Inna lillah Wainna ilayhi Rajiun

Tumepokea taarifa za huzuni na masikitiko kufuatia Sheikh Mussa Kileo Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Hizb ut Tahrir Tanzania kufiliwa na baba yake mdogo Ustadh Said Ally Kileo (pichani)

Marehemu ambaye ni Imamu wa Masjid Aqswah kijijini Kilimilang’ombe, Handeni Tanga, Mwalimu wa Madrasa na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa, Bakwata Wilaya ya Handeni amefariki ghafla jioni ya leo Mkoani Handeni

Marehemu atazikwa Kesho jumapili 19 Agosti 2018 Laasiri Inshaallah huko huko Handeni.

Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania natoa mkono wa ta’azia kwa Sheikh Mussa Kileo, ndugu, Jamaa na Bakwata Tanga kufuatia msiba huu mkubwa.

Tunamuomba Allah Taala Awalipe wafiwa ujira mkubwa, Amsamehe na kumrehemu marehemu na kumuingiza katika Pepo ya darja ya juu

Amiin

18 Agosti 2018

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.