Muhammed Abdul Hafez Karejeshwa Misri Kwa Mabavu ili Akauwawe

Habari:

Utawala wa jiji la Istanbul umeanzisha uchunguzi wa kwanini limegundulika suala la kumrejesha Misri kwa mabavu muomba hifadhi Muhammed Abdul Hafez Hussein aliyeukimbia utawala wa Al-Sisi nchini Misri na kuomba hifadhi ndani ya Uturuki. Askari polisi wanane wa Uturuki wameshasimamishwa kazi kufuatia uamuzi huo wa kumrejesha Misri kwa nguvu Hussein ndani ya Januari 18 licha ya kuwa ameshahukumiwa hukmu ya kifo. (karar.com)

Maoni:
Muhammed Abdul Hafez Hussein, ambae alihukumiwa kifo na utawala wa kidhalimu wa raisi Al-Sisi wa Misri , aliwasili Uwanja wa ndege wa Istanbul mnamo Januari 18, hata hivyo alirejeshwa Misri kwa nguvu. Picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Hussein kaketi nyuma ndani ya ndege akiwa kafungwa pingu mikononi, imekuja kufunua wazi wazi wa uwepo wa mchakato wa kumrejesha Misri kwa nguvu. Pamoja na ukweli kuwa Hussein alieleza kwa ufafanuzi tena na tena kwamba yeye ni mwanachama wa Kundi la Ikhwan, na kwamba tayari kuna hukmu ya kifo mezani ikimsubiri, ombi lake hilo lilikataliwa na akarejeshwa kwa nguvu kukabidhiwa utawala dhalimu wa Misri.

Na kutokana na sauti kali za kupinga jambo hilo zilizopazwa kupitia mitandao ya kijamii, ndipo tayari kumeasisiwa uchunguzi unaowahusisha maafisa wa vyeo vya chini, ati kuwa wao ndio walioshiriki katika mchakato wa kumrejesha Hussein nchini Misri kwa nguvu.

Kama haitoshi kwa kashfa hiyo, pia akakamatwa bwana M. Emin Celik, mfanyakazi wa usafi wa uwanja wa ndege, na kuwekwa mahabusu kwa kudhaniwa kuwa yeye ndiye aliyesambaza mitandaoni picha za Hussein. Hatimae M. Emin Celik akaachiwa huru, baada ya kampeni kali ya kupinga kukamatwa kwake ndani ya mitandao ya kijamii kupitia anuani (hashtag ) ya #BenCektim (nilipiga picha).

Hii ina maana lau zile picha za muomba hifadhi Hussein zisingesambazwa, suala la urejeshwaji huo wa mabavu kwa utawala wa Sisi lisingejuulikana kamwe.

Abdul Hafez Hussein si muomba hifadhi wa mwanzo wala wa mwisho kutimuliwa kwa mabavu na serikali ya Uturuki kwenda kwenye hukumu ya kifo. Kuna maelfu ya Waislamu kabla, waliowahi kuomba hifadhi ndani ya Uturuki na wakarejeshwa kwa nguvu kwa watawala wauwaji, na bado wengi wanaendelea kurejeshwa kwa nguvu. Vituo kwa ajili ya kuhifadhia (waomba hifadhi) wanaotaka kurejeshwa vimesheheni Waislamu wa jamii ya Uzbek , Kighiz, Uyghurs. Mbali na hilo Uturuki ni nchi ambayo majasusi wa Urusi daima wanaingia wakitoka kama mwao, baada ya kuwauwa Waislamu wa Chechnia.

Aidha, Uturuki ndio nchi iliyokodolea macho mchakato wote wa mauwaji ya mwandishi wa habari (Jamal Khashogi) yaliyofanyika katika Ubalozi wa Saudia, pamoja na serikali ya Uturuki kufuatilia qadhia hiyo hatua kwa hatua ya mauwaji hayo kupitia idara ya ujasusi, kiasi cha hata kudiriki kuupata ukanda wa sauti na picha za vidio. Bado Uturuki ilibaki kimya, hata wakati wauwaji wakiondoka kama walivyokuja, ati baada ya hapo ndio inauliza mwili wa aliyeuliwa uko wapi, na kutaka ati wauwaji warejeshwe Uturuki.

Raisi Erdogan daima yuko kifua mbele kunadi kuwa Uturuki ni mahala salama kwa wanaodhulumiwa’. Ni aina gani ya mahala salama ambapo unamkabidhi aliyedhulumiwa akatiwe kitanzi, kuuliwa au kunyongwa? Dola hii ya Uturuki haina ghera wala haiko tayari kuwanusuru madhlumu ! Hali hiyo ndio Uturuki mahala salama?

Sio siri na kwa hakika sio jambo la kumshangaza yoyote kwamba kauli za Erdogan’ hazifanani na matendo yake. Anafanya ujanja wa kujifanya anajali Palestina huku anafanya makubaliano na kijidola cha mayahudi Israel, alimuunga mkono Mursi ndani ya Misri kwa alama ya Rabia, kisha akabadilisha maana ya alama hiyo kwa kushikamana na misimamo ya kisiasa ya Kamal Ataturk. Na tunaona namna anavyomkabidhi Abdul Hafez Hussein, mtu ambaye yumo katika orodha ya kunyongwa.

Raisi Erdogan anajifanya kupinga utawala wa Assad hadharani, ambae ni muuwaji wa karibu watu milioni, lakini wakati huo huo anakula njama na Urusi, Marekani, Iran ambao ndio waunga mkono wakubwa wa utawala wa Assad. Erdogan ndie aliyeikabidhi Alleppo kwa utawala wa Assad, na sasa yupo mbioni kufanya makubaliano ya kuitoa muhanga Idlib. Na hatimae ataikabidhi Syria yote kupitia makubaliano ya Adana.

Erdogan amekuja na muelekeo na tafsiri mpya kama alivyosema Waziri wake wa Nje kwamba : ‘tuna mawasiliano yasiokuwa ya moja kwa moja na utawala wa Syria’ kutokana na kauli hii ya ‘siasa za nje za chini kwa chini’, maana yake anakiri kuwa wana uhusiano na utawala wa Assad wa Syria kwa kupitia idara ya ujasusi. Si ajabu pia kuwa kitendo cha kumrejesha kwa nguvu Abdul Hafez Hussein kwa utawala wa Misri ni matokeo ya hizo siasa za kigeni za chini kwa chini?
Kwa hakika Erdogan kawashinda wasanii wengi katika tasnia ya sanaa. Alijifanya kumwaga machozi kwa wajane (waliondokewa na waume zao) wa Palestina, mayatima wa Syria, Waislamu wa jamii ya Rohingya na Waislamu wa Yemen, lakini badala ya kukomesha mauwaji, anakula njama na wauwaji. Machozi ya Erdogan ni kama machozi ya mamba kufurahia kiwindwa chake.

Nani awajibishwe kwa qadhia ya kutimuliwa kwa nguvu Abdul Hafez Hussein? Leo Erdogan unaweza kufunikafunika mambo kwa kuwahukumu polisi nane au kuweka shinikizo kwa vyombo vya habari. Unaweza pia kuhadaa kuhusu mauwaji haya (yanayomkabili Hussein) kwa kulitumia jeshi lako. Lakini jee unakwenda kusimama vipi mbele ya Siku ya Malipo?

Imeandikwa na Osman Ebu Erva
Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imefasiriwa kutoka:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/20…/news-comment/16913.html

Maoni hayajaruhusiwa.