Biden ataendeleza sera zilezile za Kibebari kama alivyokuwa Trump na waliomtangulia

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakuna shaka yoyote kwamba uchaguzi wa Marekani unakuwa ni wenye kufuatiliwa kote duniani. Kinachofanya uchaguzi huu ufuatiliwe ni nafasi ya Taifa hili ambalo ndio taifa kuu duniani (Super Power) linaloathiri pakubwa hali ya kimataifa. Uchaguzi wa hivi karibuni ulikuwa ni kati ya Donald Trump wa Republican –rais wa sasa na Joe Biden – wa Democrat aliyeibuka kuwa mshindi kwa kupata kura 270 za wajumbe dhidi ya 214 alizopata Trump. Tunaweza kugawanya wafuatiliaji wa uchaguzi wa Marekani kwa mapote matatu. Lakini kabla ya kuyajua,ni muhimu kufahamu kwamba kwetu Sisi Waislamu ni wajibu kufuatilia kila kadhia inayojiri leo duniani kwa sababu  kadhia zinazotukia duniani zinaatuathiri kwa njia moja au kwa njie nyengine. Hivyo ni makosa kutoshughulisha na siasa za ulimwengu ikiwemo siasa za Marekani. Hakina ni kudumaa kifikra kusemwa kwamba Mambo ya Marekani hayatuhusu ndwele wala sikio!

Hapa ni ufafanuzi wa matabaka haya ya watu katika kuangalia uchaguzi wa Marekani.

Wakwanza wao ni wale  ambao daima dawamu huingalia Amerika kama baba yao na mlezi wao wa kisiasa. Wao hawajali ni chama kipi kimeshinda au mgombea yupi alieshinda,kazi yao kubwa ni kujipendekeza kwa yoyote yule sawa awe ni Democrat au ni Republican. Mfano wao ni viongozi wengi wa mataifa ya kiislamu  ambao huwa ni mawakala wa Amerika kupeleka ajenda zake.  Kwenye kundi hili wanaingia pia wale ambao huangalia chama kilichoshinda na mgombea alieshinda pia. Wote kwa pamoja ni watumwa wa Amerika kwani hupokea maaigizo kutoka kwa Amerika hatakama ni ya kutumbukiza raia wao kwenye hatari. Hawa ndio wale ambao utawaona wakipongeza haraka mgombea aliyeshinda. Huyu hapa waziri mkuu wa Iraq  Mustafa Kamal Al-Kadhimy akimpongeza Joe Biden:

“Ninatuma pongezi zangu za dhati kwa rais mteule wa Marekani Joe Biden, na makamu rais mteule Bi Kamala Haris nikitarajia kwamba tutaendelea kudumisha mahusiano ya kistratejia baina ya mataifa yetu mawili kuweza kufikia kwenye mustakabali mwema”

Naye raisi wa Uturuki ambaye alikuwa mwandani wa Trump alimpongeza Biden kwa kusema:

“Ninakupongeza wewe kwa kuchaguliwa kwako huku nikiwaombea kwa udhati  wa moyo wangu amani na mafanikio kwa watu wa Marekani.” Akaendelea kusema kwamba  Ninakariri nia yetu kufanya kazi kikaribu na utawala wa Marekani na ninaamini kuwa mahusiano na ushirikiano wa nchi zetu mbili utaendelea kuchangia kuweko kwa Amani duniani katika siku za usoni kama ilivyo leo.”

Kwa ufupi salamu za pongezi zilimiminika kwa Biden kutoka kwa mataifa mengi ya Kiislamu!  Hii ni wazi kuwa viongozi hawa wao huridhika na Marekani na ndio wanaofaulisha njama za kiudui za Marekani dhidi ya Umma wa Kiislamu ambao unaendelea kuishi kwenye utumwa na unyanyasaji. Ni aibu mno kusikia Iraq ambayo hadi wa leo inauguza mejeraha makubwa baada ya oparesheni ya Desert Storm ambao maelfu ya watu watu waliuwawa na jeshi la Marekeni.

Kundi la pili la wanaofuatilia uchaguzi na matokeo ya Amerika ni lile na siku zote wao huigopa nchi hii  pasina na kutilia umuhimu wowote wa chama kilichoshinda au raisi aliyeshinda. Hii ni kwa kua Marekani kwao wao ni  adui yao na mpinzani wao katika masuala mengi hasa masuala ya kiuchumi. Mfano mzuri , hapa ni wanasiasa wa mataifa kama vile China na Korea Kaskazini. Mataifa haya japo hayana ruwaza ya kutawala duniani kimfumo lakini yanazunguka duniani hasa barani Afrika kupora Malighafi. Wao hufuatilia uchaguzi wa Amerika na kupatiliza udhaifu wake ili wajiimarishe kiuchumi. Hawa mara nyingi husita kumpongeza rais yoyote anayechaguliwa Marekani au chama. Nchi hizi mara nyingi huwa hawataki kuburutwa na Marekani sio kwamba wana mfumo mzuri bali ni  suala tu la ung’anganizi wa rasilimali za dunia.

Kundi la mwisho ni lile ambalo halitegemei wala kuiogopa Marekani. Hawa hukumbuka daima kuwategemea maadui wa Uislamu ni kumfanyia Khiyana MwenyeziMungu, Mtume wake na Waumini kwa ujumla. Hawashawishiki na misemo ya Trump au Biden bali huichanganua  na kubaini hatari na sura ya uadui inayobeba. Hawa na wale waliosoma aya katika suratul Hud ambapo Allah ni mwenye kusema:

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

Wala msiwategemee mkawa pamoja nao wale waliodhulumu nafsi zao usije ukaguseni Moto. Na hamtakua na mlinzi mbele ya MwenyeziMungu kisha nyinyi hamtasaidiwa.

Marekani kutawala duniani sio majaaliwa na haya yanayojiri kwa sasa mporomoko wa uchumi, kuwa na sera za ubaguzi imefichua wazi kushindwa kwa Mfumo wake kuongoza duniani. Mfumo wake ndio imefikisha dunia mahala hapa ufisadi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Wala haitarajiwi hali kubadilika kuja kwa Biden na watakaokuja baada yake kwani wote hawa ni wana sera za kuzunguka dunia na kueneza humo ufisadi na kuangamiza wanyama na mimea.

Pote hili nilile linalofuatilia siasa za Marekani ikiwemo uchaguzi wake kama sehemu ya kujua uhalisia wa dola hii na sera zake, na mipango yake pamoja na mbinu zake. Wanafuatilia yote hayo ili wawe na ufahamu halisi wa Marekani huku wanafanya kazi ya kubadilisha Ulimwengu uongozwe na mfumo wa Uislamu badali ya mfumo wa Kibepari anaouongoza Marekani na kuulingania duniani kote.

Mwisho, hakika uchaguzi wa hivi punde umefichua zaidi aibu za Demokrasia jinsi inavyotawaliwa na viongozi wenye semi za chuki dhidi ya raia wake. Trump kwake iko wazi na matamshi yake dhidi ya Waislamu wa Amerika katika sera zake za suala la wahamiaji. Ama Biden anajulikana wazi kuwa yeye alipokuwa mmoja wa wanakamati wa kamati ya mahakama alisukuma kupitishwa kanuni za kikatili dhidi ya wamerekani weusi inayojulikana kama Violent Crime control and Law Act. Mbali na haya mzee huyu atakumbukwa mchango wake mkubwa katika mauaji ya halaiki huku Darfur na hii alihinikiza mauaji pale alipokuwa  mwenyekiti wa kamati ya baraza la senate ya mahusiano ya kigeni. Hivyo kuja kwake uongozini ni muendelezo tu wa sera za kibeberu za Marekani

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya.

   Makala NO 109

Maoni hayajaruhusiwa.