Unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania: Mzizi Wake Ubepari

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Imeripotiwa katika mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Tanzania kumezuka wimbi la wanawake hususan wanaoishi bila wanaume kuvunjiwa nyumba zao na kubakwa na wanaume wasiojulikana na iwapo watapinga basi hudhuriwa: https://africanarguments.org/…/tanzania-strange-worrying-r…/

Maoni:

Awali, tunalaani vikali vitendo hivi visivyo na tembe ya ubinadamu ambavyo vinavunja hadhi na heshima ya mwanamke vikiwasababishia wanawake madhara mengi ya kisaikologia na kimwili ikiwemo vifo, majeraha, kutengwa na kijamii, madhara ya kiuchumi, maambukizi ya maradhi ya kujamiiana nk.

Shambulio la kwanza la aina hii liliripotiwa mkoani Kigoma mwaka 2014 na tangu wakati huo mashambulizi kama hayo yamekuwa yakiongezeka: https://africanarguments.org/…/tanzania-strange-worrying-r…/

Wabakaji na wavamizi hao ambao wenyeji katika maeneo hayo huwaita ‘teleza’ kutokana na tabia yao ya kujipaka mafuta mwilini ili wasiweze kukamatika au kutiwa nguvuni kiurahisi wamekuwa wakivunja nyumba za wakinamama usiku kuwatishia na kuwabaka, wakiwa na silaha na kutoa vitisho na wakati mwingine kuwaacha wahanga na majeraha yanayotishia kuangamiza maisha.

Ripoti za karibuni kutoka kwa Muungano wa azaki mbalimbali zikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Tamasha, Change Tanzania, Kituo cha Mikakati ya Kisheria, JamiiForums, na Twaweza zimegundua zaidi kuenea kwa udhalilishaji huu, ambapo kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wameshashambuliwa na kubakwa.

Matukio haya yanafedhehi waziwazi uhalisia mchugu wa mtazamo wa ubepari kuhusu wanawake, ambapo unamchukulia mwanamke kama kifaa cha kushibisha ladha ya kingono. Kama ubepari unaruhusu na kuhamasisha wanawake kupitia fikra ya “uhuru binafsi”, kutembea uchi, au nusu uchi, kujiuza kwa ukahaba na mwanamke kutumika katika matangazo ya biashara, ni vipi mtu wa kawaida ashindwe kuthubutu kumdhalilisha mwanamke?

Kwa upande mwingine, kunajionesha uhalisia wa udhaifu wa mamlaka husika katika kuwalinda wanyonge na madhaifu kama wanawake hawa waliosibiwa na udhalilishaji huu. Kutokana na udhaifu huu imepelekea baadhi ya wanawake waathirika hata kusitasita kuripoti wanapofanyiwa vitendo hivi.

Zaidi ya hayo, wale wahanga wanaohitaji msaada wa Polisi mara nyingi huwa wako hatarini kudhulumiwa au kutumiwa. Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, muhanga wa makosa ya jinai anayehitaji matibabu hulazimu kupata fomu maalumu ya ya PF3 (kutoka Polisi). Baadhi ya azaki zimedai kuwa wakati mwingine Polisi huwadai wanawake wahanga kutoa rushwa ya pesa ili waweze kupatiwa fomu hizo. Wakati mwingine hata kama wanawake waathirika wameweza kuwatambua wahalifu hao (wabakaji) amma hakuna hatua inayochukuliwa, au wahalifu hao hushikiliwa kwa muda mfupi kisha huachiwa huru.

Ripoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu pia imeangazia kuwa baadhi ya waathirika wa matukio haya ya kikatili wakati mwingine hupuuzwa kamwe na kudhihakiwa.

Katika Uislamu, kinyume na ubepari, kuna mtazamo thabiti juu ya wanawake uliombatana na sheria fafanuzi kulinda na kuhifadhi wanawake na wanadamu kwa jumla. Na hili ndilo suluhisho la kudumu ambalo ubepari unakosa. Ubepari kwa upande mmoja unahubiri ‘uhuru binafsi’ unaohamasisha watu kujihusisha na unyanyasaji wa kijinsia unyanyasaji, na kwa upande mwingine hujifanya kupambana na unyanyasaji huo kinafiki.

Mgongano na mkanganyiko huu wa ubepari ni dhihirisho zaidi la mfumo huu kujifedhehi wenyewe kwa kukosa sifa na uwezo wa kuutumikia ubinadamu (ipasavyo) . Wakati umewadia kwa Uislamu kupitia dola yake ya Khilafah Rashidah kushika nafasi yake.

Imeandikwa na Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania
Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.