Dhul Hija Ni Neema Ya Kiroho Kwa Waumini Na Faraja Ya Kiuchumi Kwa Saudia

Msimu wa Hijjah umewadia mwaka 1439 H . Kama kawaida waislamu popote walipo wanakwenda kutekeleza amri ya Mola wao Mlezi ya kuhiji kwa mwenye uwezo . Na wale ambao hawakujaaliwa kuwa na uwezo watafunga siku ya Arafah kuungana na ndugu zao wanaofanya ibada ya Hijjah katika mji mtukufu wa Makka. Allah awalipe thawabu na ibada zao ziwe makbul inshaallah.
Na utawala wa Saudia nao uta neemeka kwa biashara kubwa ya kitalii kutokana na waislam kumiminika katika miji kadhaa ya nchi hiyo kwani utawala huo hijja kwake si ibada bali ni biashara na utalii
Huku wengine kila pembe ya dunia wakibaki na mateso, idhilali, dhiki za maisha na njaa , maradhi ya miripuko na ya muda mrefu, vilema vilivyosababishwa na kuwa kwao waislam .Ama kwa ndugu zetu wa Yemen hukumbuka mikondo ya damu za ndugu zao zilizo mwagwa na wakoloni wa Kimagharibi na Asia kwa msaada mkubwa wa kiranja mkuu namba mbili wa vibaraka wao Mashariki ya kati, utawala wa Saudia.
Waislamu pembe zote za dunia hufunga safari kwa vipandwa vya kila aina wafike Mji mtukufu wa Makka kwa idadi ya mamilioni ,wakionyesha mshikamano wao kama ummah mmoja ,kutekeleza ibada ya Hijjah kama walivyoamrishwa na Allah swt na kumalizikia na ibada ya kuchinja ili walipwe thawabu . Kama anavyosema :

وَأَذِّنْ فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالاً وَعَلَى كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِنْ كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ
“Na utawatangazie watu Hijja watakujia wengine kwa miguu na wengine juu wanyama waliokonda kwa machofu ya njiani kutoka kila njia ya mbali”
(22:27).

Jambo linalo huzunisha ni kuwaacha nyuma ndugu zao waislamu kila kona ya dunia wakiwa wahanga wa mateso , kuachwa vilema , njaa na maradhi pamoja na kumwagwa damu zao . Maafa hayo yamesababishwa na vita visivyoisha katika miji yao vinavyofanywa na mabeberu wa nchi za Magharibi na washirika wao huku watawala wa nchi za Mashariki ya kati ikiwemo Ufalme wa Saudi ukichukuwa nafasi ya ukiranja mkuu namba mbili kutimiza matakwa ya mabeberu hao. Saudia imevamia Yemen na kuuwa waislamu zaidi elfu kumi (10000) na kuwaacha zaidi ya watu 2.5 mil wakitanga tanga na kusumbuka kwa njaa. http://foreignpolicy.com/…/civilian-casualties-war-crimes-…/.

Masuala ya kuwagawa waislamu ki madheheb hayafai katika uislamu. Waislamu ni ummah mmoja licha ya tofauti za kimadhehebu. Na ni uwongo wa Saudia ulio wazi kuwa uvamizi wao kwa kisingizio cha madhehebu si agenda yao ya msingi kutokana na sababu ifuatayo:
Kwanini inashindwa kunyanyua hata kidole kuunyooshea utawala wa Kizayuni wa Israel unaoangamiza waislamu wa Palestina ambao ni masunni Hayo masilaha ya bilioni 100 ya dola inayonunuwa kutoka Marekani kwa ziara ya Trump pekee nchini Saudia yatatumika kwa ajili gani?
https://www.washingtonpost.com/…/trump-gets-elaborate-welco….

Ni dhahiri kuwa utawala wa Saudia unanunuwa na kurundika silaha kali kupambana na uislamu na waislamu kwa manufaa ya agenda ya mabeberu wa kimagharibi na washirika wao.
Kinachoisukuma Saudia kujikweza na kuweka mazingira mazuri ya kuratibu msimu mzima ni umuhimu hijjah kwa uchumi wa Saudia na hujizolea mamilioni ya dola kutoka kwa mahujaji wanaomiminika nchini humo kila mwaka.Mtiririko wa fedha wa msimu wa hijjah na umra ni zaidi Us $ 30 bilioni (Dh 110.2 bilioni) kila mwaka wanazolipa mahujaji kugharamia safari za ndani, malazi , mahitaji ya chakula ,kuchinja na matumizi mengineyo. http://gulfnews.com/…/a…/haj-vital-to-saudi-economy-1.533412.

Kwa hivyo msimu wa hijja kwa utawala wa Saudia ni fursa muhimu ya biashara ya utalii zaidi kuliko tukio lenyewe la hijjah na mahujaji.
Kwa mintarafu wa mambo ulivyo kihukmu na hata kiwakia, mustakbali wa mfumo wa maisha ya waislamu , usalama wao na kadhia zao , utawala wa Saudia hauna sifa hata chembe ya kuusimamia uislamu na waislamu. Jee bado kuna mwenye shaka kuwa kusimama kwa khilafah ni hitajio la waislamu kihukmu na hata kiwakia?. Tuungane sote kukataa ghilba ya mawakala wa ukafiri na nguvu zetu tuelekeze kusimamisha Khilafah rashidah.
#UislamNiHadharaMbadala

Na Suleiman Mbarouk(Ticha sule)

Maoni hayajaruhusiwa.