20 Ramadhan

بسم الله الرحمن الرحيم

Siku kama hii tarehe 20 Ramadhani 8 Hijria ilitokea tukio kubwa la Fathi Makka. Waislamu walipata ushindi kwa kuiteka Makka na kuiweka chini ya himaya ya dola ya Kiislamu.

Tukio hili lilijiri baada ya miezi kumi na nane baada ya Mkataba wa Hudaybiyya baina ya Mtume SAAW na Makureishi.

Kama ilivyotarajiwa Makureishi na washirika wao wa kabila la Banu Bakr walivunja mkataba huo, na Waislamu chini ya Mtume SAAW hawakuwa na namna ila kuwavamia na kuiteka Makka.

20 Ramadhan 1441 Hijri – 13 Mei 2020 M

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.