Huduma Za Kijamii Katika Demokrasia Zimegeuzwa Ni Hitajio La Ziada.
بسم الله الرحمن الرحيم
Hali ya utoaji na usambazaji huduma za kijamii ulimwenguni si nzuri kwa sehemu kubwa. Kukosekana kinga kwa maradhi yanayotishia maisha ,ukosefu wa elimu ya afya na magonjwa kwa raia, kukithiri kwa magonjwa sugu, kutokuwepo kwa tafiti halisia zenye nguvu za matibabu ya magonjwa ambazo zinazohusiana moja kwa moja na magonjwa msingi ya raia na mahitajio yao ya kiafya.
Serikali za ulimwengu baada ya kushindwa kuhudumia raia wametoa jukumu hilo kwa watu na makampuni binafsi ambayo badala ya kutoa huduma yanafanya biashara juu ya afya za watu huku serikali zikiwa hazina udhibiti wowote bali kukusanya kodi tu. Hali hii imesababisha kubadilika kwa mwelekeo wa utoaji wa huduma kutoka kuwa ni hitajiolmsingi la kijamii na kuwa ni fursa kubwa yenye maslahi na manufaa kibiashara hivyo mwenye nacho ndio ana uhakika wa kupata huduma nzuri.
Gharama za matibabu zimekuwa ghali mno mahospitalini kwa matibabu ya upasuaji, kulazwa, huduma za kumwona dakatari, dawa na vipimo vya magonjwa kumefanya matibabu ambayo asili ni nafuu kuwa ni magumu kwa watu wengi.`Huduma bora ya afya imekuwa ni anasa. Utoaji huduma za afya na utafiti wa dawa za matibabu ya magonjwa mbalimbali umebinafsihwa kuwanufaisha kikundi kidogo cha watu ambao kwa sasa wananufaika kwa kupitia ufukara wa mamilioni ya watu wengi. Matokeo ya sera ya ubinafsishaji wa madawa na matibabu sasa imekuwa ghali kwa raia kumudu huduma za afya nchi mbalimbali ulimwenguni.
Amma kwa upande wa kielimu ,serikali zimeshindwa kubuni sera bora ya elimu na kuitengea bajeti finyu sekta hii katika nchi zinazoendelea kumepelekea kuibuka mripuko wa taasisi binafsi za elimu yakiwemo mashule na vyuo ambapo imegeuzwa elimu kuwa ni biashara ya gharama kubwa hivyo watu wanyonge wakashindwa kuimudu huduma hii.Leo twashuhudia ongezeko la vyuo binafsi huku serikali ikimiliki idadi ndogo ,hivyo kusababisha wazazi kubeba mzigo mkubwa wa gharama za masomo.
Amma kwa upande wa nishati ya umeme umekuwa ghali sana na baadhi ya miji kutofikiwa na nishati hiyo. Mgawo wa umeme umeendelea kuathiri maisha ya watu, ikiwemo mahitaji binafsi ya nishati hiyo katika ngazi ya familia, uzalishaji bidhaa na huduma katika nchi zinazoendelea. Kwa sasa viwanda vimeendelea kulalamikia gharama za uzalishaji kupanda,kutokana na upungufu au ukosekanaji wa nishati duniani. Hali hii imechochea mfumuko wa bei za bidhaa, hasa zile za viwandani, pamoja na gharama za huduma kuendelea kuwa juu na kuumiza mifuko ya raia.
Uislamu unalazimisha uangalizi wa dola(serikali ya Kiislamu) juu ya utoaji wa huduma za kijamii (elimu,tiba n.k) na pia ukiruhusu sekta binafsi kutoa huduma hizo kibinafsi chini ya taratibu maalum zilizoratibiwa na uislam . Huduma za kijamii za serikali lazima ziwe bure kwa raia wote wa dola ya Khilafah,Waislamu na wasio Waislamu. Huduma hizi lazima zipatikane, zisambazwe kwa haraka, ziwe endelevu na ziwe za ubora wa hali ya juu. Kinyume na mfumo wa urasilimali umegeuza huduma za kijamii ni biashara na sio haki ya msingi kwa kila raia imfikie.
Makhalifa muda wote walihakikisha uangalizi wa dola juu ya huduma za jamii. Katika nyakati za baadaye za Khilafah, hospitali zilidhaminiwa na wakfu za Waislamu, japokuwa fedha kutoka hazina ya serikali ilitumika kuzikarabati baadhi ya hospitali
Hakika serikali ya Kiislamu ilisimamia kwa ukaribu uendeshaji na usambazaji wa huduma msingi kwa raia wake kama hospitali,chakula ,makazi n.k na pia kulikuwa na ufuatiliaji wa kimahakama juu ya masuala yanayohatarisha haki za raia kama uzembe katika utoaji wa huduma ,ubadhirifu wa mali za umma n.k haukuwachwa kuwa chini ya madai ya mtu binafsi bali qadhi akiitwa Muhtasib aliwakabili wenye kufanya udanganyifu na kuwaadhibu. Wajibu wa Qadhi Muhtasib kuhusiana na huduma za afya ulijumuisha kuhakikisha kuwa vipimo sahihi vinatumika katika dozi za kitabibu,akisisitiza juu ya elimu ya usafi, akikemea majengo mabovu na kuhakikisha usambazaji wa maji safi na mambo mengine yanayohusiana nayo.
Mwisho huu ndio uovu wa demokrasia kwa kutumia mwamvuli wa ubinafsishaji umeweka kanuni kumwezesha mtu binafsi kunufaika kutokana na rasilimali za ummah na kuwaruhusu matajiri kuvuka nchi moja kwenda nchi nyingine kupora mali hizo. Tafsiri yake ni sawa na kuhatarisha maisha ya jamii nzima kuifanya kuwa mtumwa kwa huyu mmoja aliyebinafsishwa. Kwa sababu vyanzo hivi ni sehemu nyeti katika uhai wa binaadamu hivyo kumilikishwa mtu mmoja ni kuhatarisha maisha ya wengine na anaweza kuwafanya kuwa watumwa kwa sababu maisha yao yatakuwa mikononi kwake.
Mtume (saw) ametuletea dini iliokamilika ambayo imeusimamisha Ummah wa Kiislamu juu ya msingi imara, ikaunyanyua kuwa Ummah bora zaidi ulioletwa kwa watu.
Katika wakati wa utawala wa Kiislamu, Ummah huu uliongoza katika nyanja zote za maisha ikibeba ushahidi wa utukufu wa Dini yake, ambayo ni roho ya maisha yake. Na inshaallah Uislamu utarejea ukiwa ni dola ya Khilafah na kuongoza wanaadamu kama alivyotubashiria Mtume wetu (saw)
Salum Maulid
Risala ya Wiki No. 128
24 Rajab 1443 Hijri /25 Februari 2022 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut Tahrir Tanzania
#WahyiChimbukoLaThaqafaYetu
#KataaUislamuMamboLeo
Maoni hayajaruhusiwa.