Umuhimu wa Hijra

Mwezi wa Muharram ndio mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiislamu. Hivyo basi tunapokuwa tunaingia katika mwezi huu uliobarikiwa ni lazima tujikumbushe kuhusu hijra na vitendo vya Mtume wa Allah alivyofanya kwa ajili ya kuifanya hijra kuwa hijra katika vile alivyovifanya Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم ni pamoja na kutafuta nusra kutoka kwa makabila yenye nguvu, ambayo yangeukubali uislamu na kumsaidia Mtume.
Na msaada huu ulikuja kutoka kwa Answar (ra) ambao waliona hii ni nafasi kubwa kwao kwa kufanya kazi kwa ajili ya Allah سبحانه وتعالى

Wakati wa #Khilafah ya Umar bin al-Khattab (ra) maswahaba (ra) walikubaliana kuanzisha kalenda ya kiislamu mwanzo au kianzio cha kalenda hiyo ya kiislamu iwe ni mwaka ambao Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alifanya hijra (kuhama kutoka makkah kwenda madina) kuelekea Madinah na kuanzisha dola ya kwanza ya kiislamu .
Kwa ushahidi wa seera ya ibn Hisham Mtume صلى الله عليه وسلم alifika madina mnamo tarehe 12th ya Rabi Al-Awwal. Hivyo basi tunapoingia mwezi uliobarikiwa wa Muharram katika mwaka 1440, ni muhimu tuikumbuke hijra na umuhimu wake.

Hijra Ni nukta ya Mageuzi ya kiislamu

Maoni hayajaruhusiwa.