Mashahidi wa Akhera na Swali la Qadhaa na Qadar

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Sheikh wetu mheshimiwa: Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, Mwenyezi Mungu akubariki na aulete ushindi kupitia mikono yako. Kuna swali juu ya kadhia ya Qadhaa na Qadar (jaala na kadari) katika kitabu Shakhsiya ya Kiislamu (Shakhsiya Islamiya), Juzuu ya Kwanza.

Kinapo zungumzia kuhusu vitendo vinavyo tukia ndani ya mzunguko unaomtawala mwanadamu katika upande usiokuwa wa kanuni za moja kwa moja za Ulimwengu, katika ukurasa wa 94 (nakala ya Kiarabu) kinaeleza, baada ya kutaja mifano, “na hivyo basi hatutalipwa ujira wa kuadhibiwa”.

Vipi tunaweza kuoanisha ibara hii na Hadith zinazo eleza kuwa Al-Mabtoon (anaye kufa kutokana na maradhi ya tumbo) na Al-Ghareeq (mfa maji) na yule aliye poromokewa na nyumba; ni mashahidi (mashahidi wa Akhera), ikiwa na maana kuwa wanalipwa ujira mkubwa, ingawa yale yaliyo watokea hayakutokamana na matakwa yao. Na Mwenyezi Mungu akubariki. Abu Hamdi Palestina.

Jibu:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ndugu yangu, mada inahusu haki juu ya vitendo vya khiari ya ujira au adhabu; yaani, vitendo vinavyo tukia ndani ya mzunguko anaotawaliwa na mwanadamu. Vitendo hivi ndivyo viliomo ndani ya mada ya ujira au adhabu, na endapo atatenda kitendo kilicho haramishwa, ataadhibiwa, na endapo atatenda kitendo cha faradhi atalipwa ujira, apendapo Mwenyezi Mungu.

Ama vitendo vinavyo tukia ndani ya mzunguko unaomtawala mwanadamu; yaani, kitendo ambacho hana khiari nacho, na hivyo haviko katika mada ya ujira au adhabu; yaani, haviko katika mada ya haki ya kulipwa ujira au adhabu, kwa sababu mtu huyo hakuvitenda kwa khiari yake.

Ama Mwenyezi Mungu kumruzuku mtu heshima kwa kitendo fulani ambacho hakukifanya kwa khiari yake, hili ni jambo jengine, kwani si katika mambo yanayo husu haki ya ujira au adhabu, bali ni rehma na fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hii ndio kadhia yake.

Kutokana na haya, Al-Mabtoon (anaye kufa kutokana na maradhi ya tumbo), na Al-Mat’oon (anaye kufa kutokana na maradhi ya tauni) nk. na kule kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amewafanya kuwa mashahidi; hawakuwa hivyo kutokana na khiari yao ya kujikurubisha na Mwenyezi Mungu (swt), na natija yake wanastahiki ujira; yaani, sio sehemu ya hadith ya Mtume (saw)

«الْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعِ مِائَةِ ضِعْفٍ وَالسَّيِّئَةُ بِمِثْلِهَا إِلَّا أَنْ يَتَجَاوَزَ اللَّهُ عَنْهَا»…

“Jema (Hasana) hulipwa mara kumi hadi mara mia saba, na ovu (Sayi’a) hulipwa ovu hilo hilo, isipokuwa ikiwa Mwenyezi Mungu atalisamehe.” [Bukhari]

Bali, ni heshima na ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Naomba hili liwe linatosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi Mwingi wa hekima.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

16 Ramadhan 1441 H – 9/5/2020 M

Maoni hayajaruhusiwa.