Waziri Mkaliaganda: Mahabusu wa Miaka Karibu Mitatu Kwa Tuhuma za Ugaidi Afiliwa Na Dada Yake
Kwa huzuni na masikitiko makubwa tumepokea taarifa za msiba mkubwa wa kifo cha Bi. Ruqaiya bint Suleiman Mkaliaganda. Kifo kilichotokea Jumamosi magharibi mtaa wa Kiyangu, Mtwara Mjini baada ya marehemu kuwa mgonjwa kwa muda.
Maziko yalifanyika juzi Jumapili mchana, na maiti iliswaliwa katika Masjid Rawdha (baada ya dhuhri) na kuzikwa katika Makaburi Msafa hapo hapo Mtwara mjini.
Marehemu ni dada khaliswa (baba mmoja mama mmoja) wa ndugu yetu Waziri Suleiman Mkaliaganda ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya ugaidi ambaye bado ni mahabusu kwa karibu miaka mitatu sasa bila ya kesi yake kusikilizwa.
Kwa niaba yaHizb ut Tahrir Tanzania natoa mkono wa taa’zia kwa ndugu yetu Waziri Suleiman Mkaliaganda kwa msiba huu mzito ambao kutokana na sheria ya kibaguzi na uonevu maumivu yake yameongezeka maradufu kwa kukosa kumzika dada yake ambaye alikuwa akimhangaikia hapa na pale kwa ajili ya matibabu kabla ya kuwa mahabusu.
Pia, natoa mkono wa pole kwa familia nzima, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu, huku tukiwaombea Allah SWT awape ujira mkubwa na istiqama katika kipindi hiki kigumu.
Tunamuomba Allah SWT amsamehe marehemu, amrehemu na amuingize katika Jannah ya darja ya juu. Amiin
Inna lililahi wainna ilayhi rajiuun
04 Agosti 2020
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Maoni hayajaruhusiwa.