Barua ya Wazi Kwa Mufti wa Oman na Wanavyuoni Jumla Nchini Oman

Kwa:
Wanavyuoni wa Kiislamu nchini Oman, hususan Mufti Mkuu Sheikh Ahmad bin Hamad al-Khalili

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

أخرج مسلم في صحيحه في باب “فَضْلِ أَهْلِ عُمَانَ” عَنْ أَبِي الْوَازِعِ جَابِرِ بْنِ عَمْرٍو الرَّاسِبِيِّ سَمِعْتُ أَبَا بَرْزَةَ يَقُولُ:
بَعَثَ رَسُولُ اللَّهِ رَجُلًا إِلَى حَيٍّ مِنْ أَحْيَاءِ الْعَرَبِ فَسَبُّوهُ وَضَرَبُوهُفَجَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ فَأَخْبَرَهُ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ: «لَوْ أَنَّ أَهْلَ عُمَانَ أَتَيْتَ مَا سَبُّوكَ وَلَا ضَرَبُوكَ»،
Imepokewa kutoka kitabu cha Sahih Muslim katika mlango wa “Fadhila za watu wa Oman’ kutoka kwa Abu al-Wa’dh’ Jabir ibn Amr al-Rasibi: Nimemsikia Abu Barzah akisema: Mtume SAW alimtuma mtu kwa kabila miongoni mwa makabila ya Waarabu, watu hao wakamtukana na kumpiga (mtu huyo) Kisha mtu yule aliporudi kwa Mtume SAW akamsimulia yote (kuhusiana na ukatili aliofanyiwa na watu wa kabila lile) Hapo, Mtume SAW akasema :
“Lau ungekwenda kwa watu wa Oman wasingekutukana wala wasingekupiga”

Basi angalieni, Rehma za Allah (SW) ziwe juu yenu (watu wa Oman) angalieni namna Mtume SAW alivyoutaja wema mkubwa wa watu wa Oman, kutokana na utambuzi wa Mtume SAW juu ya wema na utoharifu wao. Leo sisi Hizb ut Tahrir haswa, na kwa niaba ya Ummah wa Kiislamu amma, wakiwemo watu wa Oman, tunatoa mwito kwenu msimamie amana ya Ummah kama mlivyokuwa kabla, na yabebeni majukumu yenu ipasavyo, ambayo Allah Taala ameyafanya kuwa ni amana juu ya shingo za wanavyuoni, majukumu hayo ni kuwawajibisha / kuwahesabu watawala, kuzuiya dhulma zao wanazozifanya na kuzuiya upotofu wao wanapokwenda kombo.

Taarifa za karibuni kuhusiana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, kwamba Israel ina wasiwasi mkubwa juu ya mustakbali wake, na kwamba waarabu wanapaswa kuiliwaza na kuondoa khofu zao (mayahudi). Kauli hizi na mapokezi ya taadhima yaliyotangulia awali kutoka kwa Mfalme wa Oman kwa muhalifu Netanyahu, vinaonesha wazi kwamba watawala (wa Oman) hawana haya tena mbele ya Allah Taala wala mbele ya Waumini wa Allah SW. Wanadhihirisha waziwazi mafungamano yao na maadui wa Waislamu kwa kukipa nguvu kijidola cha mayahudi, waporaji na wavamizi wa mabavu ndani ya Palestina, na wanamchukulia adui na mvamizi huyo kwamba ni muhanga (aliyedhulumiwa ) eti anayestahiki huruma na maliwazo !

Wanavyuoni na masheikh ndani ya Oman, hususan wewe mtukufu Mufti, mnaheshimika na kuthaminiwa na watu wa Oman na mna haiba njema miongoni mwa Ummah, hivyo msiwavunje moyo wale waliojenga imani juu yenu, na kuweni kigezo chema kwa kutamka haki bila ya kumuogopa yoyote ila Allah Taala. Jukumu lenu kisharia ni kupinga na kujiweka kando kwa uwazi na kwa ujasiri na kutangaza hadharani kwamba mko mbali na matendo ya watawala wa Oman, ambayo ni kuleta mahusiano ya kawaida na kijidola dhalimu na cha kivamizi cha mayahudi, na kuitelekeza ardhi ya Palestina na Msikiti mtakatifu wa Al-Aqswa, kwa kuwakumbatia watawala wa dola ya Kiyahudi kuleta ukuruba nao, na kuwaonesha mbele ya watu kwamba wao ndio wanaodhulumiwa, ilhali wao ni waporaji wa ardhi, wavamizi wa mabavu na wauwaji.

Mtume SAAW anasema:
: «أَفْضَلُ الْجِهَادِ مَنْ قَالَ كَلِمَةَ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»،
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَأَبُو دَاوُد وَابْن مَاجَه،
“Jihadi Bora zaidi, ni kwa yule anayetamka kauli ya haki mbele ya mtawala jeuri”
(Tirmidh, Abu Daud na Ibn Majjah)

Kimya cha wanavyuoni kwa watawala madhalimu na khiyana yao hutumika na watawala hao kuhalalilisha khiyana hiyo na kumakinisha nidhamu zilizotungwa na wanadamu ambazo hazitokamani na aqiida ya Waislamu, bali ni zenye migongano nayo kamwe.(Watawala hao) hupuuza matakwa ya watu, kwa kuwa wanatumikia maslahi ya nchi za Magharibi na kuwasaidia kumakinisha udhibiti wao kwa nchi (zetu) na watu wake, kupambana na Uislamu na kuzuiya kurejea tena kwa maisha ya Umma kwa utekelezaji wa Uislamu ambao ni mfumo wenye kufafanua kila kitu na kutatua matatizo ya Waislamu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunatoa mwito kwa watu wa Oman na wanavyuoni wa Oman wanaopaswa kuwa mstari wa mbele, tunawalingania waungane katika mchakato pamoja na Ummah katika jukumu la kurejesha tena utawala utakaotawalia kwa yale aliyoyateremsha Allah Taala. Watu wa Oman ni wenye kuupenda Uislamu, na katika nyoyo zao wana ghera na hamu kubwa ya kuutabikisha Uislamu na kutoa Bay’ah kwa Imamu ambaye atatawalia watu kwa Kitabu na Sunnah na kuufikisha Uislamu ulimwenguni kote kwa Daawa na Jihadi.

﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿
“Enyi Mlioamini msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume (Mkaacha kufuata mliyoamrishwa) wala msihini amana zenu (mnazoaminiana) na hali ya kuwa mnajua” (TMQ 8: 27)

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
No: 1440 AH / 03
H. 1440 Shaaban 15
M. 2019 Aprili 21

Inapatikana kwa kiarabu:
http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/pre…/markazy/cmo/59595.html
Inapatikana kwa kizungu:
http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/central-media-o…/17345.html

Maoni hayajaruhusiwa.