusiwi na kwamba dola, pindi itakapo simamishwa, itazuia hili. Sikujibu kuhusu utazamaji, bali niliiwacha kadhia hii kwa waulizaji ili wafanye ijtihadi juu ya kadhia hii au kumfuata yeyote anaye kadiriwa kuwa ni Mujtahid ambaye wana imani na ijtihadi yake. Kwa maana nyingine, siku jengea hoja juu ya jambo hilo.

Nataraji kuwa jambo hili liko wazi.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

28 Rabii’ II 1441 H

Jumatano, 25/12/2019 M

Maoni hayajaruhusiwa.